Barua kwa Dr. W. Slaa

Kwa kuongezea tu na kwa msisitizo mkubwa kwako Mh Dr.Slaa...kama unasoma huu ujumbe...please please......kesi hii ina mambo mengi kwani hata kama hamtakata rufaa na mkaamua kumsimamisha Lema...bado kutakuwa na mizenge tele ya delaying tactics.....USHAURI KWAKO DR.SLAA...TAFADHALI WAKUSIMAMISHE WEWE UGOMBEE UBUNGE ARUSHA.CHADEMA WASIMSIMAMISHE MTU MWINGINE ARUSHA ZAIDI YA DR.SLAA.IKUMBUKWE KUWA ARUSHA INA MATATIZO MENGI YA MADIWANI AMBAYO HAYAJAPATIWA UFUMBUZI......PIA ARUSHA NI JIMBO KUBWA TZ.....NA NDIO MAANA CCM WANALITAKA...HASWA JK....HIVYO ASIMAME DR.SLAA MWENYEWE ARUSHA ACHUKUE JIMBO TAFADHALI...ATASAIDIA KUONDOA MIGOGORO ARUSHA KWA KIPINDI HIKI MPAKA 2015....
ANGALIZO: HATA MH.MBOWE ILIBIDI AGOMBEE HAI ILI KULINUSURU JIMBO PAMOJA NA KUWA YEYE NI CHAIRMAN NA ALISHAWAHI KUGOMBEA URAIS...HIVYO SHIME MSIKATE RUFAA NA MSIMAMISHENI DR.SLAA ARUSHA MUIMALIZE CCM.ARUSHA INAHITAJI MTU MZITO KAMA DR.SLAA......LEMA ATAENDELEA KUFANYA KAZI ZA dR.SLAA WAKATI DR.SLAA YUKO BUNGENI........this is my very important suggestion to CDM

Mkuu mimi naipenda sana M4C lakini hapo kwenye red kuna walakini. Lema hawezi kutekeleza majukumu ya Dr. Slaa hata kidogo. Tukubali kila mtu ana umuhimu kwenye chama ila Dr. Slaa kumlinganisha na Lema.... (unanipa maswali sana na uwezo wako wa kuzipambanua siasa za Tanzania)
 
Mimi kwa uelewa wangu mdogo tu ningeona Chadema ikate rufaa kwa sababu hukumu inamapungufu mengi sana

Jaji Mkuu juzi kalalamika mbele ya TV kuwa serikali inaingilia maamuzi ya mahakama. Hukumu hii ina mapungufu kwa sababu serikali ilitaka hiyo hukumu iwe hivyo. Hata wakikata rufaa ikasikilizwa na Othman Chande, bado serikali itaamua vinginevyo.
Mahakama ya wananchi ndo yenyewe kwa nyakati hizi japo ina gharama kubwa. Naamini uongozi wa juu wa CHADEMA leo utatoa maamuzi ya busara na yenye manufaa kwa chama na watanzania wapenda mabadiliko kwa ujumla.
Ntarudi jioni baada ya kusikia M4C imeamua nini.
 
Mkuu Luteni naunga mkono ushauri wako wa CDM kisikate rufaa na kita liretain jimbo la Arusha kwa kishindo kikubwa kuliko 2010.

Lakini kwa vile Chadema ni chama cha kutetea haki, na ile hukumu sio hukumu ya haki kisheria, nashauri Chadema wafanye yafuatayo.

1. Kwanza Chadema iombe expert legal opinion toka kwa wanasheria nguli na mahiri.
2.Kuangalia uwezekano wa kuomba "Stay Off Excecution Order" toka mahakama ya juu wakionyesha intention ya kukata rufaa hivyo mahakama ya juu itatoa "stay order" kwa Lema kuendelea kuwa mbunge mpaka baada ya rufaa yake kusikilizwa!.
3. Kinachotakiwa ni kutumia nguvu za hoja kupata hiyo "Stay Order" na sio hoja za nguvu!.
4. Wakijiridhisha kuwa hili la stay order haliwezekani ndipo waamue wasikate rufaa na wasimsimamishe Lema!. Nimemsikia mkazi wa Arusha akisema hata CCM ingemsimamisha JK mwenyewe na Chadema wakasimamisha jiwe, jiwe litashinda!.

Pasco
Kaka hapo nimekukubali umewaza na kuandika vya msingi sana.
 
safi sana luteni ila wanajamvi nayo mawazo ya pasco ni mazuri kwa upande mmoja! Tuangalie kama stay order itakubalika, then rufaa itawasaidia hata wale watoto wanaosomeshwa na mfuko wa mbunge lema! Tunawaomba sana wanasheria wetu wakae then waaangalie kama hiyo stay order inawezekana au laa, kama haiwezekani hamna kukata rufaa! Arusha sio kama Dodoma, Arusha watu wameenda shule wanazifamahamu haki zao na wajibu wao, yaani hata kama CCM wamweke kikwete Kwenye uchaguzi Wa mbunge Arusha na CHADEMA waweke kivuli bado CHADEMA itashida! Waarusha wanajua sana mambo ya Ukombozi na pia wapo na mungu wakati wote!
 
RIP Lema, huyo ndio kisha katwa mbawa zake.

Matusi na siasa wapi na wapi? rufaa or no rufaa adabu kaipata. Hiyo kesi alijidai kwanza kujipeleka jela, akafikiri atatoka anavyotaka yeye, hakimu akamwambia NO, hapa sio mitaani.

Sasa Lema kapewa haki yake mnalalamika nini?
 
sio majaji wote ni wapuuzi maana hata ile kesi ya mgombea binafsi wapo majaji walioona mgombea binafsi ni halali. Lema na CDM wasikubali huu ushauri wa kutokata rufaa.
 
Nazidi kukazia ushauri wangu kuwa CDM ikate rufaa kwa grounds zifuatazo:

1.Jaji haja fuata utaratibu wa kisheria wa kutoa adhabu. Adhabu ya kusimamishwa kugombea tena hakuitaja, ingawa alitumia s.114, bila yeye kuwa specific ktk kutoa adhabu.(It is fatal per se).

2.Katika hukumu yake alitumia ushahidi wa upande mmoja wa walalamikaji tu.Hakuzingatia wala kuuchambua ushahidi wa wakili wa mlalamikiwa. Kwa tendo hili jaji amekiuka the Golden principal of Natura Justice: The right to be heard (Audi alteram partem).
3.Katika kesi hii ambayo msingi wake(cause of action) ni udhalilishaji, Mtu mwenye na Locus Standi ni Dr. Burian against the whole world. Wa pili ni Lowassa. Hao waliofungua kesi ni wageni(they are strangers).katika kesi za defamation hakuna wa kuirithi.

Tujikumbushe kwenye Law of Torts:
An actionable defamatory statement has three ingredients for it to stand:
i)It must be published.
ii)it must refer to the complainant(plaintiff).
iii)It must be false.

4.Pia jaji ilibidi ajiulize juu ya ukweli au uwongo wa kauli alizosema kwenye mikutano hiyo.Kupima ukweli au uwongo wa hili mahakama ilitakiwa kumuita Dr.Burian na E.Lowassa waje wahojiwe na mahakama na mawakili wa pande zote ili kujua ukweli uko wapi. Pia ulihitajika ushahidi wa kitaalam(expert opinion) i.e DNA test ya mtoto wa Dr.Burian, ili kujiridhisha juu ya baba halali wa mtoto huyo. Ingethibitika kuwa alichosema Lema ni ukweli, basi Lema hangetiwa hatiani kwa sababu ya defense ya JUSTIFICATION(amesema ukweli).

Kwakweli hukumu hii ni kichekesho mtupu. Dawa ni kukata rufaa, si vinginevyo. CDM wakikata rufaa Lema atarudi Bungeni. Labda mahakama ya rufaa ifisadi tena.

Mkuu umetupeleka shule bure, ubarikiwe!
hizo facts ulizozieleza naona kama magamba yanazijua na ndio chambo ili cdm imeze ndoano. hii kesi si ya kusikilizwa na mahakama tena! hii ni kesi ya kusikilizwa na wananchi na hukumu yao ni ya haki, maana ili kuondoa dhuluma hizi wananchi watakifuta ccm kwenye ulingo wa siasa kwa kukifanya kijinyonge kwa kukosa kuungwa mkono, Nashauri yatengenezwe mashtaka vizuri, submision ifanyike kwa wananchi, hukumu itakapotoka watakimbiana zaidi kuliko walivyomkimbia sioi na wao kupoteana kwa aibu. Mahakama hazina thamani tena kwa jamii.
 
lema na CDM kateni rufaa wakati mnajipanga na mambo mengine. Hawa wapuuzi huwezi jua kuhusu zile kesi zingine zilizoko mahakamani. Nia zao kuua upinzani kwa kutumia mahakama.
 
RIP Lema, huyo ndio kisha katwa mbawa zake.

Matusi na siasa wapi na wapi? rufaa or no rufaa adabu kaipata. Hiyo kesi alijidai kwanza kujipeleka jela, akafikiri atatoka anavyotaka yeye, hakimu akamwambia NO, hapa sio mitaani.

Sasa Lema kapewa haki yake mnalalamika nini?

Umempelekea sioi hela ya kutunza familia angalau kwa leo?
 
lema na CDM kateni rufaa wakati mnajipanga na mambo mengine. Hawa wapuuzi huwezi jua kuhusu zile kesi zingine zilizoko mahakamani. Nia zao kuua upinzani kwa kutumia mahakama.

Tutapeleka ujumbe mzito mahakamani, tutachoma moto majengo ya mahakama, wasipotuelewa tutawafuata mahakimu tuwatie adabu.
 
Nazidi kukazia ushauri wangu kuwa CDM ikate rufaa kwa grounds zifuatazo:

1.Jaji haja fuata utaratibu wa kisheria wa kutoa adhabu. Adhabu ya kusimamishwa kugombea tena hakuitaja, ingawa alitumia s.114, bila yeye kuwa specific ktk kutoa adhabu.(It is fatal per se).

2.Katika hukumu yake alitumia ushahidi wa upande mmoja wa walalamikaji tu.Hakuzingatia wala kuuchambua ushahidi wa wakili wa mlalamikiwa. Kwa tendo hili jaji amekiuka the Golden principal of Natura Justice: The right to be heard (Audi alteram partem).
3.Katika kesi hii ambayo msingi wake(cause of action) ni udhalilishaji, Mtu mwenye na Locus Standi ni Dr. Burian against the whole world. Wa pili ni Lowassa. Hao waliofungua kesi ni wageni(they are strangers).katika kesi za defamation hakuna wa kuirithi.

Tujikumbushe kwenye Law of Torts:
An actionable defamatory statement has three ingredients for it to stand:
i)It must be published.
ii)it must refer to the complainant(plaintiff).
iii)It must be false.

4.Pia jaji ilibidi ajiulize juu ya ukweli au uwongo wa kauli alizosema kwenye mikutano hiyo.Kupima ukweli au uwongo wa hili mahakama ilitakiwa kumuita Dr.Burian na E.Lowassa waje wahojiwe na mahakama na mawakili wa pande zote ili kujua ukweli uko wapi. Pia ulihitajika ushahidi wa kitaalam(expert opinion) i.e DNA test ya mtoto wa Dr.Burian, ili kujiridhisha juu ya baba halali wa mtoto huyo. Ingethibitika kuwa alichosema Lema ni ukweli, basi Lema hangetiwa hatiani kwa sababu ya defense ya JUSTIFICATION(amesema ukweli).

Kwakweli hukumu hii ni kichekesho mtupu. Dawa ni kukata rufaa, si vinginevyo. CDM wakikata rufaa Lema atarudi Bungeni. Labda mahakama ya rufaa ifisadi tena.
moma2k ni shule nzuri lakini nikuulize swali dogo tu, unafikiri hayo yote Jaji hayajui?
 
Luteni Big up, umefanya kazi yako wanaolalama waache walalame bila jasho. Naomba tusaidieni hati ya hukumu kama mnayo tafadhali sana.

Ushauri ni muhimu maana najuwa CDM wanayo timu nzuri ya wanasheria ambao kupitia mashauri mbali mabali kama haya yako wataweza ku chambua na kuainisha wafanye nini.

Kama uilivyosema kuna mbinu chafu lakini hakika hazitaijenga CCM badala ya kuibomoa na kuiteketeza milele na mwisho wa siku wataanza kutumia mbinu za kivita na kuitumia Jeshi kabisa na hapo ndipo mwisho wao utakuwa umefika kikomo.
 
sio majaji wote ni wapuuzi maana hata ile kesi ya mgombea binafsi wapo majaji walioona mgombea binafsi ni halali. Lema na CDM wasikubali huu ushauri wa kutokata rufaa.
Unaweza kutukumbusha ile kesi iliishaje.
 
Mkuu mimi naipenda sana M4C lakini hapo kwenye red kuna walakini. Lema hawezi kutekeleza majukumu ya Dr. Slaa hata kidogo. Tukubali kila mtu ana umuhimu kwenye chama ila Dr. Slaa kumlinganisha na Lema.... (unanipa maswali sana na uwezo wako wa kuzipambanua siasa za Tanzania)

kama nimemuelewa vizuri alimaanisha shughuli za uhamasishaji, si ukatibu mkuu, NAWEZA SAHIHISHWA.
 
Mkuu luteni.umenena haya mawazo mwandikie Dr Slaa nakala mpe Mh lema ikiwezekana prnt na michango yetu humu wape.Lema anatakiwa kuweka maslai ya watanzania mbele kuliko ya kwake.wadau ktk hili wote mliochangia mmeweka ushabiki pembeni na kuzungumza kama watanzania,tuwe na uwezo wa kufikiri bila ushabiki wadau
 
Mimi naomba nitofautiane na Luteni, Nanaomba tukate Rufaa, unajua hukumu haiko sawa, na chama chetu ninaamini tunapenda kukiendesha kwa misingi ya kufuata sheria, short cut ni za CCM tusizifuate, Mungu atakuwa upande wetu na kila mtu mwenye hekima anaelewa jinsi hukumu hiyo ilivyo, ni ya Hovyo ambayo hata hakimu wa kijiji hawezi hukumu hivyo!

Naomba tukate rufaa na tutashinda, Augustine Ramadhani siyo Jaji Mkuu, Rufaa itasikilizwa vizuri tuu!
 
Kuna yaliyo wazi ya kukata rufaa na ya kutumia busara sheria is not everything.
 
Natumaini CDM watakuja na option nzuri. Kuna vichwa, wanasheria, wenye busara zao and together we can make something so meaningful. Sio kama magamba kuna Walozi, waongo, wazinzi, watukanaji, walafi na kila aina ya wavunja amri kumi za Muumba, ukicombine hapo nafikiri mnajua hybrid atakaetoka hapo.
 
Back
Top Bottom