He,
mdogo wako kumbe ziro hivyo , sasa nimeelewa kwa nini post zako huwa za ajabu ajabu!
Nimepokea barua hii toka kijijini naomba msaada wa hali na mali kumwezesha DOGO. Nitawatumia namba wale tu waliotayari kusaidia tu siyo wale wanaokebehi
View attachment 55648
Hii dunia ina vituko sana, huyu kijana ndo kwanza kamaliza shule na kupata division four, analalamika kuwa wenye divison one wanaendelea na masomo, alitegemea hao wenye div one waachwe achukuliwe yeye mwenye four???
Anyway back kwenye kuomba mchango, anakimbilia nini kuoa angali hana hata hela ya kuanzia maisha baada ya kuoa? Mke atamtunza vipi? Na ataimudu vipi familia yake?
Mshauri kama ana nia ya kusoma, arudi shule ku-reseat mitihani yake na kama hana mpango wa shule, atafute shughuli za kufanya kama biashara au mambo ya kilimo. Kwa elimu ya form four, kuna shughuli nyingi tu anaweza kufanya na zikamuungizia kipato badala ya kukimbilia kuoa.
Binafsi ningeshawishika kumsaidia kama angeniomba mchango wa ada na gharama za kurudi shule au namna ya kuanzisha biashara, vinginevyo nasikitika sintaweza. Anisamehe bure.