Barrick wasimamisha mgodi.

Infopaedia

JF-Expert Member
Oct 28, 2011
1,231
1,487
Kampuni ya African Barrick Gold imeusimamisha mgodi wake wa Bulyanhulu kwa masaa 48, kuanzia jioni ya August 1st. Uongozi wa Bulyanhulu umechukuwa uamuzi huo jioni hii baada ya mgomo wa siku mbili wa wafanyakazi. Mgomo huo ambao ulianza jana asubuhi July 31st ulisababishwa na sheria ya kufuta fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Baada ya wafanyakazi kuona uongozi wa Barrick Bulyanhulu umelala sana na hakuna jitihada zozote za kupata official reports from SSRA. Jana asubuhi wafanyakazi wakaamuwa kuanzisha mgomo mpaka hapo watakapoitiwa watendaji wa juu wa SSRA ili waelezwe na wafafanuliwa juu ya mafao yao na wao kutoa kilio chao juu ya hiyo sheria mpya. Baada ya wafanyakazi kukusanyika na kujadili. Ilionekana ni bora aje mbunge Jafu ambaye anakusanya maoni, au Waziri wa Kazi. Lakini uongozi ulifanya jitihada na kumleta Afisa uhusiano wa SSRA toka Dar office. Afisa uhusiano aliondoka bila kutowa jawabu la kuridhisha kwa wafanyakazi. Hivyo wafanyakazi waliamuwa waendelee na mgomo mpaka atakapoletwa Jafu au waziri mwenye dhamana. Hivyo wafanyakazi wakaendelea na mgomo mpaka wakati wa kutoka jioni. Jioni waliukabidhi mgomo kwa wafanyakazi wa zamu ya usiku. Zamu ya usiku waliupokea mgomo kwa mikoni miwili na kuahidi mgomo watauendeleza mpaka asubuhi na kuwarudishia waasisi wa mgomo huo. Kweli bwana, pamoja na vitisho vyote toka utawala, lakini jamaa wa usiku waliendelea kukaza uzi mpaka asubuhi. Ilipofika leo asubuhi, waanzilishi wa mgomo walikuja kupokea mgomo wao. Shift ya leo asubuhi iliendelea na mgomo huku mijadala na uongozi ikiwa inaendelea. Lakini wafanyakazi wakashikilia uamuzi wao wa kuonana na Jafu ama waziri mwenye dhamana. Ulipofika muda kama wa saa kumi na moja jioni, uongozi ukatoa taarifa kwa wafanyakazi wote. Kwamba uongozi umeamuwa kusimamisha shughuli za uchimbaji kwa masaa 48 kuanzia muda huo wa jioni. Wafanyakazi ambao ilibidi waingie kwa zamu ya usiku jioni hii hawakuingia kazini. Na waliokuwepo walirudi nyumbani kusubiri kwa masaa 48. Nje ya geti wafanyakazi walikuta police wakiwa wametawanywa. Lakini hakukuwa na tukio lolote la vurugu ama utumiaji nguvu. Wafanyakazi waliingia kwenye ma-bus ya kampuni na kurudi nyumbani kwa amani.
Source: Shuhuda wa tukio.
 
Katika habari hii, nimependa mwandishi ulivyoripoti kuhusu kukabidhiana shift ya mgomo, nimeipenda sana."Hivyo wafanyakazi wakaendelea na mgomo mpaka wakati wa kutoka jioni. Jioni waliukabidhi mgomo kwa wafanyakazi wa zamu ya usiku. Zamu ya usiku waliupokea mgomo kwa mikoni miwili na kuahidi mgomo watauendeleza mpaka asubuhi na kuwarudishia waasisi wa mgomo huo. Kweli bwana, pamoja na vitisho vyote toka utawala, lakini jamaa wa usiku waliendelea kukaza uzi mpaka asubuhi. Ilipofika leo asubuhi, waanzilishi wa mgomo walikuja kupokea mgomo wao."
huko North Mara nako mambo sio mambo, vijana wameendeleza mgomo wa kudai malundo (hela) yao.



"KWA PAMOJA TUTASHINDA MSIOGOPE"
 
Huo Mgodi una faida gani kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuneemesha huko majuu!
 
nawashauri wasirudi kazini mpaka wapate maelezo yanayoridhisha kuhusu hela zao
 
hao barrick wana bahati mie nipo mapumziko, yaani ningekuwa mtingoni, wangekoma na show zangu, lakini naamini vijana wamewakilisha vizuri.

KAMWE MSIRUDI NYUMA VIJANA KATIKA KUDAI MARUNDO YETU
!
 
hongereni sana wanangwamba..sio migomo ya akina Mgaya na Mkoba, natamani Rwegasira wa TRL angekuwa hai
 
Nchi inapita katika kipindi kigumu sana,yaani kila sehemu migomo! Tukisoma alama za nyakati inaashiria kuchoka kwa wananchi walio wengi na siasa za usanii wa nchi hii! Nahisi hatari mbeleni!
 
Kazeni buti jamani mpaka kieleweke. Wenzenu wa Resolute Golden Pride Nzega wameahidiwa kulipwa mafao yao. Barua imetumwa na SSRA, sababu eti kwa kuwa wanafunga mwaka huu. Wezi hao tusikubali. PIPOOOOOOS POWER.
 
FFU hawajafika mgodini tu? Changing times the people have spoken, Mwema wiil deploy hadi basi .
 
Nadhani kwa huko serikali itachukua hatua maana migodi ya wakubwa hiyo!
 
FFU hawajafika mgodini tu? Changing times the people have spoken, Mwema wiil deploy hadi basi .


Mfanyakazi mmoja wa mgodi mshahara wake unalipa askari wa defender wote
Huko hawawezi kutumia nguvu kabisa wanaonea walimu na wanafunzi tu!
 
km ni POLISI wa Tanzania wajue wakiwapiga hao wafanyakazi km walivyowafukia wachimbaji wadogowadogo kule Kahama MUNGU atawalaani kwani na wao yatawakuta
 
Mi nawaonea huruma hawa wafanyakazi maanake wanachezea hela ya mzungu na ukichezea hela ya mzungu, pia unachezea hela ya house boy wake pale wizarani, matokeo yake tutasikia tuu, mtu kibao wamepoteza maisha kisa wamekosa adabu na kufanya fujo kazini. Ebwanaee cheza mbali na maswala ya madini, hii kampuni ya barricks si juzi juzi tu walifukia wachimbaji wadogo wadogo naomba mtu anikumbushe ilikuwa mgodi gani tena? Nawaomba wote mnaogoma, tafadhali msilogwe mkainigia ndani ya mgodi kugoma maana itakuwa last time unaona mwanga wa jua, utafukiwa live mwanangu. Wote twafahamu madai ya mzungu yanapewa tija punde linapolalamika kwa nguvu za dola, tena adhabu ya kumsumbua mzungu ni kali kuliko umsumbue mbongo mwenzako. Hata nchi za watu (ie USA), weusi wanafahamu ya kwamba usicheze na mzungu. Nilipata fursa kusoma biography ya black mmoja jina lake Nathan McCall (Makes me wanna holler), story yake ilinisaidia sana kuelewa game la ulaya. Jamaa akiwa gangster flani aliwahi gombana na blaki mwenzake jambo lakipumbavu tu, akampiga shaba ya kifua nusura amuue jamaa, kesi ilikuwa chamtoto hamna noma wala nini akaachiwa. Muda ukapita kidogo Nathan akaenda kuvamia duka fulani ambako mzungu alikuwa meneja, hakupiga mtu yeyote risasi wala nini, alichomoa chuma akawaambia kila mtu lala chini. Ebwanaee, soo lililozuka kumchomolea mzungu bastola ilimpa kifungo cha miaka kadhaa ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa. Sasa kwa mtazamo wangu, nawashauri hao wafanyakazi wa Barricks wasambaratike na kurudi makwao yaani msikutwe eti mnagoma kazini kwa mzungu, hii ni ngoma ambayo hutaki kucheza mziki wake.
 
hao barrick wana bahati mie nipo mapumziko, yaani ningekuwa mtingoni, wangekoma na show zangu, lakini naamini vijana wamewakilisha vizuri.

KAMWE MSIRUDI NYUMA VIJANA KATIKA KUDAI MARUNDO YETU
!

Usiwe na wasiwasi mkuu. Show ilikuwa kali kama kawaida ya show za ma-miner. Mgodi ulikuwa unaongozwa na Michael kiredio kwa siku 2. Si unakijuwa kile kichwa cha conventional lakini. Halafu picha linaanza. HR manager Mzee Mtumwa Mfikirwa kaja kusikiliza watu wanadai nini. Si unajuwa miner walivyo na hasira na yule mzee na wanamtafuta siku nyingi. Wacha kabisa. Mfikirwa alipewa maneno yake nusura ya kutiwa vidole vya macho. Yule mzee hatosahau vichwa vya underground. Watu wanasubiri masaa 48 yaishe.
 
Back
Top Bottom