nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,369
Na bado wana airport ndani ya migodi, so we are not sure kama kweli hawasafirishi madini bila kuya account. Kaazi kweli kweli.
Hawa Jamaa hawata kaa na kuripoti faida hata siku moja kwenye mahesabu yao. Mimi nimeshakuwa consultant katika migodi ya Barrick and Angro, hawa ni wahuni sana. Wanatransfer faida mapema sana kwa kutumia manunuzi. Yaani wananunua spares na Equipment toka kwenye makampuni tanzu yao kwa bei za juu sana. As a result wanakuza expenses kwenye mahesabu, na kushusha faida. Mara nyingi wanatumia sana non tangible assets kama Computer Softwares na kadhalika, ambazo wanajua TRA au Watz wanashindwa kujua gharama halisi. Utakuta wanaweza kubadili software kila mwaka. Wanatumia consultancy services za kutoka kwenye kampunzi tanzu zao kwa bei kubwa hata kama utaalamu huo unaweza kupatikana nchini. Tatizo la Viongozi wetu hata ukiwatonya, ndio kwanza wao wanaenda kuvujisha siri iliwavute chochote. Kutrace hasabe zao ni vigumu sana kwani Ofisi za wahasibu zinafanywa nje ya nchi, hapa wahasibu kazi yao ni kuscan document na kusend basi.