Barclays Bank (Tanzania) yafunga matawi 10 nchini

Nyambaffu...mtu wa Pemba anahamishiwa akaunti Unguja. Wa Tabora hadi Mwanza. Na serikali imetulia tu. Inasubiri uchaguzi

Hapo utasikia wanataka kuunda tume kuchunguza..... Kiukweli ni uonevu mkubwa sana
 
Hizi bank hazikuanzishwa kuwahudumia wananchi, ni mabepari pekee sasa bongo mabepari pia wanabank zao kama wangekuwa na flexibility wa kututazama wagonga nyundo soko lipo na wangekuwa sana tu lakini kung'ang'ania wavaa tai tu siku hizi hata wachuuzi ado ado wana umate mate.

R.I.P them all
 
Ndo uchumi unakua hivyo kweli kama sio Taifa linaangamia hili ewe mungu wangu ajira ndo zinazidi kuwa mbinde hivyo
investors wote wanaoamini kuwa maendeleo ya nchi yanaletwa na ulipaji kodi vizuri wanapoteza imani.
Mfano angalia hapa kuna BP, Chevron na sasa Bacrays. Ngoja tusubiri kama tutaona mwisho wa haya yote
 
Nimeguswa sana na hili suala la restructiring ya Barclays Bank, kwa upande moja kama wanadhani kuwa kwa kuchukua hatua hizo itakuwa ni kuboresha huduma zao basi naamini kila moja angeunga mkono.

Lakini ukifanya tathmini utaona kuwa ni kinyume chake. Hakuna ufanisi wowote unaotegemewa kwa kumhamisha mteja toka Tabora au Musoma na kumpeleka Mwanza. Mteja alipofungua account kwenye tawi husika alikuwa anategemea unafuu hata kwa muda atakaotumia mara anapohitaji huduma za kibenki. Leo unamhamishia mkoa mwingine bila kujadiliana naye kama anaridhika ama laa ni uhuni ambao unapaswa ulaaniwe na kila anayeitakia nchi yetu mema.
 
Matatizo ya Barclays yamesababishwa na watu wa Emerging Markets Dubai kulazimisha Retail expansion huku Tanzania wakifikiri bongo ni Botswana,Kenya au South Africa. Matokeo yake ndio haya sasa halafu wanaoumia ni watanzania.
 
Barclays Benki kubwa duniani haiwezi kukimbia kama hivi vibenki vidogo vidogo.

Kwa takriban miaka 3 iliyopita Barclays Tanzania ilikuwa inaendeshwa kwa hasara lakini bado ipo.
 
Leo wametoa ufafanuzi.

Wanadai si uamuzi rahisi waliouchukua lakini lengo ji kuboresha huduma zao, utendaji na kufanikisha malengo yao ndani ya Tanzania.

Tatizo kubwa wanaonyesha ni hali ya kijiografia ya Tanzania iliyowaathiri katika utendaji.

Wafanyakazi zaidi ya 100 wataathirika na maamuzi haya japo wameahidi kuwa wafanyakazi hawa watalipwa stahiki zao.

Matawi yanayofungwa na yasiyo na matawi mbadala karibu basi watapewa notisi ya siku 90.
 
Wanadai Barclays Tanzania iko chini ya Barclays na ni washindani na NBC, wanasema hakuna kununuliwa au kuinunua NBC.

Wanasisitiza, issue ya Personal loans haijapelekea kutetereka kwao kibiashara.
 
Wanasema, Barclays ndo ilikuwa bank kubwa ya 4 baada ya CRDB, NBC na NMB. Swali la accounts zao kuonyesha kuporomoka kibiashara limejibiwa kijanja, ufafanuzi haujatolewa vema lakini wanasema 1st quarter haikuwa nzuri lakini ilikuwa impressive.
 
duh,walifungua matawi kwa pupa,wakatapakaa ghafla,sasa sijui ilikuwa ni deal ya mtu?,maana waTZ hatupewi mwanya
 
Wameulizwa:

Kupanuka kwa bank kunawapa matumaini wateja, kuanza kufunga matawi kunawatisha wateja na hivyo hata ambao hawataathirika kuamua kufunga akaunti zao, watajisafishaje kwa wateja?

Wamekiri wanaelewa kuwa wateja wataathirika sana na maeneo mengine watafunga kabisa, watajitahidi kuwaelewesha wateja wao wanaobakia juu ya maamuzi yao. Wanadai hawajapoteza 'credibility' na wataendelea kuwepo Tanzania na hivyo wateja wataeleweshwa kilichofanyika. Wanasema wanajua kuwa wateja wengine watakimbilia benki nyingine.

Wameulizwa pia athari kwa wafanyakazi ambao wanapoteza ajira, watawasaidiaje?

Wanasema wameshaongea nao na kuwaelewesha hatua zinazochukuliwa.
 
Wameulizwa:

Watafunga matawi mengine lini?

Wameeleza kuwa hawawezi kutabiri kilicho mbele, wanaweza kufungua matawi mapya siku za usoni au kufunga mengine kulingana na biashara itakavyohukumu.
 
Maelezo ya Bwana mkubwa Kihara Maina yana Pointi tatu muhimu kulingana na East Africa Herald. 27/5/12
1. Uamuzi umetokana na kuhakikisha huduma zinatolewa kulingana na matarajio.
  • Majibu yetu-Hebu tumuulize, Matarajio ya nani hayo? (kastama sevice yako iko wapi) inatakiwa kufikia matarajio ya wateja. Au ni matarajio ya akina nani hao

2. Tunalenga kuboresha huduma zetu, utendaji na kufikia malengo kabambe ya utendaji kazi.
  • Kuboresha gani huko wakati unaondoa huduma na kuwavugumiza kwenye matawi ya mikoa ya mbali, halafu hayo malengo yana ukabambe gani wakati serikali jiondoa katika biashara za benki kwa matarajio nyie mtahudumia wananchi. Leo mnafyatuka na kuacha mabibi wazee kwenye mataa, kwanini mlinunu benki za serikali? Unaonaje serikali iwa chenjie kagali na ninyi?

3. Kupunguza usumbufu kwa wateja zetu na wafanyakazi walioathiriwa ni lengo lilo pewa kipau mbele na tumechukua hatua muhimu za kiofisi kupunguza uhasi umeoletwa na mabadiliko haya.
  • Ni dhahiri kabisa unachofanya bwana Kihara ni tofauti na unavosema. Umeongeza usumbufu mkubwa kwa weteja wa hizo sehem unazofunga matawi. Na kwa upande mwingine, wafanyakazi unawaachisha kazi ghafla, washike mti gani. Wengine wana watoto, wazee, wagonjwa. Wewe ni mwafrika kweli. Haujui kazi moja hapa east afrika ina sapoti nusu mtaa. Wahumieni wateja na wafanyakazi, tuwasaidia kuongeza wateja kwenye hizo branchi kama ndio chalenji kuhama.

http://www.eastafricaherald.com/2012/05/barclays-to-close-10-branches-in.htmlhttp://www.eastafricaherald.com/2012/05/barclays-to-close-10-branches-in.html
 
Ukweli ni kwamba Barclays mmekurupuka katika hili la kufunga matawi, hamkushirikisha wateja wenu, hamkufanya utafiti kabla ya kufikia uamuzi huu, hamjawatendea haki, ustaarabu wala uungwana wateja wenu. Hii ni sawa na Baba mwenye nyumba kutoa notisi kwa mpangaji wake ahame nyumba yake haraka bila ya kumpa mpangaji nafasi atafute nyumba ingine.

Hivi kweli umtoe mteja Tabora umpeleke Mwanza zaidi ya kilometa 100 eti anafata Benki ya Barclays!!!!!!. Huu ni Uhuni.
 
Kwa mujibu wa taarifa toka ndani ya Benki ya Barclays zilizotangazwa na vyombo kadhaa vya habari nchini,benki hiyo ipo mbioni kufunga baadhi ya matawi yake hapa nchini zoezi litakaloambatana na kupunguza wafanyakazi zaidi ya mia moja.
Ndugu zetu watakaokumbwa na kadhia hiyo waanze kujiandaa kisaikolojia kukaa bench.
 
Wanasema, Barclays ndo ilikuwa bank kubwa ya 4 baada ya CRDB, NBC na NMB. Swali la accounts zao kuonyesha kuporomoka kibiashara limejibiwa kijanja, ufafanuzi haujatolewa vema lakini wanasema 1st quarter haikuwa nzuri lakini ilikuwa impressive.
Impressive kivipi?
Seems wawekezaji hawa wanaficha real story of their fate.
 
Nyambaffu...mtu wa Pemba anahamishiwa akaunti Unguja. Wa Tabora hadi Mwanza. Na serikali imetulia tu. Inasubiri uchaguzi
Sasa wewe ulitaka serikali ifanye nini?Unajua soko huria...Benki zimejaa,unahama mara moja,wametoa siku 90 watu wajipange,what else do you want?.Tutaacha lini hii mentality ya 'serikali itusaidie wananchi' lini?Dereva anaendesha basi kwa fujo,abiria wote wanakaa kimya lakini gari likipata ajali utasikia kila abiria akisema 'Tunaomba serikali iingilie kati kutusaidia...'.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom