Barcelona yatua London, Arsenal yaipa uwanja

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
TIMU ya Barcelona iliwasili juzi usiku mjini London kwa ajili ya kukabiliana na Manchester United katika mechi ya fainali ya kuwania ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Wembley.

Barcelona iliondoka mjini Barcelona ikiwa ni siku mbili kabla ya ratiba waliyokuwa wamejipangia kuondoka na kutua mjini London, ambapo awali walikuwa wamepanga kufanya mazoezi siku ya Jumanne na Jumatano mjini Barcelona kabla hawajasafiri kuelekea mjini London.

Hata hivyo, Barcelona ilibidi wabadilishe ratiba yao kwa sababu ya volcano inayotoa majivu huko Iceland hivyo kubadili hali ya hewa na kutishia anga la England.Timu hiyo ya Barcelona iliwasili mjini London baada ya kusafiri angani kwa muda wa saa mbili ilipotua kwenye uwanja wa ndehe wa Stansted ilikwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya The Grove ambayo wameandaliwa.

Jana timu ya Barcelona ilitarajiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mazoezi wa Arsenal ambayo imekubali kuipatia timu hiyo uwanja kwa ajili ya mazoezi London Colney."Arsenal wameonyesha ukarimu wa hali ya juu baada ya kutukubalia kufanya mazoeozi kwenye uwanja wao kwa siku za Jumatano na Alhamisi,"alisema msemaji wa Barcelona.

Alisema,"tulipojua tunakuja England tofauti na tulivyopanga tuliwapigia simu Arsenal ambao walikubali maombi yetu."
Timu hiyo ya Barcelona kabla ya kusafiri ilifanya mazoezi yake kwa muda kadhaa kabla haijasafiri, huku zikitolewa taarifa kuwa Gaby Milito ambaye alikuwa majeruhi hivi sasa yupo fiti kwa ajili ya mechi hiyo ya fainali.

"Ili kuepuka kuvuruga ratiba ya mechi kwa sababu ya matatizo yaliyopo hivi sasa ya volcano Grimsvotn kuchafua anga na kutishia pia anga la England, uongozi wa timu ya Barcelona uliamua tufasiri mapema na ndivyo tulivyofanya,"ilisema taarifa ya Barcelona.

Kutokana na volcano hiyo kusumbua nchi mbali mbali za Ulaya mpaka sasa zipo safari mbali za ndege ambazo zimeahirishwa kwa kuhofia usalama na mali za abiria.

Akilizungumzia suala hilo, kocha wa Barcelona, Pep Guardiola alisema tatizo hilo linaweza kuzipa matatizo timu zote mbili, pia alisema linaweza kuwasumbua sana mashabiki ambao wengi wao hupenda kusafiri siku ya mechi.

Hata hivyo Guardiola alisema anatarajia UEFA itaendelea na ratiba yake kama ilivyopanga hata kama mashabiki wengi watashindwa kusafiri kwa sababu ya madhara ya volcano.

"Tutacheza mechi hata kama uwanja utakuwa hauna mashabiki wengi, ingawa itahuzunisha sana, tuombe Mungu Volcano isiwasumbue wasafiri wote wanaotaka kusafiri na kushuhudia mechi,"alisema Guardiola.

Mwaka jana Barcelona ililazimishwa kusafiri kwa njia ya basi mpaka mjini Milan kwa ajili ya kucheza mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan kwa sababu anga lilikuwa limechafuka na ndege kuzuiwa kuruka kwa sababu ya majivu kutanda mawingu huko Ulaya Magharibi. Katika mechi hiyo Inter Ilishinda 3-1.
 
All the best Barca, hop Barcelona itashinda hiyo match kwa idadi kubwa ya magoli!
 
Sio kila siku ni jumapili ukiona kobe kainama moto lazima uwawakie barcelona watakula goli mbili kavu.

Mapinzani wetu wote kwenye EPL wapo Barca. Nawashangaa sana Arsenal kutolewa katika haya mashindano na Barca lakini bado wanawashngilia

Subirini muone tutakavyowafanya hao Barca.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom