Baraza la wazee wenye hekima kitaifa lahitajika

mwalimu Jr.

Member
Aug 20, 2008
51
4
NDUGU ninaamini kwamba ingawa hatuwezi kuwa na baba wa Taifa mwingine lakini kuna viongozi wenye heshima zao ambao wanatumika na nchi za nje wanaostahili kuishauri serikali, vyama vya kisiasa na watu wengine ili nchi iendelee kama ilivyoanza.

Watoto wadogo sasa hivi wameanza kujipa busara na hekima ambazo hawanazo. Hii ni kwa sababu kuna ombwe. Viongozi wetu vijana wanawaweka wazee kando kama vile wazee hao hawana chochote cha kuchangia kuhusu hatima ya nchi hii.

Hivi unaniambia baraza likiwa na watu kama Mzee Jumbe, Mzee Kawawa, Mzee Msuya, Mzee Mwinyi, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Warioba, Mzee Malecela, Mzee Gharib, Mzee Mwiru, Mzee Mengi, Mzee Bakhressa, Mzee Gulam Mohammed, Mzee Baghdad na watu kama hawa kweli tutakosa busara na hekima katika kufanya maamuzi yetu. Tusije tukageuka sungura kuwazika wazee wetu wangali hai kisha tujikute hatuna wa kutushauri.
 
Watu wenye busara sio lazima wawe wazee wanahitajika watanzania wenye uchungu na nchi yao na wasiokuwa wanafiki na wanaoweza kusema ukweli bila kuogopa maslahi yao it might not be possible to find them in this country so we can hire them and pay them to say the truth and help us not rob our people.
 
Mkuu hapo uko off the line, hao unaowasema si waliwahi kuwa viongozi wetu wa taifa, sasa kama wana busara za kutusadia now ilikuwaje hawakuziweka walipokuwa kwenye power, maana tusingefika hapa eti, au?
 
Back
Top Bottom