Baraza la michezo tanzania kuunda kamati ya muda "tennis association"

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,320
Baraza la michezo tanzania kupitia mwenyekiti wake Malinzi, limefikia uamuzi wa kuunda kamati ya muda ya watu wasiopungua 8 ambayo pamoja na mambo mengine itaratibu na kuitisha uchaguzi wa chama cha mchezo wa tennis tanzania, kusimamia chama katika kipindi cha mpito ambacho kitakuwa ni mwezi mmoja kwa mujibu wa taarifa za uhakika toka chanzo makini.
maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na malalamiko yaliyopelekwa na wadau wa tennis wakilalamikia viongozi kukaa madarakani bila kuitisha uchaguzi kwa zaidi ya miaka 10 (kumi) sasa.
katika kikao kilichofanyika awali, katibu mkuu wa TTA Inger Njau pamoja na mwenyekiti wake Denis Makoy walikiri mbele ya MALINZI kuwa kimsingi wanaongoza chama bila ridhaa ya wanachama (wadau).
katika maamuzi hayo wafuatao wameteuliwa kwenye kamati ya muda ambao watafanya kazi sambamba na uongozi uliopo katika kipindi hiki cha mpito;

JOHN BURA m/kiti
TANGO . . . . . katibu
SALUM MVITA - mjumbe
ISMAIL . . . . . . - mjumbe
VICKY CHUWA - mjumbe
HASSAN . . . . . - mjumbe

majina na orodha kamili itafahamika baada ya barua kuandikwa na kukabidhiwa rasmi kwa wahusika.

Naomba kuwasilisha.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom