HISIA KALI
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 694
- 108
mwanakijiji sidhani kama tatizo la masha au ngeleja au kijana yeyote lilitokana na in experince yao ya siasa. Nitakubaliana na wewe ukisema masha na ngeleja walikuwa hawana experince ya kusafisha siasa na maamuzi mabovu yaonekane kama ni maamuzi mazuri machoni pa jamii.
Kusimamia haki, maadili ukweli na uzalendo hakuitaji experince . Kusimamia na kuongoza opposite yake ndio kunaweza kuhitaji experince. Hata huyo mama tibaijuka hiyo wizaraya ardhi hawezi kupewa kwa hofu ya kuwaumbua vigogo wengi. Ataishia kupewa wizara ya jinsia
Masha na Ngeleja walivimba sana vichwa wakajiona kama miungu watu na kudharau wananchi. Mnakumbuka issue ya ngeleja na yule masikini mlinzi wa atm aliyekuwa analinda eneo lenye atm?. Mlinzi baada ya kuona kuna mtu yuko kwenye atm anaongea na simu badala ya kuchukua pesa alienda akamwambia kuna watu wengi wanasubiri huduma wapishe. Yule mlinzi alikuwa na moyo safi wa kusaidia wateja wapite huduma. Lakini ngeleja kwa kulewa madaraka ya uwaziri alimtukana yule mlinzi matusi na kumtishia maisha. Kwa taarifa za mwisho tulizopata yule mlinzi alifukuzwa kazi.