Baraza la mawaziri na watoto wa vigogo

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3][/h]

Makamba2(5).jpg

Katibu mkuu wa zamani wa CCM Yusuf Makamba aliwahi kujivuna kuwa amezaa watoto wenye bongo na hivyo lazima mwanae awe waziri. Kikwete alipovunja baraza la mawaziri kutokana na kipenzi rafiki na mshirika wake Edward Lowassa kusombwa na kashfa ya Richmond, alimuacha nje January. Hii ilifanya watu tumzodoe Makamba kuwa yako wapi tusijue kuwa waarabu wa Pemba hujuana kwa viremba! Sasa January pamoja na uteke wake ni waziri. Anazidi kutunisha namba ya watoto wa wakubwa walioridhi ukubwa wa wazazi wao. Leo tuna Emanuel Nchimbi mtoto wa kigogo wa zamani wa CCM, January Makamba kadhalika, Adam Malima mtoto wa swahiba mkubwa wa rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye mwanae ni waziri wa Afya na Hamis Kageshiki mkwe wa Mwinyi. Kimsingi, Makamba hakutabiri wala kubabaisha bali alijua walivyo na hisa kwenye serikali hii ya kishikaji ya kujuana na kulindana ukiachia mbali kulipana fadhili kwa mgongo wa jasho la mlipa kodi maskini. Ubaya ni kwamba wale wasio na hisa walipopewa madaraka wakajisahau kuwa hawakuwa na hisa. Hii ndiyo siri ya kubakizwa kwa watu kama Adam Malima ambaye alishirikiana na William Ngeleja kuhujumu uchumi. Kadhalika Dk. Hussein Mwinyi ambaye mabomu yaliua watu chini ya uangalizi wake na akashinikizwa ajiuzulu akagoma kwa kujua shea za baba yake kwenye serikali. Kadhalika Emanuel Nchimbi anayekabiliwa na shutuma za kughushi vyeti vya kitaaluma. Hawa ni watoto wa wenye hisa hawaguswi wala hawastuki hata wakikosea vipi.
 
Naunga mkono hoja,

kweli kuna undugu na kubebana sana kwenye vyama vya siasa!

We mwanzilishi anamkabidhi mikoba mkwe wake awe mwenyekiti unafikili ni sahihi kweli?
 
[h=3][/h]

Makamba2(5).jpg

Katibu mkuu wa zamani wa CCM Yusuf Makamba aliwahi kujivuna kuwa amezaa watoto wenye bongo na hivyo lazima mwanae awe waziri. Kikwete alipovunja baraza la mawaziri kutokana na kipenzi rafiki na mshirika wake Edward Lowassa kusombwa na kashfa ya Richmond, alimuacha nje January. Hii ilifanya watu tumzodoe Makamba kuwa yako wapi tusijue kuwa waarabu wa Pemba hujuana kwa viremba! Sasa January pamoja na uteke wake ni waziri. Anazidi kutunisha namba ya watoto wa wakubwa walioridhi ukubwa wa wazazi wao. Leo tuna Emanuel Nchimbi mtoto wa kigogo wa zamani wa CCM, January Makamba kadhalika, Adam Malima mtoto wa swahiba mkubwa wa rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye mwanae ni waziri wa Afya na Hamis Kageshiki mkwe wa Mwinyi. Kimsingi, Makamba hakutabiri wala kubabaisha bali alijua walivyo na hisa kwenye serikali hii ya kishikaji ya kujuana na kulindana ukiachia mbali kulipana fadhili kwa mgongo wa jasho la mlipa kodi maskini. Ubaya ni kwamba wale wasio na hisa walipopewa madaraka wakajisahau kuwa hawakuwa na hisa. Hii ndiyo siri ya kubakizwa kwa watu kama Adam Malima ambaye alishirikiana na William Ngeleja kuhujumu uchumi. Kadhalika Dk. Hussein Mwinyi ambaye mabomu yaliua watu chini ya uangalizi wake na akashinikizwa ajiuzulu akagoma kwa kujua shea za baba yake kwenye serikali. Kadhalika Emanuel Nchimbi anayekabiliwa na shutuma za kughushi vyeti vya kitaaluma. Hawa ni watoto wa wenye hisa hawaguswi wala hawastuki hata wakikosea vipi.
Tundu Lissu aliwahi kusema huu ni utawala wa kifalme akaonekana mtu wa ajabu kabisa
 
Nilidhani mada ni 'baraza la mawaziri na vigogo' na sio back benchers! au nimesoma vibaya?

Hata mimi nilifikri hivyo Mkuu. Lakini kwa vile akili ya wanaccm imelundikana kwenye Masaburi wamekimbilia vidagaa! Sisi Wa-TZ mazoba acha tuliwe!
 
Back
Top Bottom