Baraza la mawaziri maziwa makuu kukutana nchini kesho

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
BARAZA la Mawaziri wa nchi wanachama wa eneo la Maziwa Makuu linalojishughulisha na Mradi wa kudhibiti ukimwi (GLIA), linatarajia kukutana nchini kesho kwa mkutano wa siku tatu kujadili ajenda nne.

Mkutano huo utaanza Machi 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo utajadili taarifa ya utekelezaji wa mradi kuanzia Julai mpaka Desemba 2009, na mkakati wa kukusanya rasilimali za kuendeleza mradi huo.

Pia utajadili shughuli zitakazofanyika kwa kipindi cha kuanzia Januari mpaka Juni, 2010 pamoja na kujadili utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa mwisho wa Baraza hilo uliofanyika nchini Rwanda Agosti 31, 2009.

Akizugumza jana na waandishi jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo alisema mawaziri watakaohudhuria katika mkutano huo ni kutoka nchi ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Rwanda, Uganda na Tanzania ambayo ndiyo mwenyeji.

"Kabla ya kukutana kwa baraza hili la mawaziri wakuu wa tume za kudhibiti ukimwi, waratibu wa mradi na wajumbe elekezi wa mradi watakutana siku moja kabla," alisema Marmo.

Marmo ambaye atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo alisema jukumu kubwa la mradi huo ni kupunguza athari za kijamii na kiuchumi zinazotokana na ukimwi pamoja na kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

"Maeneo ambayo mradi unatekeleza shughuli zake na yamekwishanufaika moja kwa moja ni wakimbizi waliohama makazi yao kutokana na vita, wakimbizi wanaorudi nyumbani na jamii inayozunguka makundi hayo.

"Mitandao ya usafirishaji na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, sekta ya afya pamoja na utawala, ufutaliaji na tathimini," alisema Marmo

Marmo alisema mradi wa GLIA unafanya kazi katika nchi hizo kwa masaada wa fedha kutoka Benki ya Dunia(WB) wa dola 200 milioni za kimarekani kwa kipindi cha miaka minne ambazo zinaishia Desemba 31 mwaka huu. Mradi ulianza rasmi Julai, 2006.

Marmo alisema mradi wa GLIA ulianzishwa mwaka 1998 na Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama kwa msaada wa UNAIDS ambapo sekretarieti na makao makuu yake yapo nchini Rwanda.

CHANZO MWANANCHI
 
Back
Top Bottom