Baraza la Mawaziri lakutana kikao cha kwanza

Lakini historia inatuambia kipindi cha pili na cha mwisho huwa ni cha kuvuna kama maraisi waliotangulia walivyofanya. Kila la heri wadanganyika
 
Nisaidieni hivi manaibu waziri ni wajumbe wa baraza la mawaziri?
soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwanza, vinginevyo unajaza wingu tu kwenye jukwaa la siasa, ambako kunahitaji uje na knowledge fulani si kama majukwaa yale ya kujadili "usipofyeka kichaka hutaambukizwa ukimwi."
 
Nilikuwa sijagundua kumbe posho ya rais ni kubwa sana kwa kila kikao/safari/mazishi/sherehe anayoudhuria.
 
Shida sio kumuamini JK. Ipeni muda serikali mpya tuone itafanya nini. Tatizo watu mnataka matokeo wakati ndio kwanza dakika 47 second half.lol.. Tusiiumbue serikali changa kama hii. Tuipe 100 days kwanza alafu tuone upepo unaelekea wapi...

Serikali mpya? Mkuu the same wine in new bottle. Rais ni yule yule, imani hatuna naye tena, mabaya zaidi maneno yake si ya kweli
ww mwenywe shahidi, ahadi za maisha bora yamekuwa maisha bomu, angalia bei ya kila kitu 2005 na sasa, ona mambo ya ufisadi anavyo wabeba,
ona wanafunzi wa vyuo vikuu walivyo nyimwa haki yao ya kupiga kura, kama unategemea lolote, shauri yako, tena maisha ndio yatakuwa balaa, watch out
 
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwa katika ngwe yake ya mwisho ya uongozi wa nchi ameonesha kuwa mkali kwa mawaziri wake wapya aliowateua hivi karibuni.

Kikwete amewaeleza wazi kuwa safari hii hana simile wala subira kwa Waziri atakayeboronga katika utekelezaji wa majukumu yake.

Rais Kikwete ametoa msimamo wake wakati anawapa majukumu mapya mawaziri hao na akagusia nyanja mbali mbali zikiwemo uwajibikaji, kufuata kanuni, sheria na pia kupambana na rushwa huku akisisitiza kuwa vita dhidi ya rushwa ni suala la kikatiba na kuwataka kuhakikisha kuwa Mpango wa Pili wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa (NACSAP-11) unatekelezwa.

Akizungumza na Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu Dar es Salaam jana, Rais Kikwete aliwaeleza mawaziri kuwa katika kipindi hiki cha pili cha uongozi wake hakutakuwa na muda wa kupoteza.

Amesema, hatakuwa tayari kukubali maelezo ya kwa nini utekelezaji wa majukumu ya msingi umeshindikana na amewataka mawaziri kusimamia mapato ya Serikali yasiyotokana na kodi na kudhibiti matumizi ya Serikali.

Pia aliwataka viongozi hao kuzingatia maadili ya uongozi ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria za nchi, kuheshimu sheria katika shughuli na mambo yao binafsi na kutunza siri za Serikali kwa mujibu wa kiapo chao.

Rais Kikwete pia alisisitiza umuhimu wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuwasiliana na wananchi kwa maana ya kueleza mafanikio na mipango ya Serikali katika kushughulikia matatizo ya wananchi.

Rais Kikwete aliwataka mawaziri hao kuvitumia kikamilifu vitengo vya mawasiliano ya Serikali katika wizara zao ambavyo ndivyo vyenye jukumu la kutoa taarifa kuhusu Wizara inavyotelekeza majukumu yake.

“Uzoefu unaonesha kuwa mawaziri wengi ni wazito kufanya mawasiliano na wananchi hata pale ambako Wizara imefanya mambo mengi mazuri. Hivyo, mawaziri muwe mstari wa mbele kuelezea mafanikio ya utendaji wa Serikali katika Wizara zetu,” alielekeza Rais Kikwete na kuongeza:

“Lazima ujengwe utamaduni wa kudumu wa kuwasiliana na wananchi wote ambao ndio waajiri wetu kupitia kura zao. Mawaziri wote tumieni vitengo vyenu vya mawasiliano na vyombo vya habari kwa ustadi ipasavyo”.

Akiwapongeza kuteuliwa kwao, Rais Kikwete alisema: “Mnastahili pongezi hasa ukizingatia ukweli kwamba nyinyi mmebahatika kuteuliwa kutoka kwenye orodha ndefu ya wabunge wengi wenye sifa za kushika nafasi mlizo nazo.

Nimewateua kwa imani kuwa pamoja nanyi, tutatimiza matumaini ya wananchi wa Tanzania waliokichagua Chama Cha Mapinduzi kiendelee kuongoza nchi yetu".

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, wakati akizungumza na wakuu wa idara katika wizara yake baada ya kutoka Ikulu aliwaambia kutokana na msimamo huo wa Rais Kikwete, yeye na naibu wake, hakuna kulala hadi matarajio ya wananchi katika wizara hiyo yatakapopatiwa ufumbuzi.

Dk. Kawambwa aliahidi changamoto ya kwanza kufanyia kazi ni kuhakikisha mikopo inayotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu inaboreshwa, ili kuondoa malalamiko yasiyokwisha kutoka kwa wanafunzi hao.

Akiwa amefuatana na Naibu Waziri wake, Phillip Mlugo, Dk Kawambwa alikiri kuwapo tatizo kubwa la utoaji mikopo, hali iliyofanya wanafunzi karibu wote wa vyuo vikuu kuinyima kura CCM katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. Licha ya mikopo pia aliahidi kuhakikisha maslahi ya walimu yanaboreshwa ili kuondoa uwezekano wa walimu kugoma.

“Natambua kuwa watoaji na wapokeaji elimu, wote wako kwenye matatizo, hili eneo nitashughulika nalo zaidi.

“Leo tulikuwa na mkutano na Rais (Kikwete) ametwambia wazi, kuwa safari hii hana simile wala subira, anachotaka ni watu tufanye kazi. Na sisi tunakuja hapa kwa hadhari kuwa hakuna kulala,” alisema Dk Kawambwa ambaye awali alikuwa Wizara ya Miundombinu.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Cyril Chami, akianza kazi rasmi aliahidi kuandika waraka kwa Baraza la Mawaziri, kuomba Serikali iboreshe viwanda ikiwamo kufufua vilivyokufa kwa kuvichukua na kurudi kwenye miliki yake.

Waziri huyo ambaye amepandishwa kutoka Naibu Waziri katika wizara hiyo, alisema:“Miaka mitatu nyuma, tulifanya ukaguzi wa viwanda vyote na tukajua kwa nini vingine vilifungwa au havijaanza kazi na sasa tunataka vifanye kazi”.

Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kupokewa rasmi wizarani hapo na wafanyakazi huku akifuatana na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, alisema baadhi ya viwanda vilivyoshindwa kufanya kazi vitawezeshwa ili vifufuke.

“Kuna viwanda vingine tumeona wamiliki wameshindwa kuzalisha bidhaa walizoomba awali na wanataka kubadili aina nyingine, nao tutawasaidia wazalishe wanachoweza baada ya kutetea hoja zao,” alisema.

Kwa upande wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, wakati akizungumza na wafanyakazi wa wizara yake, alisema baada ya miaka miwili, watu watajua upole na ujana wake ukoje, kwani anaamini atakuwa amefanya kazi vizuri na kwenye hilo, hana shaka nalo.

Alisema licha ya kutegemea kuteuliwa katika wizara hiyo nzito, atatekeleza Ilani ya CCM kwa kasi zaidi, huku akiahidi kuhakikisha sheria zote zilizotungwa kusimamia maliasili vikiwamo vitalu na wanyamapori zinasimamiwa ipasavyo.

Alisema anaamini kutokana na kuwekwa sheria za uwazi na shirikishi, mianya ya rushwa na vitendo vyake wizarani hapo vitakwisha.

Kwenye Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri Dk Haji Mponda, aliwataka wafanyakazi wa wizara hiyo, kushirikiana kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Dk Mponda alitaja changamoto kubwa kwa wafanyakazi wa sekta hiyo kuwa ni kutoa huduma bora za tiba katika vituo vyote vya afya nchini ili kuinua uchumi wa nchi “Mtanzania wa leo anataka huduma bora za tiba … mtu anapoingia hospitalini au kwenye zahanati anachotaka ni kumwona mganga na kupata huduma bora, hivyo kila mtoa huduma hana budi kuwajibika katika hilo.”

Miongoni mwa mawaziri walioanza kazi kwa cheche ni wa Ujenzi, John Magufuli ambaye juzi aliagiza Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) kusimamisha nafasi za kazi za mameneja wa mikoa zilizotangazwa kwenye vyombo vya habari na kuamuru mameneja wote waliosimamishwa kazi warejee kazini.

Wakati huo huo, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na mashirika yapatayo 50 yanayotetea usawa wa kijinsia, haki za binadamu na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), yamepongeza uteuzi wa mawaziri na naibu mawaziri uliofanywa na Rais Kikwete Novemba 24 mwaka huu.

Hata hivyo, taarifa ya FemAct iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, ilielezea kutoridhishwa na idadi ndogo ya mawaziri wanawake na pia ukubwa wa Baraza hilo kwa jumla.

“Idadi ya wanawake walioteuliwa kuwa mawaziri ni ndogo sana. Katika uteuzi huu, jumla ya mawaziri ni 29, kati yao wanaume ni 22 sawa na asilimia 76 na wanawake ni wanane, sawa na asilimia 24.

“Naibu mawaziri ni 21, wanaume ni 18 sawa na asilimia 86 na wanawake ni watatu sawa na asilimia 14. WanaFemAct walitarajia kuwa hiki kilikuwa kipindi mwafaka cha kufikia uwiano wa 50:50 ingawa mikakati iliyowekwa na fursa zilizokuwapo hazikutoa fursa hiyo,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

 
Jana nilimuona JK kwenye runinga ya TBC 1 akizungumza na mawaziri akiwaambia kuwa anawatayarishia semina elekezi kama zile alizofanya mwaka 2006 kule Hoteli Ngurudoto na kutumia mabilioni; na serikali yake kuishia katika matope ya ufisadi wa Richmond.

Wakati akipanga hayo taarifa ya habari hiyo hiyo ilikuwa ilionyesha jinsi wagonjwa wa saratani wanavyokosa huduma katika hospitali ya Ocean Roda baada ya kifaa cha mionzi kuharibika na kuhitaji matengenezo ambapo inasemekana kuwa fedha za matengenezo zimekuwa ni kitendawili kwa muda mrefu sasa.

Aidh mgonjwa mmoja aliyehojiwa alisema kuwa inafikia hatua wagonjwa wanarudishwa kutokana na hospitali hiyo kukosa fedha za kununua mafuta ya jenereta. Ikizingatiwa kuwa CCM ilitumia fedha nyingi sana katika kampeni kwa mambo yasiyokuwa na maslahi kwa taifa wala wananchi, hii ni hatari sana.

Nini maoni yako, Je kuna haja ya mawaziri kutayarishiwa semina elekezi zinazofanyika katika mahoteli makubwa makubwa na kutumia fedha nyingi za serikali ilihali wananchi wanakosa huduma muhimu za kijamii?
 
Mkuu, wadanganyika walimkubali kikwete bila kulazimishwa na mtu ... na hayo ndio maisha bora kwa kila mdanganyika!! wanalialia nini sasa.
 
Mkuu, wadanganyika walimkubali kikwete bila kulazimishwa na mtu ... na hayo ndio maisha bora kwa kila mdanganyika!! wanalialia nini sasa.
Nasita kuwalaumu WATANZANIA, walipiga kura kuchagua mbadala wa kikwete lakini NEC walitumia ubabe kumtangaza jamaa mshindi kwa kuchakachua matokeo.

Ni kweli amewaandalia semina elekezi. lakini najiuliza kwa bajeti ipi?? au ndo matumizi ya kasma ya chai na vitafunwa?? au kuna mfadhili aliyefadhili hiyo semina?? Nachelea kusema kwamba Rais anatumia madaraka yake kuchota HAZINA kwa masuala yasiyo ya kimsingi. Wangetumia hizo fedha kufanikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuweka huduma at least nzuri kwa wagonjwa hospitalini au hata kuwapatia vijana wetu hiyo mikopo ya elimu.

Rais ajiulize kuhusu tathmini ya semina elekezi aliyoifanya last era imeleta impact gani?? NAMSHANGAA
 
Wakati JK alipoingia madarakani kwa mara ya kwanza 2005, mabilioni ya fedha za walipa kodi ziliteketezwa huko Ngurundoto katika uendeshaji wa semina elekezi ambazo hazikuwa na tija yeyote, mbali na kuwapa ulaji watu wachache. Hivi majuzi wakati akizungumza na wateule wake nilimsikia JK akigusia kwamba serikali yake ilikuwa mbioni kuanzisha raundi nyingine ya semina hizo. Hivi nchi hii haifanyi tathmini yeyote juu ya programu mbali mbali inazoziendesha; maana nina hakika kama semina hizo zingelifanyiwa tathmini ingelionekana wazi ya kuwa hazikuwa na manufaa yeyote.
 
Back
Top Bottom