The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Sijui hawa mawaziri wanasumbuliwa na nini?
Ninavyojua, serikali hata iwe ya kifisadi namna gani, mawaziri huendelea kuwajibika kwa pamoja hata kama wanatofautiana vyama.
Leo hii unawasikia mawaziri wanaisema serikali kwa kauli zinazopingana mfano Babu wa Loliondo anapigwa stop na waziri wa Afya kisha waziri mwingine anasema haiwezekani kumzuia. Halafu ujue mwana JF, wote wana sababu nzuri tu za kumsaidia mtanzania waliyemfilisi kwa ufisadi.
Mwingine anaisemea serikali eti wamegundua kuna balozi zinawafadhili CDM kuleta machafuko nchini. Kwa manufaa ya nani? Nchi gani hizo? Haijulikani.
Kwa nini serikali iliyo makini kiasi cha kugundua yote hayo haijamchukulia hatua hata mhusika mmoja? Mbona inakuwa vigumu kuzitaja nchi?
Kauli nyingi za binafsi na zinazotofautiana hazitakiwi under serikali moja. Hii ni bila kujali ni serikali ya kifisadi kama yetu au ni ile inayowajibika. Ndiyo maana nasema; Mawaziri wa JK acheni mikurupuko!