Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kanisa halina chama,lazungumzia uchaguzi mkuu 2015 na ka

jme

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
4,665
4,797
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa ujumbe mzito wa kwaresima kwa mwaka 2015 na kueleza kwamba kanisa hilo halina chama licha ya kwamba waamini wake wana vyama vya siasa.
Katika ujumbe huo unaongozwa na kauli mbiu ya “zingatieni haki na kutenda mema” unaotoka kitabu cha Isaya sura ya 56 aya ya kwanza(isaya 56:1),baraza hilo limesema kanisa katoliki halina chama wala halifungamani na chama chochote cha siasa nchini.
UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015
Maaskofu hao walisema “Tutakuwa tunakabiliwa na uamuzi wa kisiasa kwa kuchagua viongozi watakaotumia rasilimali za taifa letu kwa ama ustawi na maendeleo ya wengi walio katika lindi la umasikini au kwa matumizi ya fahari zao binafsi na wabia wao katika kujitajirisha walisema na kuongeza kuwa
Tunashauri zoezi hili liendeshwe kwa uadilifu na lisifanywe kuwa tendo la ulanguzi wa kura.Huku ni kudhalilisha utu wa watu na kuvuna madaraka kupitia umasikini wa watu.
Tunapenda wale wanaomba dhamana ya uongozi wa taifa hili katika Nyanja zote na sisi sote tunaotumia haki ya kura zetu tuitumie fursa hii kama dhamana na tendo la heshima ya utu wetu”ilieleza ssehemu ya ujumbe huo wa TEC.
MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Maaskofu hao walisema kuwa “Tunarudia kusistiza kuwa hiki ni kipindi adhimu kwa taifa letu.Tunapenda kulikumbusha taifa letu kwamba hili ni zoezi linalodai uadilifu mkubwa na utashi wa kisiasa wenye lengo la kujenga Taifa kwa muda mrefu.
Kejeli,vitisho,migomo,vijembe na kukosa ustamilivu katika mijadala yenye lengo la kuunda misingi ya mustabari mwema wa taifa letu vinaonesha kukosekana kwa uzalendo na ukomavu wa kisiasa.Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa ujumbe mzito wa kwaresima kwa mwaka 2015 na kueleza kwamba kanisa hilo halina chama licha ya kwamba waamini wake wana vyama vya siasa.
Katika ujumbe huo unaongozwa na kauli mbiu ya “zingatieni haki na kutenda mema” unaotoka kitabu cha Isaya sura ya 56 aya ya kwanza(isaya 56:1),baraza hilo limesema kanisa katoliki halina chama wala halifungamani na chama chochote cha siasa nchini.
 
Hivi ndivyo wanapaswa kufanya watumishi wa Mungu.Kwani badala ya watawala kukimbilia kuwatumia kwa ajili ya kuombea amani ni lazima wajue amani ni tunda la haki.Kuombea amani bila kutoa haki ni maombi nje ya mantiki(Illogical/Irelevant prayers).
 
Ulanguzi wa kura ulishaanza muda mrefu sana, kuna watu wanatafuta ubunge wanazunguka mikoani na mifuko ya pesa ili kujaribu kuwahonga wananchi.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Well said, Lakini muda si mrefu utawasikia ohooooo Mgombea wa Chama Fulani ni Chaguo la Mungu; Sijui ni Mgombea wa Chama gani alishakuwa chaguo Sheltani?. Kumbe nyuma ya Pazia nao ni Kuweka mazingira rafiki ya Kupiga deal " Escrow's Business" .

Pili hiyo haitoshi kwa watu wanao waongoza waumini katika uhalisia wa kupamabana na umasikini ; Ninadhani muda ukifika wawaeleze waumini wao kuwa wachague viongozi wanaomwogopa Mungu, "those who walk the talk," siyo Maisha bora kwa kila Mtanzania na ahadi zaidi ya 150, na mwisho wa siku "Big Results Now".

Tanzania hatuna shida na slogan tena, tunachokihitaji ni utumishi uliotukuka, Mtumishi wa watu, Kiongozi shupavu ni "Public interest first rather than personal gain.

Tunatamani tuwapate viongozi watakao kuwa wapo tayari kuzikemea familia zao na marafiki kutopora Mali za umma na matumizi mabaya ya ofisi. Mwisho kabisa tuwapate Viongozi watakaokuwa na hofu ya Mungu, huku wakiilinda Katiba na kuzitii sheria za nchi.

Tunatamani Kuwapata watu watakaorejesha uwajibikaji, uadilifu na Viongozi wenye Kutetea wanyonge wa nchi hii. Viongozi wenye Kudhubutu kusema waziwazi bila kumgunya maneno ya kwamba " Hizi ni Fedha za Umma" na sio wenye kusema, Humu kuna fedha za Umma na Humu kuna fedha za Mafisadi.'

Mtumishi wa Umma na kiongozi shupavu siku zote lazima asimame na Umma. S/he must stands for the decission that uphold the public interest, even though that decissions are unpopular.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Mambo baaaado, subiri maaskofu, haohao watakapokuja na "chaguo la Mungu" kwa mtu ambaye ni mlanguzi wa kura wa kutupa, mwizi na muongo mkuu, mwenye kupenda ufahari, sifa na kujitajirisha mwenyewe na ukoo wake, ambaye hana habari na umaskini wa watanzania. Subiri tu utaniambia
 
"... au kwa matumizi ya fahari zao binafsi na wabia wao katika kujitajirisha walisema na kuongeza kuwa ..."

Kwenye hiyo quote, je na Askofu Kilaini na Askofu Nzigilwa wana-guts za kutamka hayo? Je, wamekwisha kurejesha pesa ya Escrow?!
 
Yule askofu Kisoft asijeanza kukurupuka na machuguo yake ya ki-escrow escrw.
We need apostolic which are impartial and with commitment like this.
 
nimeyachoka kweli matamko ya hawa watu. natamani yule Fidel Castro angetawala hata nusu mwaka tu. hawa jamaa tungewasikia huko kuzimu na matamko yao haya.
Na nimeelewa kwa nini nchi kama Cuba waliwapiga marufuku hawa jamaa.
wakae pembeni watuachie nchi yetu.
 
Hivi ndivyo wanapaswa kufanya watumishi wa Mungu.Kwani badala ya watawala kukimbilia kuwatumia kwa ajili ya kuombea amani ni lazima wajue amani ni tunda la haki.Kuombea amani bila kutoa haki ni maombi nje ya mantiki(Illogical/Irelevant prayers).
Hapo umenigusa vizuri sana. Hatuwezi kuhubiri Amani bila kuhubiri Haki. Hakuna Amani mahali ambapo haki haitendiki au haionekani kutendeka. Hatuwezi kuhubiri Upendo kama hatuhubiri Haki. kuhubiri upendo bila haki ni kajeli.
 
Yule askofu Kisoft asijeanza kukurupuka na machuguo yake ya ki-escrow escrw.
We need apostolic which are impartial and with commitment like this.

Kilaini hana uwezo tena . Ni mwana Escrow na heshima mbele ya Maaskofu kama yule wa Mwaza . Askofu wa Iringa nk . Tulieni watu wameanza kuweka maneno sawa na mahubiri haya haya hadi mwisho . One day niliepewa nafasi ya kusema na waumini wa Kanisa katoliki Kigango cha Mt.Petro . Nikawaambia juu ya ukuu na uwezo wa Mungu . Kutoka kuumwa cancer aina ya Multiple MyeLoma lost 10 cm from height to a cancre free person .
Nikawauliza kwa nini wanajaa makanisani na kuimba na kutoa sadaka , na hata kufunga lakini ni wao wao hao wano pita kununua na kuuza kura, wako maofisini wana madaraka wanachukua rushwa, ma hospitalini wanaumiza wagonjwa , mahakani wanataka rushwa toka kwa wanyonge na kuwadhulumu wajane nk. Kanisa zima lilikaa kimya kabisa na kuwauliza wana maana gani kujazana kweneye nyumba ile ya ibada wakadi wao ni madalali wa haki za watu wasio na uwezo ?

Wengine walilia . My point is kama makasisi watasimama na kupigia kelele haki ya kupiga kura ya Ndiyo au hapana kwa Katiba na kuchagua watu kwa matakwa yao kwa manufaa ya Nchi slowly waumini watasikia na watafanya maamuzi mazito .
 
Back
Top Bottom