Baraza la JK limekaa kuna jipya?

Kiroroma

JF-Expert Member
Feb 6, 2009
370
114
Kutwa leo ndani ya Kikao cha Baraza la Mawaziri (Extra Odinary Meeting)Walioko kiungani tupeni yanayojili.
 
hakuna jipya hapo lazima kawaita wale lunch pamoja na kuwasimulia mambo ya kubembea
 
Kutwa leo ndani ya Kikao cha Baraza la Mawaziri (Extra Odinary Meeting)Walioko kiungani tupeni yanayojili.

Kwa nini tuna hii attitude sisi watanzania?? Hilo baraza nadhani lina kawaida ya kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kureview mambo mbalimbali yanayohusiana na wizara zao/serikali kwa ujumla.

Nashangaa kuona wewe unataka upate update? Za nini? Kama wangetaka iwe news si watu wa media wangeitwa? I think we need to spend more time working than speculating what the cabinet meeting will/is expected to come up with!!!
 
extra ordinary meeting lazima kuwe na issue nzito, hawaitani tu kama mnavyoitana jioni kwenye vikao vya mbege na dengerua.
sasa Watz wameamka, wanadadisi kila jambo hii ni katika kulinda mustakabali wa nnchi yao, sasa hivi hata ukiongea na mkeo juu ya kuhujumu nchi ujue kesho watu wote wamejua, hii ni nzuri sana.
 
labda asuse na kuamua...kujiuzulu...aachie nchi ili abembelezwe,.......arudi tena awape kazi ya kuwafanyia ubaya wale wabaya woote....
 
Kwako Dmussa, suala linalowashangaza watu hadi wajadili yote haya ni namna mambo yanavyoenda vibaya. Mtoa hoja ameijenga, kwa kuwa na matumaini kwamba pengine sasa Serikali imetambua madhaifu ya nyuma na iko imara sasa kujadili masuala yenye masilahi kwa taifa na umma wake. Maana ninachojua baraza hilo la Mawaziri litakuwa linapungukiwa na kitu "UBUNIFU" wa namna nchi inavyotakiwa iendeshwe kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi na rasilimali zake.

BLM limekuwa ni Business as Usual-BAS! Hivyo, hakuna kati ya Mawaziri pamoja na M/kiti wao anayeweza kuleta hoja ili kuboresha matokeo ya vikao hivyo. Siyo kukaa na kula bites tu. Bali ni matokeo gani ya vikao hivyo kwa watanzania wote yanapatikana? Ndiyo suala la msingi ambalo kila mjumbe anatakiwa ajiulize kila mchana na usiku kabla hajaingia kwenye chuma ya Baraza husika.

Mpaka lini tutaendelea kusubiri matunda yasiyokomaa! Kila siku yako tu na rangi ya kijani?
 
Kwa nini tuna hii attitude sisi watanzania?? Hilo baraza nadhani lina kawaida ya kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kureview mambo mbalimbali yanayohusiana na wizara zao/serikali kwa ujumla.

Nashangaa kuona wewe unataka upate update? Za nini? Kama wangetaka iwe news si watu wa media wangeitwa? I think we need to spend more time working than speculating what the cabinet meeting will/is expected to come up with!!!
Hii ndio Tanzania ya kizazi cha dot com.Wanadadisi karibu kila kitu kinachofanyika.Kadri kwoledge inavyoongezeka ndivyo watakavyo demand zaidi kutoka kwa viongozi. Kama ulivyo mquote Charles Darwin hapo chini, dawa sio kujitutumua na kufanya mambo kibabe...dawa ni kubadilika ili survival iwepo.
 
Big Up Mh. Kikwete waite ule nao lunch ukimaliza anza kuwahukumu usiwaogope hao mimi nakufagilia lakini mabest wanakuharibia
 
Jamani tusipresume hapa. tujaze vikombe kahawa tukanunue karanga tusubiri watoke kisha tuhabarishwe yaliyojiri ili hatimaye tuweze kujadili.

Kuna wakati subira huwa inaleta heri ila mara nyingi subira ni adabu ya uoga. Msihofu tutajua tu maana najua Mwanakijiji ameshakarusha KAINZI kake. tusubiri hapa
 
Kutwa leo ndani ya Kikao cha Baraza la Mawaziri (Extra Odinary Meeting)Walioko kiungani tupeni yanayojili.

Anapata baraka toka kwa baraza lake la mawaziri kabla ya kuchukua maamuzi magumu.

hivi na sophia simba yumo ndani? nina wasiwasi asije akalianzisha kwa wabaya wake humo humo yaani kitendo bila kuchelewa, mama yupo faster 5min ahead of normal time.
 
Baba na mama wakikaa sebuleni usiku kucha kama siyo kawaida yao, budi watoto kuuliza kulikoni.Kama watoto hawaulizi na kukaa kimyaa basi ujue kuna kasoro katika uelewa wao.Watanzania wana haki ya kujua kila kunapokucha viongozi wao wanawaza nini kuwaelekeza katika kujenga nchi yao pia kukidhi matarajio waliyoyatoa kwao wakati wa kampeni za 2005 :MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.Hasa kwamba maelezo mengi yanahitajika kujibu maswali yaliyo mbele ya jamii kuhusu mustakabali wa hali zao za maisha.Ni vema wakajulishwa nani kaboronga na nani anastahili zawadi.
 
Anapata baraka toka kwa baraza lake la mawaziri kabla ya kuchukua maamuzi magumu.

hivi na sophia simba yumo ndani? nina wasiwasi asije akalianzisha kwa wabaya wake humo humo yaani kitendo bila kuchelewa, mama yupo faster 5min ahead of normal time.

yaani hapa ndo nimecheka mpaka basi..yaani rais anaomba baraka kwa watu aliowateuwa
 
Baba na mama wakikaa sebuleni usiku kucha kama siyo kawaida yao, budi watoto kuuliza kulikoni.Kama watoto hawaulizi na kukaa kimyaa basi ujue kuna kasoro katika uelewa wao..

ha ha ha, mzee hapa umenifurahisha sana, sentensi nzuri sana hii.
 
Big Up Mh. Kikwete waite ule nao lunch ukimaliza anza kuwahukumu usiwaogope hao mimi nakufagilia lakini mabest wanakuharibia
JK Rais WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Hawezi hata kumfokea waziri wa hovyo zaidi katika utawala wake Sophia Simba , Makongoro Mahanga na makarunguyeye wengine, atawabembeleza, atawalambalamba miguu, atachekacheka...mwisho wa siku wanaendelea kuvurunda.
 
Nothing new...Jueni kwamba hakuna analoweza kufanya jipya yule.

Labda anapanga nao jinsi ya kumalizia mwaka na kufanya sherehe za xmas na kuukaribisha mwaka mpya!

Kwa habari ya siasa..mhhh nothing!
 
Nothing new...Jueni kwamba hakuna analoweza kufanya jipya yule.

Labda anapanga nao jinsi ya kumalizia mwaka na kufanya sherehe za xmas na kuukaribisha mwaka mpya!

Kwa habari ya siasa..mhhh nothing!
kuna mwanajamvi mmoja amesema labda anawahadithia juu ya mabembea ya Jamaika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom