Baraza la Habari Tanzania (MCT) halina meno

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,695
2,553
Kwenye magazeti ya leo kumechapishwa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotelewa na MCT kuhusu uandishi usiozingatia maadili wa kutukanana na kuumbuana miongoni mwa baadhi ya vyombo habari.

Utamaduni wa kitaanzania uliozoeleka wa kila taasisi ambayo imeanzishwa kusimamia taasisi nyingine kujificha na kushindwa kutimiza wajibu kwa kujiona na wao watazamaji na hawahusiki na matatizo yanayofanywa na hao wanaowasimamia unatupeleka pabaya.

Nilitegemea katika taarifa yao kwanza kuvitaja hivyo vyombo vya habari, wamiliki, wahariri na waandishi sababu wana vijua na wangeviita na kuvitaarifu moja kwa moja kuliko kutuma general statement kwa mtu ajichagulie mwenyewe na matokeo ya mkutano wao ndio wangeandika press lease. Pili wange vichukulia hatua kama wao wanaridhika kuna uandishi usio kuwa na maadili kama wanavyodai, vinginevyo wanatuchosha na taarifa zisizo jitosheleza na kukosa maana kwa msomaji.

Kwakuwa lengo ni majiwe yote yanageuzwa sasa basi ni wakati muafaka pia kutazama na taasisi hii kama na yenyewe iko safi na ina watu safi isije kuwa ni recycling ya watu wale wale wasio na tija na ubunifu na wamekuwa wakiturudisha nyuma watanzania wote. Kama vipi wawaombe JF members wawapige tafu manake hapa majibu ni live hapo kwa hapo hakuna longo longo, watu wana knowledge na data.

Manake ukilinganisha na media za nchi nyingine hata vile tu zinapolitiwa na media nyingine bongo kuna kazi ya kufanya.
 
Back
Top Bottom