Baraza kuu UVCCM wailaani CHADEMA kwa siasa za fujo na mauaji; Je, ni sawa?

Kijana ukisha kuwa ccm unakuwa pointless and CREDITLESS mfano salumu ally.
 
Kwa tukio la Iringa CDM mnapaswa kumshukuru Mungu kwa kubadili mipango ya kishetani iliyokuwa imepangwa na CCM vinginevyo kwa sasa tungekuwa tunaongea habari nyingine na katika hili CDM hamkuwa na ujanja na kiukweli hii ilikuwa imepangwa vizuri na ilivyoharibika naamini CCM sasa watalazimika kujipanga upya. Kuhusu UVCCM kama hao ndiyo nguvu ya chama basi CCM ilishajifia.
 
Kama Shigela ndo anaonekana ana akili kubwa na kuongoza vijana wa CCM hao wanaoongozwa wakoje? TAFAKARI
Shigela ni microbes wasabishao shigelosis ni u.h.a.r.o. so msishangae kuona yatokayo kwa huyo mdudu
 
Huyo Shigela ni Kilaza wa Sisa za kisasa kama walivyo wanaccm wengine ! ni Punguani wa aina ya kipeee
 
Kwa tukio la Iringa CDM mnapaswa kumshukuru Mungu kwa kubadili mipango ya kishetani iliyokuwa imepangwa na CCM vinginevyo kwa sasa tungekuwa tunaongea habari nyingine na katika hili CDM hamkuwa na ujanja na kiukweli hii ilikuwa imepangwa vizuri na ilivyoharibika naamini CCM sasa watalazimika kujipanga upya. Kuhusu UVCCM kama hao ndiyo nguvu ya chama basi CCM ilishajifia.
CCM wana Polisi, fedha, TSS,Jeshi ila CDM wana MUNGU Kwa hiyo inabidi ujue nani mkubwa hapo.
 

9k=


UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wamemaliza kikao cha baraza la umoja huo ambapo wamejadili ajenda mbalimbali za msingi kuhusu Uchaguzi na pia wamejadili juu ya hali ya siasa nchini na mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa amani na mauaji, ambapo wamekinyooshea kidole Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwa vinara wa matukio ya mauaji, kitu ambacho ni hatari kwa Taifa.


Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya Katibu Mkuu, jengo la Mikutano (whitehouse) katika Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi, Dodoma.

Alisema kuwa,kumekuwa na matukio ya mauaji kwenye mikutano ya chama hicho katika mikoa ya Singida, Igunga, Tabora, Morogoro na Iringa hali ambayo imekuwa ikitishia Usalama na Amani ya Nchi.

“Tunalaani Chadema kuwa vinara wa vurugu zinazosababisha mauaji na kila tukio linapotokea viongozi wa Chadema wanakuwepo, hali inayoonyesha kuwa siasa wanazoendesha si za kistaarabu” alisema

Alisema kuwa Chadema wanachojenga ni hatari kwa Taifa na pia hatari kwa Umoja wa Vijana pia na kama wana mapenzi ya kweli na watanzania waache siasa zinazasababisha mauaji mara kwa mara.

Katika hatua nyingine, Shigela amesema kuwa,Kikao cha baraza Kuu kilimalizika jana na kufanya maamuzi baada ya kujadili na kupitisha majina ya wagombea na baadhi ya nafasi majina yatapelekwa halmashauri kuu ya taifa (NEC) ambacho ni chombo cha mwisho cha maamuzi katika Chama.

Amezitaja nafasi ambazo tayari zimetolewa maamuzi, kuwa ni nafasi ya mwakilishi mmoja kutoka UVCCM kwenda UWT, Mwakilishi mmoja kutoka UVCCM kwenda wazazi, Baraza Kuu taifa nafasi tano Zanzibar na nafasi tano Bara, na sasa orodha hiyo inaandaliwa ili majina ya waliochaguliwa yatangazwe rasmi.

Amesema kuwa,katika nafasi nyingine ikiwemo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti tayari yamewekewa alama na yatapelekwa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC).

Pia amewataka wagombea ambao tayari wamefanyiwa uteuzi waache siasa za kuchafuana na zile za makundi.

Aidha alisema kuwa Mkutano Mkuu wa taifa unatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 20, mwaka huu na kutaka wajumbe wote kuhakikisha wanafika Dodoma Oktoba 19.

Shigela amesema kuwa, Baraza kuu lilipata nafasi ya kuwapongeza vijana wa Jumuiya kwa kuthibitisha kuwa umoja huo ni tanuru la kuoka viongozi kwa baadhi yao kuteuliwa nafasi mbalimbali serikalini na kwenye Chama na kulitaka Baraza kuu kuzingatia mahitaji ya vijana ili wapate fursa zaidi za kugombea ili umoja huo uweze kupeleka sura nyingi za vijana ndani ya chama.

Pia alisema kuwa wametapa nafasi ya kuitafakari taarifa ya kazi nzuri ya Serikali kwa kuwawezesha vijana katika suala la kuwapatia elimu na kuwawekea mikakati ya miaka mitano ya kusaidia vijana.

Shigela aliitaka Serikali kuwa na mipango ya kudumu ili kuweza kudhibiti majanga mbalimbali yanayotokea hapa nchini k.v mafuriko, kuzama kwa meli, mauaji n.k
 
Hawa watoto wameshazeeka hadi na uwezo wa kufikiria undani wa jambo ndio hivo hawana tena; mambo kudakia dakia tu mgugumio wa wazee wao CCM ambao wengi ni MAFISADI wasiosameheka hata kwa dawa.
 
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wamemaliza kikao cha baraza la umoja huo ambapo wamejadili ajenda mbalimbali za msingi kuhusu Uchaguzi na pia wamejadili juu ya hali ya siasa nchini na mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa amani na mauaji, ambapo wamekinyooshea kidole Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwa vinara wa matukio ya mauaji, kitu ambacho ni hatari kwa Taifa.


achana na Chadema we dada, tuambie nani mmewakata panga kugombea huko UVCCM
 
UVCCM au Umoja wa Vihiyo wa Chama Cha Mafisadi hauna lolote zaidi ya kuhitaji ukombozi. Kwa zaidi ya miongo mitano wamekuwa wanatumika kama nepi za wazee. Badala ya kushinikiza kuwepo wagombea vijana, wao wanaimba upuuzi ule ule kama wimbo wa jogoo. Ajabu tunaambiwa wengine wamesoma ingawa hawajaelimika. Huu haukuwa mkutano bali kigwena na umbea na kupanga dili za kuchakachua uchaguzi na kuiba pesa kwenye mabenki na kuingia mikataba ya kijambazi kupata pesa ya uchaguzi ukiachia mbali zile zitokanazo na ujambazi na mihadarati.
 
Shigella ni nini?. Mafuta ya kujipaka. Hata mtoto wa miezi sita anajua polisi ndo wauaji,iweje yeye hajui.
 
UVCCM au Umoja wa Vihiyo wa Chama Cha Mafisadi hauna lolote zaidi ya kuhitaji ukombozi. Kwa zaidi ya miongo mitano wamekuwa wanatumika kama nepi za wazee. Badala ya kushinikiza kuwepo wagombea vijana, wao wanaimba upuuzi ule ule kama wimbo wa jogoo. Ajabu tunaambiwa wengine wamesoma ingawa hawajaelimika. Huu haukuwa mkutano bali kigwena na umbea na kupanga dili za kuchakachua uchaguzi na kuiba pesa kwenye mabenki na kuingia mikataba ya kijambazi kupata pesa ya uchaguzi ukiachia

umeliona siyo
 
Kumbe askari nao ni Chadema nilikuwa sijajua hilo

Hata mimi aisee! Kumbe wale askari wa Morogoro na wa Iringa ni wa Chadema! Mbona lakini taarifa ya waziri wa mambo ya ndani haijataja kwamba hao askari ni wa chadema? Au waziri kakosea? Huko UVCCM Kuna vichwa au tope?
 
Back
Top Bottom