Baraza jipya la Mawaziri la Serikali ya Ufaransa

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Waziri Mkuu mteule wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, ametangaza baraza la mawaziri 34 (wakiwa ni pamoja na manaibu mawaziri).

Baadhi ya sifa za baraza hili:
- Idadi sawa ya wanawake na wanaume (17 wanawake na 17 wanaume).
- Mawaziri 7 kati yao wana umri chini ya miaka 40
- Mawaziri 7 wana asili ya kigeni, wakiwemo wenye asili ya Afrika ya Kaskazini, Carrebian na Korea.
- Mishahara yao imepungua kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mawaziri wa serikali iliyopita, ambapo Sarkozy alijiongezea mshahara kwa asilimia 170 (Euros 19,000 kwa mwezi).

Nadhani yapo tunayoweza kujifunza kutoka baraza la mawaziri kama hili, hasa katika masuala ya uwiano wa kijinsia na kubana matumizi.
 
Waziri Mkuu mteule wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, ametangaza baraza la mawaziri 34 (wakiwa ni pamoja na manaibu mawaziri).
...Tujiulize, nchi tajiri kuliko sisi -ikiwa na uwanja mpana zaidi wa shughuli za serikali- inawezaje kuwa na mawaziri wachache?

Baadhi ya sifa za baraza hili: - Idadi sawa ya wanawake na wanaume (17 wanawake na 17 wanaume). - Mawaziri 7 kati yao wana umri chini ya miaka 40 - Mawaziri 7 wana asili ya kigeni, wakiwemo wenye asili ya Afrika ya Kaskazini, Carrebian na Korea. - Mishahara yao imepungua kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mawaziri wa serikali iliyopita, ambapo Sarkozy alijiongezea mshahara kwa asilimia 170 (Euros 19,000 kwa mwezi).
...Baraza la mawaziri la kisasa kabisa, likiwakilisha hali halisi ya nchi.

Nadhani yapo tunayoweza kujifunza kutoka baraza la mawaziri kama hili, hasa katika masuala ya uwiano wa kijinsia na kubana matumizi.
...Nadhani, somo la kwanza ni "ukubwa wa pua, si wingi wa makamasi".

...Bila kusahau asili ya kigeni.
 
Mbona siku nyingi walishajifunza sema vichwa vigumu na kupeana ulaji kwa hawa viongozi wetu ndo kila siku hatusogei kimaendeleo
 
...Tujiulize, nchi tajiri kuliko sisi -ikiwa na uwanja mpana zaidi wa shughuli za serikali- inawezaje kuwa na mawaziri wachache?

...Baraza la mawaziri la kisasa kabisa, likiwakilisha hali halisi ya nchi.

...Nadhani, somo la kwanza ni "ukubwa wa pua, si wingi wa makamasi".

...Bila kusahau asili ya kigeni.

Mbona siku nyingi walishajifunza sema vichwa vigumu na kupeana ulaji kwa hawa viongozi wetu ndo kila siku hatusogei kimaendeleo
Haya mliyoyataja ndiyo Watanzania wengi wenye akili zetu hatuachi kujiuliza, "kwa nini nchi tajiri zinakuwa na matumizi madogo ya kiuendeshaji wakati sisi masikini tunaokwenda tukiomba kwao tunafuja pesa kwa kugawana ngawira?"
 
cha umuhimu hapo ni ujuzi wa watu na sio idadi au jinsia...kama wanawake wengi wana ujuzi zaidi nitaweka wanawake zaidi au kama ni wanaume hivo hivo...ukifuatilia usawa kwanza badala ya ujuzi serikali inaweza isifanye kazi vizuri na wanachi wakalalamika
 
Ufaransa ni nchi tajiri kuwa waziri ni kwa ajili ya umaarufu na siyo kwa ajili ya kipato hapa kwetu uwaziri ni kazi kama vile Mkurugenzi mkuu, Katibu Mkuu, Meneja mkuu nk. hivyo kuwa na mawaziri wengi ni sehemu ya sera ya serikali ya kutoa ajira kwa wananchi wake (FULL EMPLOYMENT POLICY)
 
Ninakubaliasana na wazo la kujali zaidi uwajibikaji kuliko kukimbilia uwiano, lakini kweli inawezekana kuwa katika taifa lenye watu zaidi ya milioni 40 kusipatikane na wanawake na wanaume wachache wenye uwezo wa hali ya juu? Hasa ikitiliwa maana kuwa uwaziri ni suala la kisiasa zaidi kuliko utaalamu.

Ufaransa ni nchi tajiri kuwa waziri ni kwa ajili ya umaarufu na siyo kwa ajili ya kipato hapa kwetu uwaziri ni kazi kama vile Mkurugenzi mkuu, Katibu Mkuu, Meneja mkuu nk. hivyo kuwa na mawaziri wengi ni sehemu ya sera ya serikali ya kutoa ajira kwa wananchi wake (FULL EMPLOYMENT POLICY)
Ikiwa umekusudia kuchekesha, nimecheka sana na hii sera ya ajira. Nakumbuka hata mheshimiwa mmoja alijisifia kuwa ukosefu wa maji nchini umepelekea kuwa na "vijana wengi wajasirimali" kujiajiri kwa kubeba maji. Ooooooh Masikini Tanzania!
 
Back
Top Bottom