Barabara zetu na waenda kwa miguu,mikokoteni,na baiskeli.

kimatire

JF-Expert Member
Nov 27, 2008
371
93
Tuangalie jinsi gani barabara za Bongo zilivyojengwa na zinavyotumika!!!Sisi NMT yaani Non-Motorized Transporters hatujaliwi na hata hatuzingatiwi katika designing na matumizi ya barabara.Mathalani katika vivuko vya waenda kwa miguu licha ya kuwa vichache tena visivyozingatia usalama wetu,hakuna madaraja zaidi ya lile la Mazense,hakuna alama nk.Pia ukiangalia njia zilizotengwa kwa ajili yetu siyo kwa matumizi hayo.Kwani hata malori yanapita huko,Hapa nazungumzia service road ambazo maana yake siyo kwa walengwa wala!!Lini utambuzi utakuja kwa hao wahandisi wetu uchwara wa barabara kutambua hilo na kuweka walkways zenye pavement blocks na wala siyo lami kama ilivyo sehemu ndogo ya Pugu Road?????Wana JF tulitizame hilo, dada,kaka,watoto wetu wanagongwa kila kukicha kila huku na kule katika kona zote za Jiji la Dar Es Salaam.Tunaangamia kwa kukosa maarifa!!! Hebu tuliangalie hili lilivyokaa.
 
Last edited:
Back
Top Bottom