Barabara ya Mandelea Dar ni kero

Mkombozi

JF-Expert Member
Feb 19, 2008
806
426
Barabara hii inatisha na ina msongamano wa ajabu unaosababishwa na ujenzi usioisha unaoendea.
Wakuu Kwa wale mlionko nje ya Dar, barabara ya Mandela huanzia pale ubungo mataa hadi kilwa karibu na uwanja wa Taifa wa michezo.
Hii barabara ni miongoni mwa barabara muhimu sana kwa watu na uchumi, inaunganisha bandari yetu ya Dar na barabara inayoelekea mikoani. Cha kusangaza barabara hii inajengwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa bila kukamilika. Pia wanaweka lami kwa vipande vipande. Pia kuna wakati mwingine huwaoni kabisa wakijenga chochote. Leo kulikua na foleni yaajabu sana, hii inatokana na magari kupita njia moja pale Buguruni. Hawa wajenzi wanasubiri kukicha ndio wanaweka vyombo vya kutengeneza barabarani wakati walitakiwa wajenge usiku ili asubui kupisha magari.
Je kwa hali hii tutafika? Kama barabara fupi tu isiyozidi km 20 inachukua zaidi ya mwaka mmoja na nusu je tutafika tunakotaka kufika? Maendeleo tutakua tukiyasikia redioni tu
 
Mkuu hyo barabara ni tatizo!
Tatizo la kutumia wakandarasi wa ndani, wakiambia hawawezi kazi wanabisha....
Naamini ikimalizika lazma huku kwingine walipoanza napo kuwe na matatizo(iwe imeharibika),

Politics everywhere, rushwa kila mahali...
 
Back
Top Bottom