Barabara ya Bagamoyo eneo la Africana yamemeguliwa na Mvua,(KUNA FOLENI YA KUTISHA!)

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Wapendwa wana JF nilikwama kwenye Foleni ya Magari Maeneo ya Africana kuanzia saa 7 na nusu na ndio nimefanikiwa kufika Boko muda huu baada ya kupita BODA KWA BODA ile inayopita Kilongawima maarufu( Kwa Mwamnyange) kufuatia maji mengi ya mvua yanayotoka maeneo ya Salasala Jogoo hivyo ninawasihi wanaotoka mjini kupita pale na wanaotoka Tegeta watafute njia Mbadala!
 
Yaani ile Barabara Maarufu ya Mwamunyange imesaidia sana kwani isingekuwepo leo ingelazimu kukaa Masaa zaidi ya 6 kwani Magari yalifungana sana...
 
Wapendwa wana JF nilikwama kwenye Foleni ya Magari Maeneo ya Africana kuanzia saa 7 na nusu na ndio nimefanikiwa kufika Boko muda huu baada ya kupita BODA KWA BODA ile inayopita Kilongawima maarufu( Kwa Mwamnyange) kufuatia maji mengi ya mvua yanayotoka maeneo ya Salasala Jogoo hivyo ninawasihi wanaotoka mjini kupita pale na wanaotoka Tegeta watafute njia Mbadala!

Wenzetu huko mvua inanyesha?
 
Asante kwa taarifa. Dah! Hili eneo! Majuzi magari yalifungana pale Mbuyuni, tangu saa 2 mpaka saa 5 ndio tulikuwa tunatoka. nadhani kuanzia sasa mpaka matengenezo yatakapokamilika sisi wakazi wa Boko na maeneo ya huko tutapata shida sana, lakini naona ndio gharama ya maendeleo hiyo
 
itatengenezwa kabla ya weekend.si unajua mkuu wa nchi lazima akapumzike huko bagamoyo.
 
Asante kwa taarifa. Dah! Hili eneo! Majuzi magari yalifungana pale Mbuyuni, tangu saa 2 mpaka saa 5 ndio tulikuwa tunatoka. nadhani kuanzia sasa mpaka matengenezo yatakapokamilika sisi wakazi wa Boko na maeneo ya huko tutapata shida sana, lakini naona ndio gharama ya maendeleo hiyo

Garama ya maendeleo kivipi?
 
Back
Top Bottom