Navojua mimi ile Eurobond ni govt security ila badala ya kuwa in tsh wanatumia euro, sababu kubwa ni euro interest rate iko chini. Ila hii ya stanbic sina uhakika itakuwa underlined in which currency presumably Tsh sababu ni local banks, hiyo itapunguza demand ya forex toka serikalini. vilevile ujue kuissue gov't bond ni sawa na kukopa maana serikali inabidi izilipe hizo bonds zikisha mature kwa hiyo ni ile ile suala ni riba.
Safari za nje wote tunakubaliana kuwa zimezidi na ni budi kwa serikali kuzipunguza na kuelekeza nguvu na muda wao kwa maendeleo ya wananchi.
Vilevile nafahamu hiyo sikuwa natoa mchanganuo wa GDP per capita la hasha, nilikuwa naangalia jumla ya matumizi ya serikali dhidi ya idadi ya wananchi, ukumbuke humu ndimo huduma za jamii (shule, hospitali) zinakotoka pamoja na mishahara ya watumishi wa umma.
Cha msingi tujadili ni namna gani serikali yetu iweze kuongeza bajeti na matumizi ya miradi ya maendeleo maana ya sasa haitoshi. vilevile sikubaliana na hawa WB kwamba serikali isikope kwingine maana cha msingi hatuwezi kutegemea WB kwa miradi yote. Tukumbuke pia kuwa moja ya sababu za ule mpango wa wafadhili kupunguza misaada na mikopo kwa Tz ni ukwasi uliozikumba nchi nyingi za magharibi baada ya mtikisiko wa uchumi.
sijaelewa link ya Eurobond kwenye hii debate but anyway labda huo ni mtazamo wangu. Kuhusu Bonds yes these bonds zinakuwa na interests ambazo kama umesoma finance kuna kitu term structure interest rate theory. Utakuta kwamba bond yeyote coupon yake inategemea na muda wa ule mkopo. Kikubwa ni kwamba Government inapokuwa imeissue bonds kwanza bonds zake zinakuwa lower risk exposure compare to kampuni ya kawaida. Pili wanakuwa na uwezo wa kudictate terms za mkopo na muda watakaolipa. Tuko pamoja? Sasa mie ninapoishauri serikali kwenda kwenye soko la mitaji tumelianzisha kufanya nini? Kwanini wasiuze bonds wakaruhusu watu wanunue wenye uwezo? That way inapunguza level of financial distress ambalo serikali italipata kwa kukopa katika financial institutions?
Kuhusu WB mie siwaambii kwamba wakope WB peke yake bali nawaambia kama wanataka waende kukopa katika Development Bank Institutions sio World Bank tu, kuna EADB, ADB etc. Pia they may ask for loan from some governments. Mbona US wamekopa from China? Kule kuna kuwa favourable terms kuliko kwenda kukopa katika local financial institutions ambapo mzigo mwisho wa siku unatuangukia sie watanzania. Nitakupa mfano mambo yakienda vibaya katika ulipaji wa mkopo inabidi iongeze spidi na umakini wa ukusanyaji kodi. Ikiwa itashindwa unadhani wapi watakimbilia kupakamua si kwasie walipa kodi ili kufidia ile deficit??? Sasa mwisho wa siku tutaumia sie walipa kodi ambao hatukuhusishwa in first place.
Labda nikuulize kwanini tukawa tunalipa ada za shule? tunajilipia huduma ya afya, tunachangia kodi ya barabara etc. Hizi ni njia mojawapo za kupunguza ukubwa wa budget yetu na kusaidia kuleta maendeleo