Banki tano zote zimeniambia sikopesheki japo nina asset kama dhamana

Mkuu unadhan ni peke yako umesoma nchi hii?.acha ujinga wewe usijifanye mjuaji wakat hapo ulipo ni matako tu huna mbele wala nyumba ukute unaishi kwa shemej yako na elim uliyonayo,
Daaah,,,unaweza kuwa umeongea ukweli ila umetumia maneno makali sana aiseee,,,taratibu jamani mtaua
 
Bora wamekunyima pengine ingekuja kukupa headache tu fikiri mfanyakaz wapewa 10ml alaf wanakukata almost 9yrs sizani wako fair ule sio msaada ila ni kukurudisha nyuma tu... Samahan ni mawazo yangu tu
 
Mkuu unadhan ni peke yako umesoma nchi hii?.acha ujinga wewe usijifanye mjuaji wakat hapo ulipo ni matako tu huna mbele wala nyumba ukute unaishi kwa shemej yako na elim uliyonayo,
Nsingekuwa mjuaji ma ma ko asingenipa huchi mwanangu.
 
kama umeajiriwa jaribu kusave atlist upate biashara ya mtaji mdogo kama laki tano au milion(usikatishwe tamaa na kafaida kidogo utakachokipata lengo ni kuweza kutengeneza records ya uwezo wako katika biashara) then ifanye kwa muda huku ukitunza rekodi zake na biashara jaribu kuiweka formal kidogo then ikiwa stable nenda pride au financial institution ndogo ndogo watakupa mkopo kubost biashara yako ndogo bila kusahau kutunza records zako za marejesho baada ya miaka miwili au mitatu nenda Nmb,Dcb,Acb and the like waombe Milioni 10-20 kwa biashara hiyo hiyo huku kwakuwaonyesha mzunguko wa biashra na uwezo wa kufanya marejesho na ukiweza kuyafanya ndani ya muda mfupi itakuongezea sifa ya kuongeza mkopo unaweza fika mpaka mil100. ukishafika mil100 na zaidi ndo uende uko barclays and the like watakupokea kwa heshima zote wakuhudumie then utakuja kwangu ntakufanyia VALUATION ya hiyo Nyumba yako ili ikae kama rehani ya mkopo. NB; nikasafari karefu kidogo kanahitaji kufanya maamuzi na kujitoa bila kusahau KUFOCUS.
 
Leo nlipita ktk bank 5 tofauti kuulizia taarifa za mikopo kwa wajasiliamali:niliwatembelea CRDB,NMB,TPB.Barclays na MUCOBA, kifuatacho ndicho nilichokipata:

1. CRDB,NMB,TPB na MUCOBA

Hawa jamaa wanakopesha wafanyakazi wa serikali au mfanyabiashara mwenye biashara tayari inamaana kwa sisi tunaohitaji mtaji kwaajili ya kuanza biashara hatuna nafasi regardless una asset gani ya dhamana..

Mfano mimi nina kiwanja kimepimwa pia kinajengwa lakini wamesema sina nafasi kwakuwa sina biashara inayorun.

2. Barclays wao ndo hawana mpango kabisa wa kukopesha mjasiliamali.
Kiukwel nimehuzunika sana kwa ubaguzi huu nina asset to be used as security bado nafanya kilimo lakin sikopesheki?, dah tufanyaje sisi??
Pole Sana
 
jaribu EQUITY
 
kwaniniusiuze hicho kiwanja?
Umeuliza swali zuri sana Miss MTAFUTAJI. Lengo la Benki si kukukopesha na kisha kuuza kiwanja chako. Ni bora auze mwenyewe kiwanja kama kweli anataka kufanya biashara kuepuka aibu ya mnada.
 
Umeuliza swali zuri sana Miss MTAFUTAJI. Lengo la Benki si kukukopesha na kisha kuuza kiwanja chako. Ni bora auze mwenyewe kiwanja kama kweli anataka kufanya biashara kuepuka aibu ya mnada.
nilimwambia akanimind kweli halafu utakuta bahati nzuri ana nyumba tayari nimefunga tu mdomo wangu hapa watu hawajui madhara ya mkopo ujue .
 
nilimwambia akanimind kweli halafu utakuta bahati nzuri ana nyumba tayari nimefunga tu mdomo wangu hapa watu hawajui madhara ya mkopo ujue .
Watu wanadhan kwenye biashara ni lazima wapate faida. Benki wanaangalia na uwezekano wa kupata hasara ndo maana wanataka kujirizisha na mzunguko wa biashara kabla ya dhamana. Usikute mleta mada kaenda benki hata business plan hana wakamwona mtupu akaja JF kulalama. WaTZ ndo tulivyo..!
 
huo muda wa kuzungushia benk biashara uwape hela si bora utafute hela yako ? unakuta mtu ana nyumba na viwaja 4 bado anakopa benk? ulinunua vya nini si akiba ikusaidie mbeleni incase of emergency? mtu ukishauri anakuja juu sasa huku kafata nini kama anataka tumshauri anachotaka si angefanya tu hukohuko?
 
Si kila mtu anaweza kufanya biashara au kuwa mjasiriamali. Ndo maana maprof' wanaofundisha biashara vyuo vikuu wamekubali kuajiriwa tu na kazi za ushauri kidogo ndo wanaingiza kipato cha ziada. Lakn huwaoni benki wakichukua mikopo ya biashara. Tafakari..!
 
Mikopo ya kibiashara iko hivyo kisura.! Hata kina Mengi wakikopa kuna vitu wanaweka rehani, fungua macho.
wajinga sana hao naona wameichukua discussion na kujipa utabiri mara oooh pengine ana nyumba nyingne au oooh hata business plan hana yaan full kujifanya watabir nimeamua kuwaangalia na ujinga wao....
wanatabir tabir utadhan sheikh yahaya
 
Mkuu, ujinga ni kudhani kuwa ukileta hoja ya kulalama humu wadau wote watakuonea huruma. Kwenye kutafuta elimu kuna kuchapwa viboko, matusi, kukatishwa tamaa na adhabu nyingine nyingi kutegemeana na medium of delivery na level yake. Unachokitafuta hapa wewe ni elimu kwa maana kwamba wewe ni mjinga katk masuala ya mikopo ya kibiashara, hujui vigezo vya kukufanya ukopesheke na taasisi za fedha. Hivyo, jitahidi kuwa na kifua cha kupokea changamoto na kuzitafsiri kwa mtazamo chanya utapata mengi ya kujifunza.

Hujui kama mabenki wanatumia utabiri kuamua kukukopesha au la..? Kama una business plan lazima utakuwa ume-include financial projections za biashara yako. Je, hizo projections sio utabiri wa namna gani biashara yako ita-perform kwa miaka 3 au zaidi ijayo..? Usiwe mwepesi wa kukata tamaa na kudhani umebaguliwa. Simama kwenye nafasi ya benki halafu mtu anakuja kwako humjui lakini anataka umkopeshe baada ya kusikia unatoa huduma hiyo. Wewe utamkopesha mara moja..? Nadhani hapana, lazima utajiridhisha katk yafuatayo:
  1. Utambulisho kwa vielelezo unavyovitaka (kwa benki ni; eneo la biashara, TIN na leseni ya biashara)
  2. Anataka mkopo kiasi gani na kwa ajili ya nini (kwa benki ni; business plan na sera ya benki kwa aina ya biashara inayoombewa mkopo i.e. si benki zote zinatoa mikopo kwa biashara ya kilimo)
  3. Historia na uwezo wa kurejesha mkopo katk muda mtakaokubaliana (kwa benki ni; financial records za biashara yako kwa kipindi flani i.e. hawakopeshi biashara inayoanza ili kupunguza risk kwa kufanyia kazi facts badala ya projections peke yake)
  4. Ikiwa atashindwa kurejesha katk mazingira ya kawaida kuna njia gani ya kurejesha pesa yako (kwa benki ni; dhamana au bima).
Pia, tunatakiwa kujua kwamba pesa ya benki ni ya wateja wa fixed deposits na wanahisa, hivyo, BoT wanatoa guidelines kwa mabenki yote kulinda pesa za wateja na kuepuka kulipa fidia ikitokea benki imefilisika. Na hapo ndo urasimu unapoanzia au tuseme umakini katk utoaji mikopo. Mfanyabiashara siku zote ni mtu anayejishusha na ndiyo maana wasomi wengi kwa kujikweza hawawezi kufanya biashara. Ukikubali kujishusha utasaidiwa..!

Eng. WFM
 
Inasikitisha sana....Bank hawataki kusikia kitu inaitwa entrepreneur
 
Back
Top Bottom