Bank ya crdb heshimuni wateja

Samawati

Member
Oct 6, 2010
90
71
Nitaanza kwa kuwapeni pongezi kwa kujitahidi kuwa benk nzuri
yenye kupanuka siku hadi siku na kujitahidi kuboresha huduma.
Mmekuwa mkijitahidi kuboresha taratibu zenu ili kukidhi matakwa ya wateja.

Hata hivyo, katika kufanya hivyo kuna machache yanajitokeza na inabidi myatatue
ili msizidi kuwaudhi wateja na kusababisha wahamie bank nyingine.
Nitaelezea machache ambayo nimeyashuhudia mwenyewe.

1. Huduma za ATM
Inasikitisha kuona kwamba ATMs zenu zimeanza kuwa kero kubwa.
Ukienda ATM za Namanga,au ile iliyoko barabara ya TPDC, kuna usugu wa kutokuwa
na pesa.Hii Inaudhi sana.Pia ukienda ATM za bank nyingine zenye VISA/MASTER CARD nako
kero ni kupata message " your issuer is not recognized at the moment" au kitu
kama hicho. Inakera sana

2.Foleni
Mmeweka utaratibu wa kutoa namba.Huu ni utaratibu mzuri kama
kaunta nazo zitaitikia kwa ufanisi.Haiingii akilini kwa mfano kuwaketisha watu kwa masaa
huku umewapa namba, halafu kaunta nyingine zimeandikwa "CLOSED" na kubakiza kaunta moja au mbili
tu zikifanya kazi.Mnamdanganya nani? Kibaya zaidi kiwango cha juu kutoa kwenye ATM ni
1m. ikizidi hata senti moja zaidi inabidi upange foleni hii ya kuudhi kwa masaa.
Kuna siku nimepanga foleni masaa matatu CRDB Mlimani City. Hii inaudhi sana.

Jirekebisheni kwa hili.

3.Huduma nyingine kwa wateja
Nawapongeza kwa kuanzisha Mikocheni branch japo iko mbali mno.
Kwa mtu asiye na gari kufika huko siyo urahisi maana kulivyojificha mhh! na pia
kuna na "private" road inayozuia magari yasiyo private kuingia humo!
Uzuri wa Mikocheni branch na ugumu kufikikika ni kwamba hakuna msongamano
wa watu. Ukienda hukai hata nusu saa bila kupata huduma.
Kibaya nilichokiona hapa ni kushindwa kuwaheshimu wateja kwa maana ya huduma
ya maliwato!Inaingia akilini kweli mtu kuja mbali kote kule,
halafu kushindwa kumsaidia huduma ya mahali pa kujisaidia?
Nilishangaa sana kuona mama mjamzito akielekezwa na walinzi aende chooni nje karibu na
gate la walinzi ambako kuna choo kimoja cha walinzi ambao ni wanaume!!

Mama yule alishindwa kutumia choo kile maana alijisikia kudhalilishwa! Alipoomba kutumia toilet ya ndani ya
bank alikataliwa na kuambiwa ati hizo ni za staff! JAMANI! CRDB MNASAHAU HIZO PESA MNAZOJENGEA
NI PESA ZA WATEJA MNAOWANYANYASA??
KUWENI WASTAARABU! MHESHIMIWA DR KIMEI NADHANI UKIWA KAMA BABA UNAJUA
MATESO WAYAPATAYO MAMA WAJAWAZITO wakiwa kwenye hali hiyo! CHUKUA HATUA KABLA WAKINA MAMA
HATUJAANZA KAMPENI YA KUSUSIA BANK YAKO YA CRDB!
 
ukienda knye website ya crdb kuna sehemu ya maoni nashauri nako uweke yatawafikia kwa haraka zaidi, unayosema ni kweli nimefanya kazi crdb for 7yrs nimeshuhudia yote hayo kuna baadhi ya staff hawako makini
 
Mfumo wa bank zetu na matumizi ya kadi bado yako karne ya 18. Foleni kwenye mabank inaudhi sana. Mimi ni mteja wa crdb, kweli ukienda bank ujue hiyo siku imesha, manake utakaa hapo kwa masaa. ushauri wangu
1. Watu wajifunze kutumia kadi kununua vitu kama mafuta (petrol / diesel)
2. Wafanyabiashara wawe na systems za wateja kununua vitu kwa kutumia kadi
3. Bank ziweke mashine nyingi ambazo zinaweza kutumika kuweka na kutoa hela bila kuingia bank
4. Watu wajitahidi kutumia huduma za internet banking zinasaidia sana. Mimi nimepunguza sana kwenda bank kwa kutumia huduma hii.

Kwa wenzetu (first world) ni mara chache kukuta foleni bank.

INAWEZEKANA TUBADILIKE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom