Bandari wazuiwa kufichua uozo kwa JK

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Bandari wazuiwa kufichua uozo kwa JK


na Hellen Ngoromera


amka2.gif
AHADI ya Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), kuonana na Rais Jakaya Kikwete kupitia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), imeyeyuka.
Pamoja na mambo mengine, DOWUTA ilipanga kuonana na Rais ili kumweleza uozo wa bandari ikiwemo kupuuzwa kwa agizo la Rais Kikwete kutaka bandari kutobinafsishwa.
Akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalumu, Katibu Mkuu wa DOWUTA, Abdallah Kibunda, alisema chama hicho kupitia TUCTA kilipanga kuonana na Rais Kikwete kupitia Wizara ya Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana tangu mwaka jana lakini matokeo yake azma yao haikutimia.
Dowuta ilipanga kuichongea kwa Rais Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kutokana na kukiuka agizo lake la kutaka bandari kutobinafsishwa.
Katibu mkuu huyo alisema kwa sasa ni ngumu kutimiza azma yake ikizingatiwa kuwa Rais huyo ni mpya kwa maana ya kuingia madarakani katika awamu nyingine ya miaka mitano.
“Kwa kawaida vyama vya wafanyakazi huonana na mheshimiwa Rais kupitia shirikisho letu la TUCTA, mwaka jana tulifanya jitihada za kuonana naye lakini ilishindikana.
“Mratibu mkuu wa utaratibu huu ni Waziri wa Kazi. TUCTA iliratibu ajenda za vyama na kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambapo DOWUTA tulikuwa na ajenda tatu,” alisema Kibunda.
Alizitaja ajenda hizo kuu tatu kuwa ni serikali kuacha kabisa dhamira yake ya kubinafsisha bandari za nchi kwa mtindo wowote ule.
Alisema hatua hiyo ya Rais kutotaka bandari kubinafsishwa ilizua mtindo wa kuvigawa baadhi ya vitengo kwa mtindo wa kushirikisha sekta binafsi.
Ajenda nyingine ni vyama vya wafanyakazi kutoshirikishwa katika vyombo vya maamuzi ya mstakabali wa taifa vya kutunga sheria wakati ni jambo lisilo na mashaka kwamba vyama hivyo ni wadau na washiriki wakuu wa kudai uhuru wa nchi.
“Wafanyakazi pia ni wachangiaji wakuu wa uchumi wa maendeleo wa nchi yoyote ile. Ni tabaka muhimu katika taifa lolote hivyo DOWUTA tulitaka kumkumbusha mheshimiwa Rais kupitia vikao hivyo,” alisema.
Alimshauri Rais kuwa na ratiba inayoeleweka ya kukutana na vyama vya wafanyakazi kupitia TUCTA kwani nafasi hiyo itamwezesha kuweza kufahamu mambo mbalimbali ya nchi.
Alisema tabaka la wafanyakazi ni muhimu katika nchi kwani linabeba wasomi na wataalamu mbalimbali hivyo ikiwa atalitumia vizuri atafaidika katika utendaji kazi wake.
 
Our faith ought to be anchored in strong institutions but not strong African leaders...............................
 
Back
Top Bottom