"Bambo" apata ajali mbaya

mjunguonline

Member
Mar 10, 2011
73
5
Msanii wa sanaa ya uchekeshaji Dickson Makwaya a.k.a "Bambo mzee wa kuchamandi" amepata ajali mbaya ya kugongwa na gari akiwa katika pikipiki maeneo ya Kigogo Mbuyuni jana usiku. Hali ya msanii huyo si nzuri sana na ameumia sehemu kubwa ya mwili wake na inasemekana kuwa amevunjika mfupa wa paja. Msanii huyo amelazwa wodi ya wagonjwa wa mifupa MOI na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji Asubuhi hii. Mungu amsadie arudi katika hali yake ya zamani.Mzee wa "Aluuu....,Kukuluka mwanangu....Huwezi kupasua Godoro!
 
Jamani TOYO bila shaka ita2malizia wasanii we2 wajaribu kuepuka kupanda jamani. Mmmmmhh!
 
Jamani TOYO bila shaka ita2malizia wasanii we2 wajaribu kuepuka kupanda jamani. Mmmmmhh!

Kwani unadhani wanapenda kupanda hizo TOYO tatizo Bongo gari bado ni anasa, wewe fikiria kistarlet tu bila millioni 6 bado haujakimiliki. boda boda zitatumaliza sana na kusababishiwa ulemavu wa viungo kwa jamii pana ya Tanzania.
 
Pole sana Bambo.
Wandugu pikii piki usiku msipande kabisa, Angalieni rate ya ajali za piki piki kati ya usiku na mchana and you will not the huge difference
 
Hizi pikipiki zitatumaliza kwani kila uchao ni vifo vya pikipiki... nadhani kwa sasa vinaongoza kuliko vifo vya sababu nyingine... Pole Bambo...
 
Hizi ndizo ambazo Baba Riz alizisifia kuwa zimeongeza ajira? akasahau pia zimeongeza ajali..... akili matope..
 


Wasanii wenzake na Bambo wakiwa na sura za majonzi mara walipofika hospitalini kumwona mwenzao Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo aliyelazwa kitandani.


IMG_2392.jpg
Picha ya dereva wa pikipiki waliyopata nayo ajali alfajiri ya leo.

IMG_2396.jpg
Picha ya Bambo

IMG_2385.jpg
 

Attachments

  • IMG_2385.jpg
    IMG_2385.jpg
    17.9 KB · Views: 105
Pole sana Bambo, mungu atakusaidia
Epuka pikipiki wapendwa au ukipanda hakikisha unampa mashariti dreva atakayekubeba
 
augue salama
Tuombe i wasimshughulikie kama wahanga wa bodaboda manake pale moi si mchezo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom