BALOZI ZETU NJE YA NCHI: wapi zipo na wapi hazipo?

Balozi za Tanzania

Ubelgiji- Pia unashughulikia uhusiano na Luxembourg, Uholanzi, European Union na ACP/EU, lakini tuna consulate pia Uholanzi sijui hasa kazi yake ni nini

Afrika Kusini unashughulikia mambo ya Namibia, Lesotho, Botswana na SADC
Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda, UAE, Zimbabwe, Msumbiji(unashughulikia pia mambo ya Mauritius)
Marekani unashughulikia pia, Benki ya dunia, IMF, Venezuela, Brazil, Argentina na Mexico

Canada pia unashughulikia uhusiano na Cuba

China pia unashughulikia uhusiano na Vietnam, Laos, Cambodia, Mongolia, Thailand and the Democratic People's Republic of Korea (DPRK)

DRC pia unashughulikia Gabon, Central African Republic, Cameroon na Congo Brazzaville

Misri pia unashughulikia mambo ya Israel, Lebanon, Palestine, Libya, Iraq na Syria

Ethiopia pia unashughulikia mambo ya Eritrea, Djibout, Yemen, AU na ECA

Ufaransa pia unashughulikia mambo ya Spain, Portugal, Algeria, Morocco, Tunisia, UNESCO

Ujerumani unashughulikia pia mambo ya Switzerland, Poland, Czech, Slovakia, Hungary, Bulgaria, Rumania, Austria na Holy See(sina hakika kama bado iko hivi)

India unashughulikia pia mambo ya Sri Lanka, Nepal, Bangladesh, Myanmar, Malaysia, Singapore, Indonesia na Brunei Darusalaam

Italia unashughulikia mambo ya Greece, Albania, Serbia and Montenegro, Croatia, Slovenia, Bosnia-Herzegovena, Serbia, Turkey, IFAD, FAO na WFP

Japan unashughulikia pia mambo ya Phillipines, South Korea, Australia, New Zealand na Papua New Guinea

Kenya unashughulikia mambo ya Sudan, Seychelles, Somalia, UNEP na HABITAT

Nigeria unashughulikia mambo ya Benin, Togo, Cote d'Ivoire, Guinea, Senegal, Mali, Liberia, Sierra Leone, The Gambia, Burkina Faso, ADB na ECOWAS

Russia unashughulikia mambo ya Belarus, Georgia and Ukraine

Saudia unashughulikia mambo ya Oman, UAE, Pakistan, Iran, Qatar, Bahrain na Kuwait
Sweden unashughulikia pia mambo ya Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia na Lithuania

Umoja wa mataifa pia unashughulikia mambo ya UNDP, UNICEF, UNFPA, Jamaica, Trinidad and Tobago, Barbados na Guyana.

Uswisi unashughulikia pia mambo ya UN kwenye ofisi za Geneva na Vienna
Uingereza unashughulikia nchi za UK Ireland na jumuiya ya madola

Zambia unashughulikia pia Angola Sao Tome na Principe, COMESA (sina hakika kama bado ina function)

watu wa wizara ya mambo ya nje wanaweza kutuambia zaidi, maana wao ndio insiders wanajua vizuri. Lakini muulizaji aliuliza swali kwanini Sudan, na hasa uhusiano kwenye elimu ya dini.

Foreign Policy yetu kwa kweli haileweki, kidogo ilianza kuwa na shape wakati wa Mkapa lakini sasa ni kama haina mwelekeo, bado balozi haina majukumu makubwa ya kunufaisha nchi zaidi ya kuwa ni kama symbols of unity. Unaweza kuona hata Jamaica tuna uhusiano nayo hata Eritrea, why? ni kama tunaiga tu hatujui ni nini hasa tunataka.
 
Afrika Kusini unashughulikia mambo ya Namibia, Lesotho, Botswana na SADC
Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda, UAE, Zimbabwe, Msumbiji(unashughulikia pia mambo ya Mauritius)
Marekani unashughulikia pia, Benki ya dunia, IMF, Venezuela, Brazil, Argentina na Mexico

Asante Mkuu kwa kutufahamisha vizuri ingawa nadhani kuna masahihisho ya hapa na pale. Tuna ubalozi Burundi-4 UN rd Bujumbura, Rwanda,Uganda, UAE-No S6A! Nasr Street Khalidiyah, Abu Dhabi, Zimbabwe-Ujamaa House, 23 Baines Avenue(unashughulikia pia Mauritius). Hizi nimezitoa kwenye website ya moja ya balozi zetu na hata yenyewe bado inamatatizo ya overlapping, k.m. Saudi Arabia inasemwa ndiyo inashughulikia UAE wakati inasema tuna ubalozi UAE. Tukirudi kwenye swali la msingi, asante kwa kutufahamisha kuwa Sudan inashughulikiwa na Ubalozi wa Kenya na sio Misri au Ethiopia kama wengine tulivyodhani. Kinachonishangaza ni ukimya wa mtoa mada maana pamoja na makelele yote ya kuomba ufafanuzi amekaa kimya wakati mwanzoni alikuwa anawasihi watu wachangie! Kwa mtaji huu......
 
kwani kuna tatizo na kuwa na uhusiano wa kibalozi na eritrea na jamaica?

uchaguzi wa ubalozi wetu upi utuwakilishe pia katika nchi nyingine huzingatia zaidi ya mambo mengi zaidi ya ukaribu wa nchi zinazohusika ndio maana ubalozi wetu new delhi hautuwakilishi pakistan bali ni ule wa saudia.
 
Fundi Mchuno, IDIMI na wengine yapasa tuwe na positive thinking.
Binafsi nilianzisha mada nikawa nimepitiwa na shughuli zingine za kimaisha, na kila nilipokuja JF mada za mafisadi zilinishughulisha. sie wengine sio waandishi wa habari, bali muda ambao umeshoka kikazi unaingia ktk JF ADDICTION...

Kuna Mpuuzi namwita samahani kwa kusema tuna uhusiana wa Masomo ya DINI na Sudan. Ni Mvivu kufikiri. Sudan inatoa nafasi nyingi za vijana kusoma Medicine na Engineering free of charge.its like Italy. Suala laweza kuja wanaofaidika ktk dini gani, hili hapa halina nafasi kwani kila sehem lipo kundi linalonufaika kivyake.

Bongolander nafikiri kuna masahihisho mengi hajawekwa ktk hio websites, na huo ni UVIVU wa viongozi wetu kupdate infomation. Haiwezekane Balozi wa UAE aje ashughulike na Burundi, hata zile sababu za awali za Uchumi zitakuwa none sense.

Hapo Nyuma TZ walikuwa na Ubalozi Saudia ukiwakilisha UAE, hivi sana mambo yamebadilika, UAE wan full baloz, hadi dubai wana consulate, nafikiri hali ni hio kwa Malaysia tayari balozo ameshachaguliwa logistics tu zimebakia. Huko sababu za kibiashara ndizo wanazozitoa.

Kimsingi nakubaliana na sababu za kiuchumi za baadhi ya nchi kuwa na balozi mmoja atakae kuwa anafanya usimamizi nchi zingine. ila kama walivyozungumza members wengine kuwa baadhi au wengi wa balozi zetu zimelala usingizi FOFOFO.

Sudan ubalozi unasaidia si wa Kenya,nafikiri kati ya Eritrea au Ethiopia. Niliuliza hili kimsingi kwani wanafunzi wanaosoma SUDAN wakati wa kubadilisha Passport wanatakiwa warudi DSM kubadilisha, nafasi ya Balozi kufanya kazi kama hizi hazipo.kama tulivyodiscuss huko nyuma familia nyingi za TZ zipo Taabani, nauli nayo inakuwa mtihani. Kama mmefanya utafiti utakuwa vijana wengi walokwenda kusoma nchi za Russia na dunia ya tatu, utasikia wanakaa zaid ya miaka 3 au wengine hadi wanamaliza masomo yao ndio warudi bongo, hawawezi Rudi likizo kwani Nauli wanakuwa wanakosa.

thanks kwa washangiaji...wengine wameweza jifunza pia.
 
Kuna Mpuuzi namwita samahani kwa kusema tuna uhusiana wa Masomo ya DINI na Sudan. Ni Mvivu kufikiri. Sudan inatoa nafasi nyingi za vijana kusoma Medicine na Engineering free of charge.its like Italy. Suala laweza kuja wanaofaidika ktk dini gani, hili hapa halina nafasi kwani kila sehem lipo kundi linalonufaika kivyake.

Mbona unajihami Mkuu? Si useme tu ni wafuasi wa dini gani wanaofaidika na hizo skolaship? Kwani huko kwingine wanaenda watu wa dini za huko peke yao? Pengine wakatoliki peke yao ndio wanaoenda Italia! Waluteri Skandinavia!

Sudan ubalozi unasaidia si wa Kenya,nafikiri kati ya Eritrea au Ethiopia.

Sudan inashughulikiwa na balozi wetu aliye Kenya. Nenda kwenye website ya balozi yetu yeyote utapata habari hizi. Eritrea hatuna ubalozi.
 
FUndi Huna data au piga simu ubalozi uulize kwa mambo usoyajua.

1.Kuhus Balozi ani anahudumia Sudan kwa data nilizonazo si Kenya.Lengo si kushindana nani anajua nani hajui,mie nimeeuliza hilo kwa lengo zuri,Hii itasaidia vijana wetu wanaonataka kurudi TZ wabadilishe passport,badala yake wanaweza kwenda nchi ya karibu.

2. please usilete issue za Scholarship za nchi mbalimbali wanaofadika kina nani...na then u-compare hayo unayoyasema. Pia inavyoonekana ulijiunga late JF, nenda ktk mada za elimu kule kulijadiliwa issue za kuwepo shule za kidini Tanzania. pitie kule.
 
Nina mwezi tu katika hii forum kwa hiyo nakiri ukinda wangu. Sasa Mkuu unataka kuniambia kuwa tuna ubalozi Eritrea? Ulipiga simu Foreign ukaambiwa hivyo? Cha haraka zaidi ni kwenda kwenye web site zao na utapata uhakika wa nani anashughulikia Sudan. Haiwezi ikawa baada ya kuongea nao ukaja na jibu kuwa ni aidha Eritrea au Ethiopia! Ungeambiwa nchi gani katika hizo mbili ndio inawajibika. Hili la dini umeliingiza mwenyewe. Ume'hint' kwamba kuna upendeleo wa aina fulani halafu kwa sababu unazozijua mwenyewe ukaendelea kuzuia mjadala. Sasa, ndugu yangu, kwa kifupi, kwa vile umeshasema kuna upendeleo, naomba unieleze ni nani anayependelewa. Ni kwa kabila? Ni kwa dini? Hizo skolaship zinatolew kwenye shule za dini tu? kama ni hivyo, uwazi wake uko wapi? Hili jukwaa siyo kibanda cha kunywa chai kwamba mliotangulia ni lazima muaminiwe kwa sababu tu mliwahi humu. Ukitoa hoja isiyoeleweka utaulizwa. Ndio maana ya hii forum. Ndugu yangu,jaribu kuwa muwazi zaidi. Kama interest yako ni katika dini sema tu. Hakuna ubaya katika hilo. Ili tu usitufanye sisi wengine ni wajinga kwa kujaribu kupenyeza ishu zako kwa visingizio vingine. Unataka kuniambia hoja yako ni kuwa unataka serikali ifungue ubalozi ili vijana walio huko wabadilishe passpoti zao kirahisi? Mbona wanafunzi wametapakaa nchi nyingi tu ambako aidha hakuna ubalozi au kama upo umbali sana ( kwa mfano marekani kuna watanzania California na ubalozi uko washington n.k)! Wewe umeona Sudan tu!
 
Mkuu Chuma, hii nimeitoa sasa hivi kwenye Tanzania Natonal Website. Nadhani inakujibu kuhusu nani anasimamia mambo ya Sudan. Siyo siri tena, hakuna haja ya kumjua mtu foreign kwenye hili. Aliyekufahamisha amekuingiza mkenge. Heri ungetangulia kwenye mtandao. kuna mengi humu,si JF peke yake.
ADDIS ABABA

Embassy of the United Republic of Tanzania

P.O. Box 1077

Addis Ababa

Ethiopia

Tel. (251-1) 518155, Direct Line: (251-1) 511063 Fax: (251-1) 517358,

E-mail: tz@telecom.net.et

Accreditation to: Ethiopia, Organisation of African Unity (OAU),

United Nations Economic Commission for Africa (ECA), Eritrea, Djibouti

and Yemen



BEIJING

Embassy of the United Republic of Tanzania

No.53 Dong Liu

San Li Tun

Beijing

China

Tel.: (86-10) 65322344, (86-10) 65321719, (86-10)65325572, Fax (86-10)

5321695, (86-10) 65322394

E-mail: tzbeijing@iuol.cn.net or tzbeijing@info.ioul.cn.net

Accreditation to : People’s Republic of China, Thailand, Democratic People's Republic of Korea, Cambodia,Vietnam, Laos and Mongolia



BONN

Theaterplatz 26, 5300 Bonn 2,

GERMANY

Tel: (49-228) 358514 (49-228) 353219 Fax: (49-228) 358226

E-mail: tzbonn.habari@t-online.de

Accreditation to : Germany, Switzerland, Czech Republic, Slovakia, Hungary, Bulgaria, Romania, Austria and Vatican



BRUSSELS

363 Avenue Louise, 11050 Brussels

Belgium

Tel: (32-2) 6406500-27, (32-2) 64764749,

Fax : (32-2) 6468026

E-mail : tanzania@skynet.be

Accreditation to: Belgium, Luxemborg, The Netherlands, European Union

and ACP/EU



CAIRO

11 Abou Karamat

Cairo

EGYPT

Tel (20-2) 3374155/337486/3457559

Fax (20-2) 3457559

E-mail; tanrepcairo@infinity.com.eg

Accreditation to: Egypt, Israel, Lebanon, Palestina, Libya, Iraq and Syria



GENEVA

47 Avenue Blanc, CH 1201 Geneva,

Switzerland

Tel: (41-22) 7318920/7323752/ 7319461/ 7328255 Fax: (41-22) 7328255

E-mail: mission.tanzania@itu.ch

Accreditation to: UN Offices in Geneva and Vienna



HARARE

High Commission for the United Republic of Tanzania

Ujamaa House, 23 Baines Avenue

Harare, P.O.Box 4841

Zimbabwe

Tel: (263-4) 721870/722627

Fax: (263)724172

Email. tanrep@icon.co.zw

Accreditation to: Zimbabwe and Mauritius



KAMPALA

6 Kagera Road

P.O.Box 5750

Kampala

Uganda

Tel: (006-41) 256272/257357/342306

Fax (006-41) 343973/075-787838

E-mail : tzrepkla@imul.com

Accreditation to: Uganda and Burundi



KIGALI

Boulevard de L`

uganda

Telecom House

Block C 2nd Floor

Cacyiru B.P. 3973

Kigali

RWANDA

E-mail ; tanzarep@rwandatel1.rwanda1

Accreditation to Rwanda only



KINSHASA

142 Boulevard 30 Jin B.P.1612

Kinshasa

DRC

Tel 34364

Accreditation to: Democratic Republic of Congo, Gabon,

Central African Republic, Cameroon, and Congo-Brazaville



LAGOS

8 Agoro Odiyan Street, Victoria Island

P.O. Box 6417

Lagos

Nigeria

Tel: (00234-1) 613604

Fax : (00234-1) 610016/618908

Accreditation to Nigeria, Benin, Togo, Cote d`Ivoire, Ghana, Guinea, Senegal, and ADB



LONDON

43 Heartford Street,London W1Y 8DB

Tel: (44-207) 4998951/ 4993627

Fax: (44-207) 4993627

E-mail ; tanzarep@tanzarep.demon.co.uk

Balozi : balozi@tanzarep.demon.co.uk

Trade Centre UK: Trade+Tourism@tanzania-online.gov.uk

Accreditation to:United Kingdom, Ireland and Commonwealth



LUSAKA

Ujamaa House, No. 4200,

United Nations Avenue,

P.O. Box 31219, 10101 Lusaka,

ZAMBIA

Tel.(260-1) 243222-4, 250826

Fax ( 260-01) 254861

E-mail- tzreplsk@zamnet.zm

Accreditation to: Zambia, Angola, Malawi, Sao Tome and Principe



MAPUTO

Ujamaa House,

P.O. Box 4515

Maputo

MOZAMBIQUE

Tel: (258-1) 490110-3, 491165

Fax: (258-1) 494782

E-mail : ujamaa@zebra.eum.mz

Accreditation to:Mozambique, Swaziland, Comoros and Madagascar



MOSCOW

Pyatniskaya, Ulitsa 33

Moscow,

Russia

Tel(7-095) 9538221, 9530940, 9566130, 9534975, 2349045

Fax : (7-095) 9566130

E-mail; tzmos@wm.west.call.com, Accreditation to: Russia, Belarus, Georgia and Ukraine



NAIROBI

Taifa Road

Re-insurance Plaza, 9th Floor

P.O. Box 47790

Nairobi

KENYA

Tel: (005-2) 331056-7, 331104 , 218269

Fax (005-2) 218269

E-mail: tanzania@user.africaonline.co.ke

Accreditation to:Kenya, Sudan, Seychelles, Somalia,

UNEP and HABITAT



NEW DELHI

10/1 Sav Priya Vihar

New Delhi 110016

INDIA

Tel: (91-11) 6853046-7, 6968409, 6968406-7

Fax: (91-11) 6968410

(Accreditation to: India, Sri Lanka, Nepal, Bangladesh and Myanmar



NEW YORK

205 East 42nd St.

NY 10017,

New York,

U.S.A

Tel. (1-212) 9729160,9729123

Fax: (1-212) 6825232

E-mail- TZREPNY@AOL.COM

Accreditation to: UN and its specialized agencies UNDP, NICEF, UNFPA, Jamaica, Trinida and Tobago, Barbados and Guyana



OTTAWA

50 Range Road Ottawa

Ontario K1N 8J4

CANADA

Tel: (1-613) 2321509, 7331349

Fax: (1-613) 2325184

E-mail;Tzottawa@synapse.net

Accreditation to: Canada and Cuba



PARIS

13 Av. Raymond, Poinacare

75116 Paris,

France

Tel: (33-1)53706368, 53706369,53706370

Fax (33-1) 47550546.

E-mail: tanzanie@infonie.fr

Accreditation to: France, Spain, Portugal, Algeria, Morocco, Tunisia, and UNESCO



PRETORIA

845 Goont Avenue

P.O. Box 56572, Arcadia

Pretoria 0007

South Africa

Tel: (012) 3424371-93, 3426378-9, 3424562

Fax: (012) 4304383

E-mail; tanzania@cis.co.za

Accreditation to: South Africa, Namibia, Lesotho, Botswana and SADC



RIYADH

P.O. Box 94320, Riyadh 11693

Saudi Arabia

Tel. (966-1) 4542833, 4549660

Fax: (966-1) 4565361

E-mail: tzriyad@deltasa.com or Nhende@deltasa.com

Accreditation to: Saudi Arabia, Oman, U.A.E, Pakistan, Iran, Qatar, Bahrain and Kuwait



ROME

Embassy of the Unite Republic of Tanzania

Via Cesare, Beccaria 88

00196 Rome,

Italy

Tel: (39-6) 36005234, 32651471,

Fax (39-6) 3216611

E-mail : tanzarep@pcg.it

Accreditation to: Italy, Greece, Albania, Yugoslavia, Croatia,

Slovenia, Bosnia- Herzegovena, Serbia, Turkey, FAO, IFAD and WFP.



STOCKHOLM

Oxtorgsgatan 2-4,Box 7255,103-89

Stockholm

Sweden

Tel. (46-8) 244870, 203526

Fax (46-8) 109815, 203526

E-Mail: mailbox@tanemb.se

Accreditation to: Sweden, Denmark, Finland, Norway, Iceland,

Estonia, Latvia and Lithuania



TOKYO

21-9, Kamiyoga 4,Chome Setagaua-Ku

Tokyo 158

Japan

Tel.(81-3) 34254531-3, 34284227

Fax: (81-3) 34257844,

E-mail; Tancon@user.africaoline.co.ke

Accreditation to Japan, South Korea, Philippines, Australia



WASHINGTON

2139 R, Str, NW.

Washington D.C.

200008 U.S.A

Tel: (1-202) 8841080, 8841082

Fax: (1-202) 7977408

E-mail: Balozi@ tanzaniaembassy-us.org

Accreditation to: USA, World Bank, International Monetary Fund (IMF), Argentina, Brazil, Mexico and Venezuela.



DUBAI

Tel: (971-4) 2957770, 2957600

Fax: (971-4) 2957266
 
Foreign Policy yetu kwa kweli haileweki, kidogo ilianza kuwa na shape wakati wa Mkapa lakini sasa ni kama haina mwelekeo, bado balozi haina majukumu makubwa ya kunufaisha nchi zaidi ya kuwa ni kama symbols of unity. Unaweza kuona hata Jamaica tuna uhusiano nayo hata Eritrea, why? ni kama tunaiga tu hatujui ni nini hasa tunataka.

Kama sera yetu ya mambo ya nje ilikuwa inaeleweka wakati wa Mkapa basi na sasa inaeleweka, kumbuka kwamba Sera haijabadilika, lakini waweza sema utendaji uko vipi!

By the way mimi naona siku hizi ndio tuna-policy inayoeleweka zaidi kuliko kipindi chote!!! siku hizi balozi zinapimwa kwa kuongeza biashara kati ya nchi husika na Tanzania
 
FUndi Huna data au piga simu ubalozi uulize kwa mambo usoyajua.

1.Kuhus Balozi ani anahudumia Sudan kwa data nilizonazo si Kenya.Lengo si kushindana nani anajua nani hajui,mie nimeeuliza hilo kwa lengo zuri,Hii itasaidia vijana wetu wanaonataka kurudi TZ wabadilishe passport,badala yake wanaweza kwenda nchi ya karibu.
2. please usilete issue za Scholarship za nchi mbalimbali wanaofadika kina nani...na then u-compare hayo unayoyasema. Pia inavyoonekana ulijiunga late JF, nenda ktk mada za elimu kule kulijadiliwa issue za kuwepo shule za kidini Tanzania. pitie kule.

naamini utaratibu ni kwamba afisa wa ubalozi alikuwa anakwenda kwenye nchi ambazo ubalozi upo accredited na kutoa huduma ya passport mpya. labda palitokea utata wa mawasiliano kati ya watanzania waliopo sudan na ubalozi wetu kenya. suali je balozi au afisa ubalozi wetu nairobi anafika sudan kuonana na watanzania wa huko? je watanzania sudan wamefanya jitihada za kuonana na balozi/afisa ubalozi wetu kenya au ndo walikuwa wanatuma mawasiliano addis?
 
Fundi,

habari za web za serikali yetu hazipo updated.
nimecopy kwako:
RIYADH

P.O. Box 94320, Riyadh 11693

Saudi Arabia

Tel. (966-1) 4542833, 4549660

Fax: (966-1) 4565361

E-mail: tzriyad@deltasa.com or Nhende@deltasa.com

Accreditation to: Saudi Arabia, Oman, U.A.E, Pakistan, Iran, Qatar, Bahrain and Kuwait

Chini kabisa ukaweka Dubai, wakati Dubai sio NCHI, nchi ni UAE.
Ukiangalia utakuta ubalozi wa Saudia una handle issue za UAE na Qatar, wakati sasa tunavyoongea Qatar na UAE TZ wana ubalozi miaka kadhaa sasa. Huu ni uzembe wa Asasi zetu zinazosimamia infomation. Vijana wanalala kupiga story kusbiri mshahara na kudai kuonngeza mshahara wakati info za two lines wameshindwa ku-edit. ndo maana nikasema hizi info ni za zamani...within 2 years kuna mabadiliko makubwa.

Hoja za Kafara ni za Msingi if at all Balozi wetu nairobi anahusika huko. Kimsingi Balozi zetu za sijui..may be london ndio ipo ACTIVE.zingine zahitaji PUSH.
 
Nina mwezi tu katika hii forum kwa hiyo nakiri ukinda wangu. Sasa Mkuu unataka kuniambia kuwa tuna ubalozi Eritrea? Ulipiga simu Foreign ukaambiwa hivyo? Cha haraka zaidi ni kwenda kwenye web site zao na utapata uhakika wa nani anashughulikia Sudan. Haiwezi ikawa baada ya kuongea nao ukaja na jibu kuwa ni aidha Eritrea au Ethiopia! Ungeambiwa nchi gani katika hizo mbili ndio inawajibika. Hili la dini umeliingiza mwenyewe. Ume'hint' kwamba kuna upendeleo wa aina fulani halafu kwa sababu unazozijua mwenyewe ukaendelea kuzuia mjadala. Sasa, ndugu yangu, kwa kifupi, kwa vile umeshasema kuna upendeleo, naomba unieleze ni nani anayependelewa. Ni kwa kabila? Ni kwa dini? Hizo skolaship zinatolew kwenye shule za dini tu? kama ni hivyo, uwazi wake uko wapi? Hili jukwaa siyo kibanda cha kunywa chai kwamba mliotangulia ni lazima muaminiwe kwa sababu tu mliwahi humu. Ukitoa hoja isiyoeleweka utaulizwa. Ndio maana ya hii forum. Ndugu yangu,jaribu kuwa muwazi zaidi. Kama interest yako ni katika dini sema tu. Hakuna ubaya katika hilo. Ili tu usitufanye sisi wengine ni wajinga kwa kujaribu kupenyeza ishu zako kwa visingizio vingine. Unataka kuniambia hoja yako ni kuwa unataka serikali ifungue ubalozi ili vijana walio huko wabadilishe passpoti zao kirahisi? Mbona wanafunzi wametapakaa nchi nyingi tu ambako aidha hakuna ubalozi au kama upo umbali sana ( kwa mfano marekani kuna watanzania California na ubalozi uko washington n.k)! Wewe umeona Sudan tu!
Fundi hapa sijaona cha kukujibu...kwani umekiri bado mgeni krk Jamvi..si vibaya ukapoteza muda search issue zinazohusu UDINI. Ofcourse wewe ulikuwa na Jibu lako, mie nilishaeleza kwanini nikauliza juu ya Sudan, hamna MTU aliekatazwa kuuliza popote kulingana na HITAJIO lako. Ulivyotafsiri wewe kuwa kwakuwa nimeuliza juu ya Sudan basi kuna issue ya UDINI..naweza sema huo ni ukekengeza..kuwa huru kimawazo.
 
Chuma,
Swali lako hili hapa,
Wana JF naomba kuuliza kwani hatuna ubalozi sudan? wakati sudan wana ubalozi wao hapa TZ kwa miaka zaid ya 10 sasa...

wapi ulipotaja wanafunzi? Sababu uliyoitoa ni kwa nini hatuna ubalozi Sudan wakati wao wanao kwetu? Ndiyo maana wengi wakakuomba ufafanue swali lako. Ungeunganisha nchi nyingine kwenye swali lako la msingi hapo ningekuelewa.

Kuna Mpuuzi namwita samahani kwa kusema tuna uhusiana wa Masomo ya DINI na Sudan. Ni Mvivu kufikiri. Sudan inatoa nafasi nyingi za vijana kusoma Medicine na Engineering free of charge.its like Italy. Suala laweza kuja wanaofaidika ktk dini gani, hili hapa halina nafasi kwani kila sehem lipo kundi linalonufaika kivyake.

Halafu unakiri kuwa kuwa kuna uwezekano kuwa kuna watu wa DINI fulani lakini kama kiranja wa zamani unazuia mjadala kwa kusema kuwa halina nafasi kwa sababu hiyo ni hali halisi. Hivi sivyo ulivyonijibu baadaye kuwa limeishajadiliwa sana kwenye masuala ya elimu. Ni lazima uelewe kuwa ukileta hoja humu hauwezi kutupangia maswali ya kuuliza. Tuna uhuru wa kutaka ufahamisho pale pote ambapo tunaona kuna upungufu. Kuweko kwako kwa muda mrefu not withstanding. Humu wote tuko sawa, wa mwaka 2006 mpaka aliyeingia leo Januari 2008.Kuanzia Junior Member hadi Expert Member. Ndiyo raha yake.

Hiyo ya makosa kwenye website niliishaikiri kwenye post yangu moja ya awali. Sasa Mkuu, kwa hiyo kwa sababu kuna makosa unataka kukazania kuwa Sudan wanawakilishwa kutoka Eritrea au Ethiopia kama ulivyodai awali? Eritrea ambako hatuna ubalozi?

Sijafanya search yeyote kuhusu UDINI. Nilichofanya kwa sababu nilikuwa sijui ubalozi wetu upi unasimamia masuala ya Sudan ni kutafuta balozi zetu nje. suala la udini lina kuja kutokana na post zako mwenyewe. Ni rahisi kuelewa msimamo wako uko wapi linapokuja suala la udini. Hii ni haki yako ya msingi na wala sitathubutu kukuingilia. Umejuaje nina makengeza?
 
Hivi kwa nini balozi aliye Zimbabwe anasimamia Mauritius na siyo aliye South Africa au Maputo? Nadhani logistically ni rahisi kufika kwenye hizo nchi mbili kutoka Port Louis kuliko Harare. Hii hasa ukiangalia uhusiano wetu wa kibiashara na Mauritius. Au na mimi nimechemsha?
 
Fundi kama unasema ni rahisi kujua msimamo wangu wa dini..ki-physics ACTION and REACTION are equal but opposite..kama umeweza kujua msimamo wangu the same mie nimejua msimamo wako.

Sikusema aliemwanzo ni bora au si sawa na aliechelewa...nilichokueleza ni kuwa poteza muda kusoma zaid post za huko nyuma...itakuwa kila mara akija mtu mpya basi afahamishwe...itakuwa kupoteza muda na ndio maana kuna archieve JF.

Infomation ulizoweka za web sikuziamini na ndo maana nikauliza recent issues kwa mtu anaejua. Kusema kitu fulani hujui si kwamba utaonekana mjinga, wengine watafahamisha.


Kuhusu Sudan wewe ndie ulie translate kichwani kwako maelezo yangu. Swali kama uliquote lipo so clear..labda kuna mtu anakupa tafsiri au ndo uwezo wako wa kufikiri sikulaumu.

Mwisho ukipata wasaa wafikishie ujumbe jamaa wa Foreign ku-update hizi infomation zao.Lengo Jamii ya waTZ popote walipo wajue wapi wanaweza pata msaada wao wakati wa Matatizo.
 
Hivi kwa nini balozi aliye Zimbabwe anasimamia Mauritius na siyo aliye South Africa au Maputo? Nadhani logistically ni rahisi kufika kwenye hizo nchi mbili kutoka Port Louis kuliko Harare. Hii hasa ukiangalia uhusiano wetu wa kibiashara na Mauritius. Au na mimi nimechemsha?

kwa nini hasa imekuwa hivi sijui. ila ninachoelewa mimi ni kwamba
inategemea vitu kadhaa na baadhi yake ni hivi
- nchi inayohusika kwam mfano mauritius ikubali ubalozi wetu msumbiji au afrika kusini ndo uwe accredited kwa nchi yao pia
- mauritius imkubali balozi wetu aliyeteuliwa msumbiji au afrika kusini kuiwakilisha tanzania nchini mwao
- geopolitics za nchi husika zipoje
- serikali inaamini ni ubalozi wetu upi utakidhi mahitaji ya mahusiano na nchi husika

aidha wakati mwengine ni serikali inachelewa kwenda na wakati hata kama hayo masuala niliyoyataja hapo juu yamebadilika
 
Mkuu Chuma, mbona unaendeleza ubishi usiokuwa na maana? Bongolander na mimi tulisema anayesimamia shughuli za Sudan ni balozi wetu Kenya. wewe ukatubeza ukasema kutokana na data ulizonazo (za uhakika kuliko hizi za website zetu) anayesimamia shughuli za Sudan ni Eritrea au Ethiopia. Sasa kwa vile unaamini hivyo, mimi siwezi kukulazimisha uamini ya kwangu basi waelekeze hao vijana waende Eritrea au Ethiopia kubadili pasi zao. Haina haja ya kulumbana.

Nashukuru sana kama umejua msimamo wangu maana ndio mjadala utaenda vizuri maana utajua ninakotokea.

Hivi una maana kweli kuwa kila jambo likitokea hapa niende kwanza kwenye archives ili nione wakubwa wangu mlijadili vipi? Are you serious kweli?

Mimi kwa bahati mbaya sina ndugu nje anayehitaji msaada wa ubalozi. Kwa vile mwenzetu kuna vijana unaowafahamu wanahangaika si vibaya kama ukimtumia e-mail Katibu Mkuu Foreign ukimkumbushia haja ya kuwa na ubalozi Sudan ili vijana wasihangaike wanapohitaji kubadili pasi zao na humo humo ukamchomekea hii ya ku-update website yao.
 
By the way mimi naona siku hizi ndio tuna-policy inayoeleweka zaidi kuliko kipindi chote!!! siku hizi balozi zinapimwa kwa kuongeza biashara kati ya nchi husika na Tanzania

Mkuu unaeleweka vizuri kabisa. naungana na wewe kuwa sera ya sasa na ya Mkapa hazina tofauti, labda kweli tofauti ipo kwenye utekelezaji. Ben alikuwa anasisitiza economic diplomacy na alijaribu kuisimamia kwa kiasi fulani na balozi zilijaribu hata kujiendesha kwa kiasi fulani, japo kwa mbinde!
Ukiangalia balozi za wenzetu ambao wanajua kuzitumia utagundua, kuwa biashara ni sehemu tu ya kazi ya ubalozi, na sio kazi pekee ya ubalozi. Tanzania inahitaji mambo mengi sana kutoka nchi za nje, ambayo balozi zetu zinaweza kufanya kazi hizo. kuna teknolojia nyingi sana Tanzania inahitaji kutoka nje(simple technologies of big use on daily lives), sijui kama balozi zetu zina watu wenye jukumu la kuingiza teknolojia nyumbani, sijui kama balozi zetu zinafanya u-spy kwenye issues za kibishara ili kuwe na upper hand, sijui kama balozi zetu zinafanya u-spy wa kuleta teknolojia za kutufanya tusihangaike kuita hata wakandarasi wa kujenga nyumba, au hata kuweza kujenga nyumba za kisasa kuliko haya mabanda tunayoishi kama mimi.
Hata hii tunayosema biashara ukiangalia Kenya wanapiga bao la nguvu kweli Tanzania, lakini tanzania kwa kenya ni kama sifuri kabisa, role ya balozi zetu kuongeza biashara ni kama inalegalega sana, pamoja na kusemwa vizuri kwenye paper. Sasa hivi taifa linafanya biashara kwa kupitia private sector, sijui foreign wanashirikiana vipi na private sector kwenye biashara. Hapa ndio naona weakness fulani ya mifumo ya hapa Bongo kuzi-limit balozi zetu kwa traditional roles, wakati dunia inaendelea kuwa modern, mimi hapa naona tatizo fulani. Membe kama unasoma hii, itakuwa jambo la busara kama haya ukiyafanyia kazi, japo kuanza na nchi za hapa karibu!
 
Back
Top Bottom