BALOZI ZETU NJE YA NCHI: wapi zipo na wapi hazipo?

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
43
Wana JF naomba kuuliza kwani hatuna ubalozi sudan? wakati sudan wana ubalozi wao hapa TZ kwa miaka zaid ya 10 sasa...
 
Mbona Ziko Nchi Nyingi Ambazo Hatuna Balozi Na Wao Wanazo Hapa.

Kwa Nn Uulize Sudani Tu?
 
Sijapata kujiuliza kuhusu hilo, Ila uhusiano na Sudan ni mzuri tu...hasa katika elimu ya dini
 
Kama alivyouliza Mtu wa Pwani, mbona huulizii Nchi za Nordic (isipokuwa Sweden)na nyingine kama hizo ambazo pamoja na kuwa na ubalozi nchini kwetu ni wafadhili wetu wakuu! Kwa nini Sudan tuu?
 
huenda suala ndani yake limejificha suala weka wazi ulichokusudia tujue tuchangie vipi
 
Nadhani ubalozi wetu Ethiopia unahudumia na Sudan vile vile.
 
Ndiyo upo Ubalozi wa Israeli kwa muda mrefu sasa, na pia kuna Ubalozi wa Palestina, Iran, Vaticani, Saudia n.k
 
Mimi siku zote najua Israel wana ofisi ya Ubalozi Nairobi Kenya na siyo Dar.

Ofisi za ubalozi wao pale Dar ziko mitaa gani?
 
nadhani swali lake hasa linabase kwenye kama tuna uhusiano wa Kibalozi na Israeli. Naamini tunao ndio maana Balozi wao ambaye yuko Kenya yuko pia accredited kwa nchi za Tanzania bila ya shaka na Uganda..
 
Je, tukisema Tanzania ina uhusiano wa kibalozi na Israel, lakini Dar hakuna ubalozi wa Israel tutakuwa tumekosea?
 
Je, tukisema Tanzania ina uhusiano wa kibalozi na Israel, lakini Dar hakuna ubalozi wa Israel tutakuwa tumekosea?

Nilivyokuwa najua ni kuwa Ubalozi wa Israel Kenya unahudumia Tanzania,Uganda na Kenya.Labda waamue kufungua ofisi ndogo Tanzania.
 
Baada ya vita ya 1967 Tanzania tulivunja uhusiano wa kibalozi na Israele ili kuwatetea wapalestina.

Naamini kabisa kabla ya hapo Israele walikuwa na ofisi ya Ubalozi nchini Tanzania.

JKT ilianzisha na Israel na hata sasa wanafufua JKT kwa kuwashirikisha.
UDSM na ilijengwa na kuendeshwa kwa muda na Israel Kilimanjaro Hotel pia ilijengwa na Israel.
 
Personally nadhani its in our best interest kuwa na full diplomatic relations with Israel kuliko na nchi kama Yemen kwani faida za kuwa na uhusiano wa Karibu na Israel ni nyingi sana kkusema kweli

Najua wengi wataudhika nayo but so what? ila so far nashangaa huyo Membe mpaka leo hajaenda kuitembelea Israel
 
Baada ya vita ya 1967 Tanzania tulivunja uhusiano wa kibalozi na Israele ili kuwatetea wapalestina.

Naamini kabisa kabla ya hapo Israele walikuwa na ofisi ya Ubalozi nchini Tanzania.

JKT ilianzisha na Israel na hata sasa wanafufua JKT kwa kuwashirikisha.
UDSM na ilijengwa na kuendeshwa kwa muda na Israel Kilimanjaro Hotel pia ilijengwa na Israel.

supposedly na jengo la makao makuu ya usalama wa taifa
 
Madela,
Ile ofisi ya zamani ya ubalozi wa Marekani waliinunua kutoka kwa Waisraeli baada yao kuondoka mwaka 1967. Unaikumbuka ile iliyoripuliwa na mabomu 1998?
 
inakuwaje sasa kikwete ndio apokee credentials zake na wala sio huko huko kenya? au anazunguka nchi zote anazowakilisha?
 
Back
Top Bottom