Balozi wa Tanzania Ujeruman aripoti Poland.

Steven Sambali

JF-Expert Member
Jul 31, 2008
352
170
Juzi ilikuwa furaha kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa kupita, kutembelewa na balozi wetu. Mheshimiwa Mr. Ahmada R. Ngemera alifika mapema na hivyo kuwa na sisi kwa masaa mengi tu. Mara ya mwisho kutembelewa na balozi hapa ilikuwa wakati wa balozi Daraja.

Tunashukuru kwa kukubali kuwa na sisi na kukaa naye "Kinyumbani" na si ki-ofisi. Tunategemea kuwa huu ni mwanzo tu na kama alivyoahidi, atakuja tena hapa ili kujenga daraja ambalo limekosekana kwa muda mrefu. Kusema ukweli nchi kama Wakenya na South Africa, bidhaa zao zimejaa kila kona kuanzia kwenye utalii, mvinyo, vyakula, matunda nk. Kuna siku niliona mahindi mabichi kutoka South Afrika nikaishiwa nguvu. Ila huwezi shangaa hasa ukichukulia ndege zao zinakuja kila siku kutoka Afrika kuja Europe.

Kutoka Poland tunaweza kushirikiana kwenye maeneo mengi sana na hasa ukichukulia kuwa Poland ni nchi ambayo miaka kadhaa iliyopita walikuwa wako chini sana kama sisi. Kimichezo tunaweza kupata faida nyingi sana kama kuleta wachezaji au vijana kusomea kwenye vyuo vya michezo ambavyo hapa wanavyo vingi. Mara ya mwisho kama sikosei, walikuja hapa Simba na huo ulikuwa mwaka 1974 na Simba waliporudi wakacheza mechi na Yanga huko Mwanza ambayo imebaki kwenye historia hadi leo.

Kumekuwa na tabia mbaya kati ya nchi zote mbili. Tanzania huwa wanadharau sana Poland na Poland wanadarau sana Tanzania. Ukweli ni kuwa hiyo ni madhara ya vita baridi ambayo hadi leo tunaendelea kuyalea. Wapolish wakienda Tanzania huwa wanakuja wameshangaa kuwa hawakufahamu kuko hivyo na Watanzania wakifika Poland huwa wanashangaa sana kuwa hawakufahamu kuwa pako hivi. Ukweli kuwa wako European Union, inatosha kabisa kutoa sura kuwa jamaa wako juu sana. Ukichukulia hata makala aliyoleta Mheshimiwa Mo (Mbunge), Poland inatumia umeme kuzidi nchi zote za kusini mwa Afrika ukiacha South Africa. Pia ukija kwenye shule za uchumi, dunia nzima sasa inawatazama wao baada ya THEORY za Prof. Balcelowicz kuonekana zimeshinda za hao wengine wengi wa West. Habari zake zinapatikana hapa: [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Leszek_Balcerowicz[/ame]. Huyu jamaa baada ya Ukomist kufa, aliweka misingi mizuri sana ya uchumi ambayo mwaka jana wakati uchumi umetetereka, Poland hawakupata shida kabisa. Mabenki yalibaki yanatumia akiba ambazo huyu jamaa aliagiza ziwekwe. Pia kwenye kuwekeza, alitaka kila kitu kiwe kinajitegemea, bila kutegemea kampuni mama huko zilikotoka.

Poland wana chuo kimoja cha biashara/uchumi kinaitwa SGH. Hapo ni kisima cha busara na kila serikali ya inayokuja, huwa lazima waende wakachote hapo busara zao. Nafikiri hili lingelifaa sana hata kwetu tuwe tunalitumia. Sema tu wenzetu pamoja na kuwa ni Waalimu, bado huwa wanaendelea na siasa na bado wanarudi kufundisha.

Inabidi niseme karibuni Poland mtakaotaka kutangaza biashara zenu hapa. Kwa vijana watakaotaka kuja kusoma, lazima niseme kuwa kuna vyuo vizuri tu na gharama zao hazijawa juu sana. Kuna vyuo vya uganga, ufundi, michezo, University za kawaida. Pia kuna mji unaitwa LODZ (soma WUJI) ambao kuna chuo kizuri sana kwa ajili ya Film na Acting. Mmoja ya watu waliosoma hapo ni Marehemu Mzee Gamba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Kenya Film Corporation na alikuwa kama co-Director wa film ya RISE AND FALL OF IDD AMIN. Pia wakali wengine ni kama Director Wajda na Roman Polanski.

Vijana mnaweza kupata habari zaidi kwenye mitandao inayohusu Waafrika wanaoishi hapa Poland:

http://afrix.org/home.php (hii ni kama Facebook).

http://afryka.org/ (Sorry, Polish Only).

http://afryka.org/fundacja/index-en.html (Foundation yetu).

Mtu akihitaji msaada, basi tuwasiline kwa email: sambali@afryka.org

Tutajitahidi kusaidia kwa kiasi tutakachoweza ili kubadili maisha ya Watanzania. Inawezekana kwa tukaweza kubadili wawili au watatu. Wachezaji mpira pia mnakaribishwa ingawa Poland wanaweza kuwa hawalipi vizuri ila kama unakipaji, inaweza kuwa njia ya kuanzia. Geremy wa Cameroon alipita hapa. Kalu Uche wa Nigeria pia amecheza sana ligi za Poland.

Picha za balozi wetu akiwa Warsaw, hapo jana:
http://m.prezydent.pl/aktualnosci/n...asadorow-zlozylo-listy-uwierzytelniajace.html

Hapa juu balozi wetu akiwa na Rais wa Poland, President Lech Kaczyński na picha inayofuata akiwa tayari kwenye kukagua Gwaride.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
.
 
Juzi ilikuwa furaha kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa kupita, kutembelewa na balozi wetu. Mheshimiwa Mr. Ahmada R. Ngemera alifika mapema na hivyo kuwa na sisi kwa masaa mengi tu. Mara ya mwisho kutembelewa na balozi hapa ilikuwa wakati wa balozi Daraja.

Tunashukuru kwa kukubali kuwa na sisi na kukaa naye "Kinyumbani" na si ki-ofisi. Tunategemea kuwa huu ni mwanzo tu na kama alivyoahidi, atakuja tena hapa ili kujenga daraja ambalo limekosekana kwa muda mrefu. Kusema ukweli nchi kama Wakenya na South Africa, bidhaa zao zimejaa kila kona kuanzia kwenye utalii, mvinyo, vyakula, matunda nk. Kuna siku niliona mahindi mabichi kutoka South Afrika nikaishiwa nguvu. Ila huwezi shangaa hasa ukichukulia ndege zao zinakuja kila siku kutoka Afrika kuja Europe.

Kutoka Poland tunaweza kushirikiana kwenye maeneo mengi sana na hasa ukichukulia kuwa Poland ni nchi ambayo miaka kadhaa iliyopita walikuwa wako chini sana kama sisi. Kimichezo tunaweza kupata faida nyingi sana kama kuleta wachezaji au vijana kusomea kwenye vyuo vya michezo ambavyo hapa wanavyo vingi. Mara ya mwisho kama sikosei, walikuja hapa Simba na huo ulikuwa mwaka 1974 na Simba waliporudi wakacheza mechi na Yanga huko Mwanza ambayo imebaki kwenye historia hadi leo.

Kumekuwa na tabia mbaya kati ya nchi zote mbili. Tanzania huwa wanadharau sana Poland na Poland wanadarau sana Tanzania. Ukweli ni kuwa hiyo ni madhara ya vita baridi ambayo hadi leo tunaendelea kuyalea. Wapolish wakienda Tanzania huwa wanakuja wameshangaa kuwa hawakufahamu kuko hivyo na Watanzania wakifika Poland huwa wanashangaa sana kuwa hawakufahamu kuwa pako hivi. Ukweli kuwa wako European Union, inatosha kabisa kutoa sura kuwa jamaa wako juu sana. Ukichukulia hata makala aliyoleta Mheshimiwa Mo (Mbunge), Poland inatumia umeme kuzidi nchi zote za kusini mwa Afrika ukiacha South Africa. Pia ukija kwenye shule za uchumi, dunia nzima sasa inawatazama wao baada ya THEORY za Prof. Balcelowicz kuonekana zimeshinda za hao wengine wengi wa West. Habari zake zinapatikana hapa: http://en.wikipedia.org/wiki/Leszek_Balcerowicz. Huyu jamaa baada ya Ukomist kufa, aliweka misingi mizuri sana ya uchumi ambayo mwaka jana wakati uchumi umetetereka, Poland hawakupata shida kabisa. Mabenki yalibaki yanatumia akiba ambazo huyu jamaa aliagiza ziwekwe. Pia kwenye kuwekeza, alitaka kila kitu kiwe kinajitegemea, bila kutegemea kampuni mama huko zilikotoka.

Poland wana chuo kimoja cha biashara/uchumi kinaitwa SGH. Hapo ni kisima cha busara na kila serikali ya inayokuja, huwa lazima waende wakachote hapo busara zao. Nafikiri hili lingelifaa sana hata kwetu tuwe tunalitumia. Sema tu wenzetu pamoja na kuwa ni Waalimu, bado huwa wanaendelea na siasa na bado wanarudi kufundisha.

Inabidi niseme karibuni Poland mtakaotaka kutangaza biashara zenu hapa. Kwa vijana watakaotaka kuja kusoma, lazima niseme kuwa kuna vyuo vizuri tu na gharama zao hazijawa juu sana. Kuna vyuo vya uganga, ufundi, michezo, University za kawaida. Pia kuna mji unaitwa LODZ (soma WUJI) ambao kuna chuo kizuri sana kwa ajili ya Film na Acting. Mmoja ya watu waliosoma hapo ni Marehemu Mzee Gamba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Kenya Film Corporation na alikuwa kama co-Director wa film ya RISE AND FALL OF IDD AMIN. Pia wakali wengine ni kama Director Wajda na Roman Polanski.

Vijana mnaweza kupata habari zaidi kwenye mitandao inayohusu Waafrika wanaoishi hapa Poland:

http://afrix.org/home.php (hii ni kama Facebook).

http://afryka.org/ (Sorry, Polish Only).

http://afryka.org/fundacja/index-en.html (Foundation yetu).

Mtu akihitaji msaada, basi tuwasiline kwa email: sambali@afryka.org

Tutajitahidi kusaidia kwa kiasi tutakachoweza ili kubadili maisha ya Watanzania. Inawezekana kwa tukaweza kubadili wawili au watatu. Wachezaji mpira pia mnakaribishwa ingawa Poland wanaweza kuwa hawalipi vizuri ila kama unakipaji, inaweza kuwa njia ya kuanzia. Geremy wa Cameroon alipita hapa. Kalu Uche wa Nigeria pia amecheza sana ligi za Poland.

Picha za balozi wetu akiwa Warsaw, hapo jana:
http://m.prezydent.pl/aktualnosci/n...asadorow-zlozylo-listy-uwierzytelniajace.html

Hapa juu balozi wetu akiwa na Rais wa Poland, President Lech Kaczyński na picha inayofuata akiwa tayari kwenye kukagua Gwaride.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Hongereni sana Mr Steve!.
 
Hata mimi nilikuwa sina mengi ninayofahamu kuhusu Poland. Asante sana kwa kunijuza.

Bujibuji,

Ntajitahidi mara mojamoja niwe naleta habari za huku na kuwagawia Watanzania kama ambavyo tumekuwa tukijitahidi kuibadili sura ya Afrika kwenye macho ya Wapolish. Juzi juzi tu nimeshiriki kuandika kitabu ambacho kimependwa sana na Umoja wa Waalimu wa Poland. Kitabu hiki ni kwa ajili ya Waalimu wa shule ya msingi na kimeandikwa ili kuwajulisha watoto wadogo wa Kipolish jinsi watoto wenzao wa Afrika walivyo. Wasiwe na ile picha moja tu inayoonyeshwa kwenye TV na magazeti yao na hizi NGO tofauti wakitafuta pesa za misaada, kuuza habari kwa waandishi wa habari nk.

Cha ajabu utakuta kwamba, nchi kama UK, German, USA, Japan nk wamewekeza sana hapa Poland. Pia watu haohao wanauza au kuwekeza biashara zao Tanzania. Ila watakuja Tanzania na kusema Poland hamna kitu na watakuja hapa na kusema Tanzania hamna kitu. Wajinga siye tunabaki kuamini tu.

Kinaniuma kitu kimoja. Utakuta matangazo kibao ya Kitalii ya Wakenya. Utasikia mtu anasema nilikuwa Tanzania, ukimuuliza ulinunua Tour ya Kenya, utasikia ndiyo. Yes, kuna matangazo ya kitalii ya Tanzania ila kwa sababu ni machache basi gharama zinakuwa kubwa sana.

Itakuwa vema kama nitaenda mbali zaidi na kusema kuwa si Poland tu. Nchi kama Belarus, kuna matrekta mazuri sana ambayo hadi nchi kama German, USA, UK yanauzwa na bei ni cheap sana. Kuna nchi kama Czeck tunaweza kujifunza jinsi ya kufanya biashara ya utalii. Mji wao mkuu una watalii zaidi ya wenyeji wa pale. Kuna nchi kama Hungury na Ikarus zao, hawa jamaa wako mbali sana. Kuna Rumunia, Bulgaria (kocha wetu Mziray alisomea hapo), Ukraine na Russia kwa ujumla, hawa wako juu sana kulingana na sisi na hivyo ni rahisi kujifunza kutoka kwao kwani hatutofautiani sana.

JUMAPILI (tarehe 07/02), kwenye ukumbi uitwayo Warsaw SALA KONGRESOWA ambapo dada yetu Wema Sepetu aligaragazwa kwenye mashindano ya urembo duniani, kutafanyika ugawaji makundi kwenye mashindano ya UEFA 2012 ambayo yatafanyika Poland na Ukraine. Karibuni sana muone/tuone jinsi wenzetu wanavyojiandaa. Labda na sisi tunaweza kuandaa mashindano ya Afrika maana hata nchi kama Mali na umasikini wao, waliweza kuandaa. Uzuri wa haya mashindano siku zote yanaacha nchi imebadilika sana kwani inabidi kufanya shughuli nyingi na kuacha mizaha ukiwa kazini kwani vinginevyo utashindwa kwenda na muda.

http://www.jeanmicheljarre.pl/img/news/kongresowa_big.jpg

http://www.arbiter.pl/files/g/2_1049717391_IMG_4013_.jpg
 
Back
Top Bottom