Balozi wa REDDS 2008 arejesha Taji na Zawadi

mi Nafikiri Hakuna Wa Kualaumiwa
maana Mama Na Baba Walkuwa Kwenye Shuguri,,na Hao Wachungaji Wakati
Ananyakua Taji Kabla Ya Hili
Walijua Atalaumiwa Nani Jamani????????????

Red's Nanyie Angalien Vizuri Uko Kwenu Labda Kuna Mtu Ana Gundu Au Kuna Viongzi Wenu Wachafu Wanawachafua Watoto Wa Watu Ndio Maana Wanakimbia!!1just For Info Nasikia Kuna Kijana Anaitwa George Kavishe
Anaumwa Huuu Ugonjwa Wetu Na Amekuwa Akitembea Na Warembo Tofauti Sana Ila Ninachosema Ukimwi Hautaisha Kwa Atyle Hii
Ona

Kila Miss

Lundega Yuleyule

Kavishe Naeeeeeeeeee Yupo

Predeshe 3456 Nae Yupo

Jack Pemba Yupo Ulizeni Bagamoyo Walivyofanyiwa Fujo Ya Pesa Hao!!!!

Wito Ukiona Ndugu Yako Anaingia Huko Mkane Kabisa Na Ukoowww

Ona Maneno Haya....!
 
Yeye kama dini yake hairuhusu kushiriki mashindano yanayodhaminiwa na pombe kwa nini alishiriki? pili hayo mashindano yameanzia kwenye vitongoji na akashiriki toka huko so alikuwa hajui kuwa dini yake hairuhusu? eti kanisa lao ni la kilokole na baba yake ndo mchungaji wa hilo kanisa, kwa nini huyo baba yake alimruhusu binti yake aende kushiriki hayo mashindano?
 
Nauliza hivi yeye Angela Luballa wakati wa mashindano hakuvaa bikini? au safari hii haikuwepo? kama alivaa kwake si dhambi kuacha sehemu kubwa ya mwili wake nje? Na je kama angeshinda Miss Tanzania angerudisha zawadi? au wakati anashiriki hakujua kama kuna miss REDDS?

Kuna tatizo hapa!!
 
naheshimu uamuzi wake lakiini, wakati anakwenda kugombea hakujua kwamba redds ni pombe na sio juice? Mwanza si alikwenda? au redds alifikiri ni kinywaji cha coca cola? kasoma wapi eti huyu dada, lafudhi yake imeniacha njia panda, kama hataki nataka kusema vile? all the best sis, next time fikiria kwanza umezibia wenzako sasa , wale happy go lucky

Inawezekana kabisa binti alijua kuwa redds inahusiana na pombe, lakini hiyo haimzuii kubadili uamuzi wake kama alivyofanya. Ni vema ujue kuwa wakati mwingine mtu anatambua makosa ya uamuzi wa awali na kuamua kujirekebisha. Wakati mwingine mtu analazimika kubadili uamuzi baada ya kupata ushauri wa watu wengine wa karibu kama wazazi, ndugu, au marafiki. Na huenda hii ndiyo hali iliyojitokeza kwa binti huyu.

Mimi binafsi nampongeza binti kwa ujasiri alioufanya wa kuamua kurudisha zawadi ili kulinda imani yake. Na ninamtakia baraka na mafanikio katika maisha yake hata bila hizo zawadi (gari na fedha alizokuwa amepewa kwa ushindi wake). Nina imani kuwa kama kweli amefanya uamuzi wake kwa misingi ya imani yake, Mungu huyo anayemwamini atamfanikisha katika maisha yake kwa njia nyingine.

Binti ubarikiwe sana na Mungu azidi kukuongoza na kukupigania maishani mwako ili daima uishi maisha ya ushindi.
 
kujitoa kwake kunachangiwa na maswali alokua naulizwa babake ambaye ni kiongozi kanisani kwani waumini walitaka kujua inakuaje mtotot wa mlokole ashiriki umiss na kutangaza biani maswali mengi sana (according 2 vyombo vya habari nilivopitia last wk)mana msee huyu wa kanisa akadai mwanae alionesha ana kipaji cha umiss toka alipokua 4yrs thats y hawakuona ubaya kumruhusu(sasa hapa dini nayo sijui waliikumbuka inasemaje), ila walakini wa waumini ulipozidi hapo msee na familia ikabidi imshauri binti avue taji

si mnaelewa tena dini biashara na waumini a.k.a wanunuzi wakishaanza kua na walakini na bidhaa(kiongozi+kanisa lao)haitauzika so watu watakimbia kanisa ...tusikose wanunuzi a.k.a waumini ngoja mtt avue taji..(utani tu lakini)
 
Huyu mbona kachemka tena sana tu....Kama alikuwa anajua hilo kwa nini asingejiengua mapema?Je angeshinda umiss TZ angevua?sawa kasema tatizo ni kilaji kwani dhehebu gani la kikristo linalo ruhusu mashindano haya ya kimiss??si yote yanapinga kuwa ni kinyume ya maadili mtu kupita amevaa kichupi nakuonyesha maungo yake dini zote haziruhusu.Huyu binti anajitafutia umaarufu kwa kuzitema zawadi hizo.
 
Mimi nadhani kama itikadi yake ilikuwa haimruhusu asingeshiriki katika hayo mashindano ya kumtafuta mrembo wa miss vodacom 2008. Hapa ni kutaka kuudanganya umati wa watanzania na kuwafanya watu wajinga anachotakiwa kufanya ni kuomba radhi kwanza kwa waandaaji na baadae wadanganyika woote pamoja na kamati ya Lundenga. Mimi ninachoona hapa huyu binti ameact under influence of her parents. Ya Kaisari mpe Kaisari.....................Usimix imani na mambo fulani.
 
Kwa tabia za wasichana wetu wa siku hizi kurubuniwa na vilaki huyu kurudisha 2.5m na kusamehe 3m ya mshahara wa mwaka tumsifu tena sana.Mimi wiki hiyo 1 nachukulia ni muda aliokua anatafakari afanyeje.Mi nimeshaoa lakini huyu ni binti wa kumuongeza kwenye ukoo wowote,hongera angeja na kama umejua kwakua mameneja wa Tbl wanalalamikiwa sana kwa kuwarubuni warembo

Huyu mtoto, mimi namfahamu, baba yake ni Mchungaji Deo Lubala, ni askofu wa kanisa la world alive kule sinza. waliishi sana America, hapa Tanzania hata miaka minne hajafikisha, wamerudi juzi tu hapa, amekulia kule America na amesoma kule America.

Kanisa lile ni kanisa la kilokole, hata kama aliingia kule, najua aliingia kwa nguvu zake tu, wazazi wake wanaweza wakawa walimshauri aachane na icho kitu. mimi nampongeza sana kwa kuacha kuendelea na hilo shindano la kishetani, la kimapepo. Mungu anasema, tusiuangalie uzuri wa nje, tuangalie uzuri wa ndani ya mioyo yetu maana huko ndiko zitokazo chamchem chafu au safi. kwa nje sisi wote tu wazuri na hatuna hata sababu au sauti ya kumkosoa Mungu kwamba alimuumba huyu mzuri sana na huyu sio mzuri sana, because kile mtu yuko kama alivyo kwa Neema ya Mungu, kwa mapenzi ya Mungu, na hata kama kuna vitu vilivyoathiri akawa hivyo alivyo, Mungu bado anamuona ni mzuri tu. hakina sababu ya mtu kushindania uzuri, ati uzuri, kwahiyo wengine wabaya eeee, ni uchafu wa shetani kabisa. ndio maana network yake ni kwenye umiss, kutangaza mipombe na kusambaza mapepo ya zinaaa ya mahaba. asante sana lubala kwa busara yako, sasa umeutangazia ulimwengu kuwa, ulikuwa umepotea, na sasa umerudi kwenye njia, twende zetu mbinguni mwana.
 
Tukio hili ni changamoto kwa dini zetu hasa kwa wakati huu wa mabadiliko.
 
Wazee, ukiona ulipotea kwenda kwa shetani, unatakiwa kukimbia bila hata kuomba ruhusa, yaani huwezi kusema ooooh shetani unajua nikijitoa sasahivi nitakuwa nimevuruga biashara au shuguli yako etc, ni kulala mbele na kuondoka, kuwapa chao na wewe ubakie mtakatifu takataaaaa. wewe unaesema dini ni biashara, huamjui Mungu, usisubirie upate matatizo, ukonde utake kufa ndo uombe msaada kwa haohao unaosema wanafanya biashara wakuombeee. pole sana.

angela alichofanya ni cha busara, hatuna urafiki na shetani, huo wote uliuwa mpango wa shetani kuchafua picha ya kanisa la Mungu, kwamba hata mtoto wa askofu anashiriki mashindano ya kishetani. shetani ameshindwa kwa Jina la Yesu. achukue milioni mbili zake na angela anaenda zake na Yesu. Amina.
 
mi nafikiri hakuna wa kualaumiwa
maana mama na baba walkuwa kwenye shuguri,,na hao wachungaji wakati
ananyakua taji kabla ya hili walijua atalaumiwa nani jamani????????????

RED'S nanyie angalien vizuri uko kwenu labda kuna mtu ana gundu au kuna viongzi wenu wachafu wanawachafua watoto wa watu ndio maana wanakimbia!!1just for info nasikia kuna kijana anaitwa GEORGE KAVISHE
ANAUMWA HUUU UGONJWA WETU NA AMEKUWA AKITEMBEA NA WAREMBO TOFAUTI SANA ILA NINACHOSEMA UKIMWI HAUTAISHA KWA ATYLE HII
ONA

KILA MISS

LUNDEGA YULEYULE

KAVISHE NAEEEEEEEEEE YUPO

PREDESHE 3456 NAE YUPO

JACK PEMBA YUPO ULIZENI BAGAMOYO WALIVYOFANYIWA FUJO YA PESA HAO!!!!

WITO UKIONA NDUGU YAKO ANAINGIA HUKO MKANE KABISA NA UKOOwwW

Hawa brand managers wana matatizo binti kajiokoa mapema
 
Mambo matata na utatanishi mkubwa... Sikujua kama kuna makanisa yanakubaliana na mchakato mzima wa mashindano ya Ulimbwende lakini yanagomea suala zima la kuhusiana na Pombe...

Kweli kuna utata katika dini zetu.!

Ndg,

Tofautisha baina ya dini na 'muumin', hiyo itakuwezesha kuwa mpembuzi makini.

Wasalam.
 
Kwa tabia za wasichana wetu wa siku hizi kurubuniwa na vilaki huyu kurudisha 2.5m na kusamehe 3m ya mshahara wa mwaka tumsifu tena sana.Mimi wiki hiyo 1 nachukulia ni muda aliokua anatafakari afanyeje.Mi nimeshaoa lakini huyu ni binti wa kumuongeza kwenye ukoo wowote,hongera angeja na kama umejua kwakua mameneja wa Tbl wanalalamikiwa sana kwa kuwarubuni warembo
....
...Khoryere, alichofanya binti si sahihi na ni uvurugaji wa tukio zima la kumpata huyo mrembo wa Redd's na wala msitake kumsifu kuwa eti amefanya jambo la ujasiri si kweli kumbuka imeripotiwa kuwa aliamua kurudisha taji na zawadi baada ya baba yake ambaye ni mchungaji kubanwa huko kanisani kwake kwa nini binti amekubali kuwa mrembo wa redd's.

Nina imani kama baba wa huyo binti asingewekwa kiti moto huko kanisani asingerudisha taji na zawadi ukizingatia kuwa kinywaji cha redd's kinafahamika kwa watu wengi na kwa muda mrefu sitaki kuamini kuwa walikuwa yeye na wazazi wake kuwa hawakuelewa kuwa redd's ni pombe. Nadhani ni fundisho kwa Lundenga na kamati yake kuwa makini na hao mabinti wanaowachukua kushiriki hayo mashindano kwa vigezo vya imani na idhini ya wazazi kuliko kuwapotezea watu muda na kuharibu hata sifa ya mashindao yenyewe ni uswahili tu hapo hakuna cha kumpongeza ikibidi Lino na Redd's wamshitaki tu huyo mrembo kwa alichofanya ili iwe fundisho kwa wengine!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
dada huyu alichemsha saaana.
mimi siamini kwamba kuna dini inaruhusu kabisa mtu aende katika mashindano ya urembo. Kumbuka kuna kuvaa vile vinguo vya kuogelea (hata kama hapa TZ wamekataa lakini huko ktk mashindano ya dunia bado vipo). Mashindano yenyewe yanadhaminiwa na kilevi - Redds . Alikuwa na miezi kadhaa ya kutafakari kabla ya kushiriki !

ameamua kushiriki, ameshinda, ameshangilia, amevikwa taji, kupewa zawadi, nk. then all of a sudden eti yeye ni mlokole ! ulokole gani huu. Kwa yesu unatakiwa uwe "moto" au "baridi" na sio uvuguvugu. ashindwe na alegee. anyway tunamsamehe kwa vile amegundua kosa na kumrudia muumba wake.
 
....
...Khoryere, alichofanya binti si sahihi na ni uvurugaji wa tukio zima la kumpata huyo mrembo wa Redd's na wala msitake kumsifu kuwa eti amefanya jambo la ujasiri si kweli kumbuka imeripotiwa kuwa aliamua kurudisha taji na zawadi baada ya baba yake ambaye ni mchungaji kubanwa huko kanisani kwake kwa nini binti amekubali kuwa mrembo wa redd's.

Nina imani kama baba wa huyo binti asingewekwa kiti moto huko kanisani asingerudisha taji na zawadi ukizingatia kuwa kinywaji cha redd's kinafahamika kwa watu wengi na kwa muda mrefu sitaki kuamini kuwa walikuwa yeye na wazazi wake kuwa hawakuelewa kuwa redd's ni pombe. Nadhani ni fundisho kwa Lundenga na kamati yake kuwa makini na hao mabinti wanaowachukua kushiriki hayo mashindano kwa vigezo vya imani na idhini ya wazazi kuliko kuwapotezea watu muda na kuharibu hata sifa ya mashindao yenyewe ni uswahili tu hapo hakuna cha kumpongeza ikibidi Lino na Redd's wamshitaki tu huyo mrembo kwa alichofanya ili iwe fundisho kwa wengine!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kipanga: dada huyu ameingia katika mashindano haya kwa hiari na amejitoa kwa hiari. Hakuna kilichoharibika, maana hata pesa za ushindi amerudisha na taji. Swali linakuja, je kulikuwa na mkataba alioingia na Redds na Lino? Je mkataba ulikuwa unasemaje kuhusu kurudisha taji? Kama hakuna mkataba unaombana kwamba hawezi kurudisha taji, basi inabidi Redds wakubali matokeo. Na kwa kweli bado nampongeza dada kwa msimamo wake, whether ali-quit kutokana na external forces or individual decision, she has the right to change her mind, just like waandaji wana haki ya kumvua mrembo wao taji.
 
Susuviri,
Sikubaliani na wewe hata kidogo pamoja na kuwa binti aliamua kwa hiari yake kushiriki kwa hatua liyofikia sikubalia kuwa ana hiari ya kujitoa eti kwa vile tu anarudisha zawadi na taji. Kumbuka waandaji wanaweka vigezo katika kumpata huyo mrembo wa redd's anapojitoa mtu kwa mtazamo wangu itapelekea waandaji kurudi nyuma tena kuona nani achukue hiyo nafasi najua inawezekana kupata replacement kwani hata huyo mrembo angeweza kufa pia achilia mbali kujitoa lazima redd's wangetakiwa kumpata mrembo mwingine. Lakini kubwa ni mazingira ya tukio lenyewe alipotangazwa kuwa ameshinda kuwa membo wa redd's alitakiwa hapo hapo awaambie waandaji mapema kuwa jamani mi
dini yangu hainiruhusu kutangaza kilevi angekuwa amefanya jambo la maana sana that's means hata hao waandaji wangekuwa na nafasi ya kumtafuta mtu mwingine wa kuchukua hiyo nafasi. Lakini alitangazwa ameshinda, si ajabu akampigia simu na baba na mama yake, amepokea zawadi na wazazi walishuhudia then akurupuke kuwa narudisha taji na zawadi kuwa dini hairuhusu Oooooh!! come on then unamsifu???

Inawezekana kweli huendaLino au redd's hawana mikataba na warembo katika kushiriki katika hayo mashindano lakini kama nilivyosema awali kuwa Lino na redd's watakuwa wamejifunza kitu na huenda next time wakafikiria mechanisms za kuwawajibisha warembo watakaokwenda kinyume.....Mzee kuna muda, resources na energy watu wamepoteza kufikai hatua ya kumpata mshindi sasa kirahisi tu unawarudisha watu to 0 halafu unamsifia?? Sorry mkuu nina mashaka na busara na hekima zako!!!!
 
Naomba na mimi kuchangia kidogo.
huyu binti namsifu kwa ujasiri japo umechelewa, na alichokuwa anatamani kakipata, yani kujulikana kama ni mrembo.
Kama kweli alikuwa msikivu wa familia yake yani wazazi, lazima wangemshauri asishiriki, ila kwa ukaidi alishiriki, na specifically alipanda jukwaani pale mwanza, kwaajili ya kutafuta miss redds pekee, walizunguka jukwaani mara kadhaa, na yeye akiwamo, je alijua kuwa redds ni pombe? je kama alikuwa hajui, ina maana ni mjinga sana, au kama alijua ni pombe alitakiwa asipande jukwaani siku ile pale mwanza.
Baada ya hapo kwa kuwa haya mashindano ni ya mikataba(?) basi kwa kubatilisha mkataba, inabidi redds wamlipishe faini kufidia gharama zao za usumbufu.
Fundisho wazazi wawe karibu na watoto wao, kuwashauri, kama hawasikii, basi dunia itawafunza, waumini hawana haja ya kumhukumu mchungaji kwa ajili ya mtoto aliezidi miaka 18, wanamtesa na kumuonea tu.
Wengine wameshindikana, wanahitaji sala na kufunga tu.
japo sikubaliani na mashindano ua urembo, lakini huyu apigwe faini.
 
Ni wazi kuwa huyu bint amepata shinikizo arudishe hilo taji.

Ni wazi kabisa Angela anapenda fani ya urembo na hata wazazi wake walikuwa tayari kumsapoti.

ikumbukwe kuwa wazazi walikuwepo siku ile ambayo Tanzania Breweries Ltd. kupitia kinywaji chake cha Redds walipoandaa hafla ya kumpongeza Angela. Sikuwepo, lakini nina amini kuwa kulikuwa na bia na pombe nyinginezo. kwa maana hiyo ufahamu ulikuwepo kwa wao wote kwa maana ya yeye angela na wazazi wake kuwa TBL siyo kampuni ya soda na vilivyokuwa vinatumiwa siku hiyo siyo juice wala soda, ni wazi limekuwepo shinikizo from third party.

Sijui ni kwa kiasi gani huyu bint atakuwa ameathirika kisaikolojia.
 
Susuviri,
Sikubaliani na wewe hata kidogo pamoja na kuwa binti aliamua kwa hiari yake kushiriki kwa hatua liyofikia sikubalia kuwa ana hiari ya kujitoa eti kwa vile tu anarudisha zawadi na taji. Kumbuka waandaji wanaweka vigezo katika kumpata huyo mrembo wa redd's anapojitoa mtu kwa mtazamo wangu itapelekea waandaji kurudi nyuma tena kuona nani achukue hiyo nafasi najua inawezekana kupata replacement kwani hata huyo mrembo angeweza kufa pia achilia mbali kujitoa lazima redd's wangetakiwa kumpata mrembo mwingine. Lakini kubwa ni mazingira ya tukio lenyewe alipotangazwa kuwa ameshinda kuwa membo wa redd's alitakiwa hapo hapo awaambie waandaji mapema kuwa jamani mi
dini yangu hainiruhusu kutangaza kilevi angekuwa amefanya jambo la maana sana that's means hata hao waandaji wangekuwa na nafasi ya kumtafuta mtu mwingine wa kuchukua hiyo nafasi. Lakini alitangazwa ameshinda, si ajabu akampigia simu na baba na mama yake, amepokea zawadi na wazazi walishuhudia then akurupuke kuwa narudisha taji na zawadi kuwa dini hairuhusu Oooooh!! come on then unamsifu???

Inawezekana kweli huendaLino au redd's hawana mikataba na warembo katika kushiriki katika hayo mashindano lakini kama nilivyosema awali kuwa Lino na redd's watakuwa wamejifunza kitu na huenda next time wakafikiria mechanisms za kuwawajibisha warembo watakaokwenda kinyume.....Mzee kuna muda, resources na energy watu wamepoteza kufikai hatua ya kumpata mshindi sasa kirahisi tu unawarudisha watu to 0 halafu unamsifia?? Sorry mkuu nina mashaka na busara na hekima zako!!!!

Kipanga, I cannot invest so much emotion in beauty pageants, lakini naona ishu hii imekugusa sana, hivyo naomba bila jazba na matusi nikujibu kiutu uzima Kabla ya yote naomba nitofautishe mada hapa. Kuna suala la mrembo binafsi na imani yake ya dini. Kuna suala la investment kwa upande wa waandaji. Kuna suala la mikataba.
Sasa naomba tuanze na imani ya binti ambayo ni eneo nililotumia kumsifu binti huyu. Imani yake binti ni private matter. Anaweza akawa ameshindana na kutokana na factors mbalimbali akaona kwamba alichokifanya ni kinyume na imani yake. Hivyo akajitokeza hadharani na kusema hataki taji na kulirudisha. Mi namsifu kwa sababu ni kheri afanye hivyo kuliko kuanza kuwapiga chenga waandaji, kutafuta vijisababu vya kutoshiriki au kuleta vituko na kuzima simu eti hapatikani kwenye shughuli mbalimbali. [Nakumbuka Nancy Sumari aliwafanyia hivyo waandaji mpaka wakaandikana kwenye magazeti, Mrembo huyu wa mwaka jana, Radhia naye hajafanya shughuli zozote za kijamii] Like this it is straight forward na Angela anampatia nafasi mrembo mwingine ambaye atafanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu. Ndiyo maana nimemsifia dada, amekuwa mwazi na hajapindisha.
Investment kwa upande wa waandaji: Waandaji waliandaa hafla mbalimbali, lakni ni hafla moja tu ambayo iliandaliwa specific for Angela, ni ile iliyofanyika wiki iliyopita ya kupokea taji kutoka yule mshindi wa 2007. Gharama zingine za fainali ya Miss Tanzania walipomtangaza, fashion show ya Redds iliyofanyika Mwanza, haziwezi kuhesabika maana shughuli ingefanyika whether Angela angeshiriki au la. Kama wana mpango wa kumdai compensation, nadhani this is the only area wanaweza kumdai (kukabidhi taji). Zaidi ya hapo, alikuwa ni mmoja ya washiriki. So hakuna investment kubwa iliyofanyika kwa upande wa Redds.
Mikataba: Kama Redds na Lino wanafanya shughuli hizi bila mikataba basi nitawashangaa sana. Redds huu ni mwaka wao wa 3 au 4 wanatoa taji, Lino ni miaka 10 na kitu wanaandaa Miss Tz na hawajajifunza kusaini mikataba na warembo? Kwa kweli hii si fundisho tosha. Ndiyo maana kumbe wanashindwa hata kumvua taji washindi wao wanaoboronga? Maana hawana legal premise ya kufanya hivyo!? Sasa kama ni kweli hawana mikataba hii fundisho haijawagharimu vya kutosha. Maana wana bahati dada huyu alikuwa mstaarabu.
 
Back
Top Bottom