Balozi wa nyumba kumi:Ana mamlaka gani kisheria leo hii,ana kazi gani kwa wananchi?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Hakuna cheo nisichokitambua na ambacho kina wababaisha watu wengi huku mtaani kwetu kama hiki cha balozi.Wengi hata wale waliokwenda shule bado wana endekeza enzi za chama kushika hatamu ambapo balozi wa nyumba kumi alikuwa na nguvu kubwa kwa watu japo sina uhakika kama ni cheo kilichokuwa kipo kisheria au la.Ninachokifahamu mimi ni kuwa huyu si kiongozi wa serikali.Mwenyekiti wa serikali za mitaa ndiye kiongozi mkuu katika mtaa husika.Lakini cha ajabu yupo huyu aitwae balozi naye anajionesha kama ana tambulika.

Binafsi kwangu nimekuwa nikiwakatalia kupokea amri zao kwa hoja hii kuwa yeye si kiongozi wa serikali.
Baada ya mauaji ya ovyo kutokea hapa Songea mkuu wa wilaya alipita na kuwaeleza wananchi kile kilichotokea.Katika mikutano yake yote hapa mjini alikuwa anakumbana na maswali mengi ambayo alikuwa hawezi kuyatolea ufafanuzi zaidi ya kuleta ubabe.Hivi sasa ametoa amri ya kulinda sungusung mitaani.Sasa zoezi hili limekuwa likiendeshwa na hawa jamaa wa kujiita mabalozi wa nyumba kumi kumi.Jambo hili kwenye mkutano mmojawapo Sabaya Mkuu wa wilaya alikataliwa kuwatumia hawa watu badala yake tulimwambia hiyo ni kazi ya serikali ya mitaa.Balozi hatambuliki hivyo hataweza kujibishwa pindi mambo yatakapokuwa ymeharibika.Lakini inaonekana ameendelea na ubabe huo wa kuwatumia.

Juzi mimi niliwatimua wajumbe walotumwa na balozi nikawaambia hilo ni jukumu la Mwenyekiti wa serikali za mitaa.Wakarudisha jibu kuwa nimekaidi amri ya serikali.Nikaletewa barua ya kuitwa ofisini.Huko akaitwa na huyo balozi,nikamwambia Mwenyekiti kuwa huyu simtambui na wala sitatii amri hiyo akitaka atangulie mahakamani.Nikamwambia kama ni kweli ana tawala kisheria basi barua ilitakiwa iandikwe na balozi huyu ya kuniita mimi lakini badala yake umeandika wewe.
Naandika hili ili kuwaeleza na wengine amabao bado hawajatambua kuwa cheo hiki ni batili.Hakipo.
 

Juzi mimi niliwatimua wajumbe walotumwa na balozi nikawaambia hilo ni jukumu la Mwenyekiti wa serikali za mitaa.Wakarudisha jibu kuwa nimekaidi amri ya serikali.Nikaletewa barua ya kuitwa ofisini.Huko akaitwa na huyo balozi,nikamwambia Mwenyekiti kuwa huyu simtambui na wala sitatii amri hiyo akitaka atangulie mahakamani.Nikamwambia kama ni kweli ana tawala kisheria basi barua ilitakiwa iandikwe na balozi huyu ya kuniita mimi lakini badala yake umeandika wewe.
Naandika hili ili kuwaeleza na wengine amabao bado hawajatambua kuwa cheo hiki ni batili.Hakipo.

uko sawa kabisa. sasa hatima yake imekuwaje? kaenda mahakamani au kapotezea? waangalie vizuri hao wazee wasije kukufanyia fitina lakini. uzuri hapo inaonekana bado unapata support ya mwenyekiti ila akiungana tu na balozi watakuumiza.
 
Haha nimeipenda hio, hawa mabalozi waccm kazi ya chama imewashinda wanaingilia kazi za wenzao.
 
Samweli Sitta wakati yuko Spika, kuna mbunge alitoa hoja kuwa mabalozi wa nyumba kumi wawe wanalipwa mshahara na serikali, Sitta alijibu kwamba, utaratibu wa mabalozi wa nyumba kumi ni utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi, hivyo serikali haiwezi kuwalipa chochote, labda Chama Chenyewe kitoe fungu lake ndio walipwe. Hivyo ndugu wanajamvi, Mabalozi hawa si utaratibu wa serikali, bali ni Mabalozi wa Chama Cha Mapinduzi.
 
Wakuu nadhani mmekuwa mkisikia malalamiko kwamba serikali ilikubali ujio wa vyama vingi lakini baadhi ya sheria hazikubadilishwa ili kuvifanya vyama vingi vifanye kazi badala ya ule mfumo wa chama kimoja. Tatizo kubwa lilikuwa hili la mabalozi wa nyumba kumi. Kuna sheria inawatambua hawa japokuwa hawapo kwenye mfumo wa kiserikali. Wakuu kama kuna mtu amewahi kuandikisha maelezo polisi basi nadhani amewahi kukumbana na swali hili: Nani mjumbe wako wa nyumba kumi? Hiyo ni confusion kubwa. Pia nadhani mnajua kuwa kwenye serikali ya mtaa kun Mwenyekiti na wajumbe wa serikali ya mtaa ambao si wajumbe wa nyumba kumi. Sina hakika kama hawa wanatambuliwa katika ile sheria inayowatambua wale wa nyumba kumi.
 
Back
Top Bottom