Balozi Edward Mhina Amefariki Dunia...

Mkulu Balozi Mwawado,

Mkuu vitu vyako humu ndani ya JF vina-amount to the level ya uablozi balozi, najua kuwa wewe ni mjasiriamali, lakini la Balozi Mwawado lina-fit sna ndugu yangu, anyways shukrani kwa wasifu wa marehemu.

kweli anatoa vitu vya kibalozi lakini angalia isije ikadhaniwa mwawado wa jf ndio yule balozi kassim mwawado anayetuwakilisha egypt nadhani. inaweza ikawa taaabu kweli!
 
Mwawado, any new developments? Please, keep us uptodate....

Marehemu atazikwa kijijini kwao Tongwe, Muheza Jumatano mchana.Jumanne jioni kutakuwa na Misa ambayo itafanyika St.Albans na baadaye kuuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake Makongo...Kwa wale watakaoenda Muheza -Tanga, safari itaanzia Makongo..kuna magari kadhaa ambayo yapo wazi kwa wanaotaka kuhudhuria Mazishi.

Serikali itawakilishwa na Waziri wa Elimu,katika mazishi hayo. Baadhi ya Watoto wa marehemu wamekwishawasili Dar-es-salaam kwa ajili ya utaratibu wa Mazishi ya Baba yao.Kama kuna chochote na Upo Dare-es-salaam usisite kuwasiliana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Vicent Mrisho) ambaye ndiye Mratibu Mkuu wa shughuli ya Msiba.

Mkuu BabaDesi kwa ufahamisho tu ni kwamba Eva amewasili mchana leo(Jumatatu) akitokea Washington Dc kwa ajili ya mazishi,na atakuwepo Dar mpaka baada ya 40.
 
Mkuu, shukurani nyingi kwako kwa information muhimu hii. Nilikuwa nimetoka kidogo lakini nashukuru kwa kuikuta hii na nakushukuru zaidi wewe. Nitajitahidi kumpata ili kumpa pole. Ubarikiwe.
 
Sisi wote hapa duniani niwapitaji makao yetu ni mbinguni kwa baba,Tulimpenda sana ila Mwenyezi Mungu yeye amempenda zaidi.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
Amen.
 
Alikuwa hana makuu baba wa watu. Aliitumikia Nchi kwa UADILIFU mkubwa mno na heshima kubwa. Wengi mtakumbuka jinsi alivyozifanya nchi hizi za SCANDINAVIA ZIIAMINI sana Serikali ya Mwalimu na kutusaidia sana Watanzania. Miezi ya hivi karibuni nimemuona akitumia usafiri wa kawaida hapa mjini, akikaa maeneo ya kawaida kabisa na kujichanganya na watu wa kawaida kabisa. Mungu ailaze roho mahala pema peponi. Amina.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom