Ballali Anyang'anywa Viza ya Marekani & Wengine Wasema Tayari Keshakimbilia Malta !

Mnakumbuka balozi Sefue alisema hajui Ballali amelazwa wapi? Je ni juhudi zipi alizofanya kama balozi ili kujua Ballali amelazwa wapi? Au alikuwa ni mmoja waliokuwa wanafahamu kwamba Ballali ameshaondoka Marekani?

Katika hatua nyingine kumhusu mtuhumiwa huyo wa ufisadi, Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa amedai kuwa baada ya Ballali kufukuzwa kazi wiki iliyopita alitorokea katika Kisiwa cha Malta kwa lengo la kujificha.

Katika mahojiano na Mwananchi, Dk Slaa alidai kuwa amepata habari kuwa wiki iliyopita Ballali aliondoka Marekani kwa ndege ya kukodi kuelekea Kisiwa cha Malta ili asiweze kurejeshwa nchini kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

"Nimepata taarifa kwamba Ballali wiki iliyopita alikodi ndege kwenda kujificha katika Kisiwa cha Malta ili asirejeshwe nchini, pia nimeambiwa aliondoka na madaktari watatu, baadaye nitatoa majina yao na namba za ndege aliyotumia," alisema Dk Slaa.

Awali, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jaffery Salaiz, alisema wameamua kumfutia viza baada ya serikali ya Tanzania kuulizia hadhi ya gavana huyo anaposafiri au kuwako nchini mwao.
 
Soma barua pepe
Wasiliana nasi
Nafasi za kazi
Burudani na Starehe
Kolamu Maalum

Habari zaidi



Misemo na nahau
"Bahati ni upepo sasa upo kwangu"

Habari za kawaida
Posted Date::1/16/2008
Ufisadi BoT: Baada ya kufukuzwa kazi, Marekani yamfutia viza Dk Ballali
* Ubalozi wasema hastahili kuishi nchini humo

* Wasema hawajui anakotibiwa

* Ndulu asisitiza kuwa bado ni mgonjwa

Dennis Msacky na Ramadhan Semtawa

SERIKALI ya Marekani ikiwa imetangaza kumfutia viza aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daud Ballali, anadaiwa kuwa ametorokea kwenye Visiwa vya Malta.

Kufuatia kufutiwa viza, Ballali sasa haruhusiwi kuishi wala kwenda nchini Marekani.

Katika hatua nyingine kumhusu mtuhumiwa huyo wa ufisadi, Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa amedai kuwa baada ya Ballali kufukuzwa kazi wiki iliyopita alitorokea katika Kisiwa cha Malta kwa lengo la kujificha.

Katika mahojiano na Mwananchi, Dk Slaa alidai kuwa amepata habari kuwa wiki iliyopita Ballali aliondoka Marekani kwa ndege ya kukodi kuelekea Kisiwa cha Malta ili asiweze kurejeshwa nchini kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

"Nimepata taarifa kwamba Ballali wiki iliyopita alikodi ndege kwenda kujificha katika Kisiwa cha Malta ili asirejeshwe nchini, pia nimeambiwa aliondoka na madaktari watatu, baadaye nitatoa majina yao na namba za ndege aliyotumia," alisema Dk Slaa.

Awali, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jaffery Salaiz, alisema wameamua kumfutia viza baada ya serikali ya Tanzania kuulizia hadhi ya gavana huyo anaposafiri au kuwako nchini mwao.

Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za uhamiaji za nchi hiyo, kuanzia sasa Ballali hawezi kuishi katika nchi hiyo wala kusafiri kwa kuwa viza yake imefutwa.

"Hakuna njia yoyote Ballali anaweza kuishi Marekani kwa kuwa viza yake imefutwa, hata kama ana mali kule," alisema.

Pia Afisa Balozi huyo alipoulizwa kama wana habari kuhusiana na Ballali kuwako katika matibabu nchini Marekani, alisema mpaka sasa hawajui kama kweli yuko nchini mwao, kwani wao wamekuwa wakisoma katika vyombo vya habari vya ndani.

"Mpaka sasa hatuna uhakika kwamba Ballali yuko Marekani, habari za kuwako kwake Marekani tumezipata kupitia vyombo vya habari vya ndani, lakini kama ubalozi hatuna taarifa rasmi kwa hilo," alisema.

Alisema Ballali alikuwa na viza ambayo alipewa kwa wadhifa wake wa kuwa Gavana wa BoT, lakini baada ya kufukuzwa kazi kwa madai ya ufisadi, imefutwa.

Hata hivyo, alisema kama Ballali atakuwa nchini Marekani basi itambidi arejee nchini Tanzania kwa kuwa hana kibali cha kuishi nchini humo.

Katika taarifa ya awali ya ubalozi, ilisema hatua hiyo inatokana na Ballali kutokuwa tena gavana wa BoT baada ya kuachishwa kazi.

Ballali ameachishwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kubainika ufisadi wa zaidi ya Sh 133 bilioni ambazo zililipwa chini ya uongozi wake.

Ufisadi huo unahusu Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ambayo ukaguzi wa Kampuni ya Ernst&Young, ulithibitisha kufanyika katika kipindi cha mwaka 2005/06.

Marekani ikizungumzia zaidi sakata hilo, ilisema Tanzania iliulizia kuhusu hadhi ya Ballali, baada ya kuachishwa kazi kufuatia kubainika ufisadi huo mkubwa wa fedha za umma katika akaunti moja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali ya Marekani tayari imeitaarifu Serikali ya Tanzania kuwa inabatilisha viza ya Ballali kwa sababu haiwakilishi tena Tanzania.

Marekani ilisema Ballali alipewa viza hiyo kutokana na wadhifa wake kama mwakilishi wa Serikali ya Tanzania.

"Kwa hiyo, kwa sababu ajira yake sasa imesitishwa, haiwakilishi tena serikali ya Tanzania na hastahili kuwa na viza aliyo nayo sasa hivi ambayo siyo ya kuhamia Marekani (non-immigrant visa status).

"Kuongeza uwazi na kupiga vita ufisadi ni maadili makuu mawili ambayo

Serikali ya Marekani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

vinayathamini sana," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Marekani inaunga mkono uamuzi wa Serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi kuhusu ubadhirifu uliofanywa kwenye BoT na inaamini kuwa uamuzi huu unadhihirisha azma ya Rais Kikwete kupambana na vitendo vya rushwa.

Katika taarifa hiyo, Marekani ilisema kuwa uchunguzi na ufunguzi wa mashtaka

wa haraka kwa wahusika katika kadhia ya BoT ni muhimu.

"Nchi zetu mbili zinafanya juhudi za dhati kufanya kazi pamoja kwa karibu katika

kung'oa mizizi ya rushwa na kumpeleka mbele ya vyombo vya sheria, mtu

yeyote atakayepatikana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa," ilisema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alimweleza mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake jana kwamba, haijajulikana lini Ballali atarejea nchini kwa kuwa bado anaendelea na matibabu.

Profesa Ndulu alifafanua kwamba, Ballali kwa sasa anapata matibabu katika hospitali ambayo iko karibu na nyumbani kwake.

"Siwezi kujua atarejea lini nchini kwa sababu bado anaumwa, kuumwa anaumwa kweli," alisema Profesa Ndulu.

Kumekuwa na utata kuhusu Ballali kwamba amekuwa na uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Marekani hivyo kuwepo hofu ya kutorejea nchini.

Hata hivyo, uamuzi huo wa Marekani unaweza kuwa hatua moja mbele katika kushirikiana na serikali ya Tanzania kumrejesha Ballali nchini iwapo atahitajika kuja kujibu tuhuma za ufisadi.
 
Baadaye hawa waandishi wakijua kuwa haya si ya kweli sijui watayakana au vipi?

PR zingine bwana? watu wanalishana makasa sana huko bongo!
 
Hiyo Malta iko ahera? Tunamuhitaji mtu wetu kwani nafasi bado ipo kule Ukonga, Keko etc.
 
Mwafrika naungana na wewe kwamba hii ni PR Ballali hajafutiwa chochote na yuko US anaendelea na matibabu yake .Hajaenda kokote huku ni kulishana makasa.Ushabiki huu hauna maana wakati mwingine kuweni na investive report kabla ya kuanza kupamba habari.
 
kabishaneni na hao mwananchi na hata Dr Slaa
hiyo ni copy and paste na hata hivyo lisemwalo lipo kama halipo laja.
Na nyie mnaojua alipo naomba mtuhabarishe anaendelea je kiafya
 
Mimi nimeshasema hizi habari kuhusu Balali asilimia 90 ni majungu na uzushi na kumi zilizobaki ni nusu ukweli...
 
nakubaliana na wewe INVINCIBLE, kwamba tunaowaita usalama wa taifa kwa hakika ni USALAMA WA CCM!

kama kweli usalama wa taifa wanafanya kazi yao inavyotakiwa, hizo fedha zisingeibiwa kiasi hicho.lakini zinaibiwa kusaidia kukandamiza upinzani, huku mafia wachache wakijaza vitambi vyao.INSTITUTIONS za serikali hazifanyi kazi iliyousudiwa.
 
Inanisikitisha sana kuona usanii unaochezwa sasa ni wahali ya juu.
Habari za kuaminika ni kwamba kikwete alikutana na Balali DC kati ya december 12 na 14, 2007. Na ni Balali aliyekwenda DC kumwona kikwete. Halafu tunaambiwa Balali yu mgonjwa akiwa amefanyiwa opereshini massachusetes. Sasa balali amekimbia Marekani kakimbilia Nchini Malta.

Kama haya yote ni kweli, kiongozi mkuu wa nchi na wasaidizi wake wote wamekuwa wakitudanganya. Wanajua nini kinaendelea na nini kinafichwa. Tumeibiwa sisi, tunalia sisi, tuna kufa sisi, wao mambo yao mswano
 
Malta of all places? He can't be that stupid!

The Following 2 Users Say Thank You to Pundit For This Useful post:

Jasusi (Yesterday), Mzee Mwanakijiji (Yesterday)

Kwenye hii topic so far ninaziamini hziz hapa juu, reading between the lines ina maana Balali bado yuko US,

My Take:-

Something is not right, either kuna mkono wa serikali yetu kwenye US kumnyima viza na hatimaye kujaribu kumrudisha kwa nguvu ili azimwe asiyatoe anayoyajua, au kuna kinyamkera hapa kinacheza,

Ninasema enough, kwa sababu wale tuliowaaminia kutupa dataz hawatupi, sasa nimeamua kuziingilia mwenyewe, kama kuna aliyenazo na hataki kuzitoa kwa sababu zinazoeleweka, tuwasiliane, ikifika kesho asubuhi nitaanza kuzitafuta, and guess what nitaziweka hapa JF, mkuu Halisi nitakutafuta asubuhi!

Hiii ni Jf huwa hatushindwi kuzipata!
 
FMES,
Ile ya kumrudisha kwa nguvu sahau. They would have wanted him dead. You just wait. There is a big PR game being played here. Unfortunately wachezaji wote ni amateurs. Kwa sasa hivi kwa Balali kujibizana nao hakutamsaidia. Ngoja waweke karata zao zote hadharani. Atakuja na karata ya mwisho. Kwa sababu kama ni kumrudisha nyumbani si wamfungulie mashtaka wayakabidhi kwa Interpol? Simple!
 
Jasusi,

Ukiwa makini utagundua mapungufu kibao kwenye hizo habari.

Hii inaonyesha kuwa wale waliokula hizo hela wanacheza na magazeti ya bongo na kupoteza watu mwelekeo. Ndo maana nilikuwa nawasoma watu hapa wanavyoshabikia visa vya kutungwa.
 
Hawezi kupewa special treatment when it comes to a remand prison. That will contravene with the principle of equality before the law. Lakini let us not be naive jamani, he is a kafara here. there is no way he could have done this alone and they might kill him to keep the secrets from coming out..
 
Jasus, you are right: "There is a big PR game being played here. Unfortunately wachezaji wote ni amateurs".
Mengi tumeshayasikia kuhusu Balali, we have the report, kama kweli kapona kifo cha sumu basi ashukuru "mizimu" yake.
Lakini hapa ni "kamba hukatika pembamba"; Dr. Slaa you should go for the heavyweights, Mr. Kikwete, Wariobas's Meremeta, Rostam's etc etc as you (Dr Slaa) showed us the way how you investigated the BOT scam, you have to fight for the full report on Ernest & Young. We are forgetting that Ballali and the culprits (kati yao ni former and sitting Presidents )is part of scandal which is 133 billion, we are having on hand a Richmond Scandal which is worth more than 170 billion.
Maana yangu ni kuwa to win this fight, please FIGHT For the release of the full Ernest & Young report. The president is hiding something here!! Also go systematically and be vigilant on other issues, these guys (in the Government) have made us busy with Balali giving them time to play with Richmond and buzwagi reports!!
 
Back
Top Bottom