Ballali aibuka na kujibu

Status
Not open for further replies.
Mwanakijj samahan..thread ya ufisadi ATCL siioni...nimepost kidogo link ikaunganishwa kwa admin..vipi tena kulikoni...
Thanks for your inquiry, the thread you are after is currently being updated but it is also on hold pending verification. All your posts are in safe hands. It will be brought back once ready. Thank you and have a good day!
 
FMES,
Naomba uwasiliane tena na sources zako. Balali hajaongea na haja"authorize" yeyote kuongea kwa niaba yake. Wakati utafika, Balali ataongea. Believe me!
 
kuna mtu anawaingiza mjini watu nyumbani we ngoja.. hasa makala ya Tanzania Daima kesho.. subirini tu muone.. wenye kujua hawasemi, na wanaosema wanadhani wanajua.. ndio maana kuna mtu kampa "data" Dr. Slaa kuwa jamaa kakimbilia Malta na hivyo Dr. Slaa akakimbilia kwenye vyombo vya habari. Ningekuwa mimi wao, nisingeharakisha kusema...
 
Naomba uwasiliane tena na sources zako. Balali hajaongea na haja"authorize" yeyote kuongea kwa niaba yake.


Mdogo wa Ballali ambaye anaishi naye Boston, Marekani ameliambia gazeti hili kuwa kaka yake ambaye sasa anaendelea vyema

Mkuu Jasusi,

Heshima mbele sina source zaidi ya hiyo hapo juu, una maana hawa magazeti wanadanganya kumbe?

By the way mbona kuna watu wanamuongelea kila siku hapa JF au?
 
Mkuu Jasusi,

Heshima mbele sina osurce zaidi ya hiyo hapo juu, una maana hawa magazeti wanadanganya kumbe?

Kuna tatizo kubwa sana katika mtiririko wa Habari kuhusu Ballali na BoT.... Tuwe makini sana na watoa habari kwani hivi sasa watu wengi wenye maslahi na suala hili wameingia kwa nguvu kubwa na baadhi wana ushawishi mkubwa katika jamii ya Watanzania... Lakini jambo la msingi ni kusubiri Ballali mwenyewe kutoa tamko na si kupitia kwa mtu ambaye hata hatajwi jina. Pia inawezekana mtu anayejiita mdogo wake, aliongea na mtu na mtu akaongea na mwandishi bila kusema wako mji gani na ndipo Mwandishi akachukulia juu juu tu (kwa kutumia taarifa ya Serikali) kuwa yuko Boston.

Lakini hata mimi mtu mwingine anasema Ballali amesema, "Ballali amesikitika sana na yalotokea. anarudi kwa kuwa yeye ni mtumishi wa umma, hajafukuzwa kazi na anataka na yeye kueleza upande wake" kwa kauli hiyo ni kwamba bado hajasema upande wake maana kama alimtuma mtu kusema, angesema yale nilioyosema..... Japo naamini yaliyosemwa hayako mbali na ukweli, kwamba ANA SIRI NZITO na yuko tayari kuchunguzwa YAISHE na yeye na FAMILIA YAKE WABAKI KWA AMANI
 
Kuna ujumbe ulipelekwa jana kwa Balali.. subirini hii wiki inayokuja.. unapocheza chess hakikisha unamlinda King! CCM wamesahau hilo..

Mwanakijiji,

Hiyo chess yhao inatusaidia nini sisi wananchi wa kawaida? Yeye kama anawajua waliomlazimisha kuchota pesa zetu basi awataje, haya mambo ya chess ni ujinga mtupu.

Kama mtu ni clean na huna cha kuficha kwanini ujifiche? Yeye aitangazie dunia kwamba ana rudi na hana cha kuogopa na kuomba ulinzi ili asidhuriwe.

Kinachofanyika sasa ni mafisadi kuchezeana chess bila heshima yoyote kwa wananchi ambao ndio waliwakabidhi hivyo vyeo na ndio wameumia kwa ujinga wao huo.

Ballali huyo huyo aliyeenda bungeni akadanganya, kwenye vyombo vya habari akadanganya, mnampa benefit of doubt kwa misingi ipi?

Hawa viongozi wetu wanatuchezea kweli kweli. Kama kilichotokea kwenye mashamba yake si dalili tosha kwamba muda wa ubabaishaji unafika mwishoni. Asipoangalia wananchi watafanya mabaya hata zaida ya hayo.

Wenzake wamesema yeye ndiye kachota, anasubiri nini kuweka ukweli wake wazi?

Hapo yuko tayari kumlinda Mkapa kwa nguvu zote.
 
FMES,
Naomba uwasiliane tena na sources zako. Balali hajaongea na haja"authorize" yeyote kuongea kwa niaba yake. Wakati utafika, Balali ataongea. Believe me!

Mkuu Jasusi,

Ni kweli tunajua Ballali hajasema lakini pia tunajua kuna cordinated efforts toka upande wake ku SPIN habari kwa faida zake.

Kama hajasema, kitu gani kinamzuia kusema? Akumbuke maneno ya Salim, uwongo ukiachiwa kurudiwa na kurudiwa baadaye watu wanaweza kuamini kama ukweli.

Sasa mpaka waziri anatangazia umma kwamba Ballali alimdanganya, yeye kabana angle tu. Kinachommaliza Ballali ni ule uwongo alioutoa kwenye TV na kwenye bunge. Kama wakati huo alidanganya kwanini tuamini sasa anasema ukweli?
 
1. Hiyo chess yhao inatusaidia nini sisi wananchi wa kawaida?

2. Yeye kama anawajua waliomlazimisha kuchota pesa zetu basi awataje, haya mambo ya chess ni ujinga mtupu.

3. Kama mtu ni clean na huna cha kuficha kwanini ujifiche?

4. Ballali huyo huyo aliyeenda bungeni akadanganya, kwenye vyombo vya habari akadanganya, mnampa benefit of doubt kwa misingi ipi?

5. Hawa viongozi wetu wanatuchezea kweli kweli. Kama kilichotokea kwenye mashamba yake si dalili tosha kwamba muda wa ubabaishaji unafika mwishoni. Asipoangalia wananchi watafanya mabaya hata zaida ya hayo.


6. Wenzake wamesema yeye ndiye kachota, anasubiri nini kuweka ukweli wake wazi?


Mtanzania Heshima mbele,

Maneno mazito haya, na ndio kumkoma nyani kwenyewe huku! Saafi sana mkuuu tembeza bakora and let the chips fall where they may!
 
Fisadi Mtoto Kumbe Mnajua Jinsi Mama Na Baba Zenu Wasivyona Aikili Hata Kugundua Ref No...embu Wawaonyeshe Kabla Ya Kuzitoa Muwasaidie Kuhakiki Ndio Maana Nawapongesa Kwa Kujitahidi Kuwapeleka Shule Baada Ya Wao Kuc,,,,a..tupe Mengine We Ni Shaidi Muhimu Kwetu Wana Jf Utatusaidia Sana Inaonekana Unamambo Mengi Yamwage Kijana Nikupe Fisadi-mkubwa
 
Mkuu Jasusi,

Ni kweli tunajua Ballali hajasema lakini pia tunajua kuna cordinated efforts toka upande wake ku SPIN habari kwa faida zake.


Naomba uwasiliane tena na sources zako. Balali hajaongea na haja"authorize" yeyote kuongea kwa niaba yake. Wakati utafika, Balali ataongea. Believe me!

Mkuu Wangu Jasusi,

Heshima mbele mkuu, pole mkuu I mean kwamba for once na wewe this time arround uko kwenye upande wa pili wa fence, maana siku zote huwa uko mstari wa mbele kuwapiga mawe mafisadi, what an experience no? It is very hard ndugu yangu kutetea fisadi na ufisadi kwa ujumla,

I feel for you mkuu lakini ninayaaminia maneno yako kuwa Balali, atafanya the right thing in time kwanza kwa kurudi nyumbani bongo ambako hajafukuzwa na mtu, na pili atajibu tuhuma dhidi yake ambazo tayari zimeshaanza kutolewa wazi! Otherwise there is nothing personal against him au wewe! Binafsi nimesubirir sana kuheshimu maneno yako kuwa in time atasema na kwamba tusimhukumu bila facts, lakini sasa facts zimeanza kutoka mkuu kwa hiyo ndio maana tuna-react tu on zile info zilizotoka, lakini pia tunasubiri upande wake, ila in the meantime ni kumkoma nyani tu!

Ahsante Mkuu.
 
Mwanakijiji,

Hiyo chess yhao inatusaidia nini sisi wananchi wa kawaida? Yeye kama anawajua waliomlazimisha kuchota pesa zetu basi awataje, haya mambo ya chess ni ujinga mtupu.

Kama mtu ni clean na huna cha kuficha kwanini ujifiche? Yeye aitangazie dunia kwamba ana rudi na hana cha kuogopa na kuomba ulinzi ili asidhuriwe.

Kinachofanyika sasa ni mafisadi kuchezeana chess bila heshima yoyote kwa wananchi ambao ndio waliwakabidhi hivyo vyeo na ndio wameumia kwa ujinga wao huo.

Ballali huyo huyo aliyeenda bungeni akadanganya, kwenye vyombo vya habari akadanganya, mnampa benefit of doubt kwa misingi ipi?

Hawa viongozi wetu wanatuchezea kweli kweli. Kama kilichotokea kwenye mashamba yake si dalili tosha kwamba muda wa ubabaishaji unafika mwishoni. Asipoangalia wananchi watafanya mabaya hata zaida ya hayo.

Wenzake wamesema yeye ndiye kachota, anasubiri nini kuweka ukweli wake wazi?

Hapo yuko tayari kumlinda Mkapa kwa nguvu zote.

Tumeyaskia mengi humu, sijui nani ana-spin nini na kwa faida ya nani; what we know now even the mode of operation of the BOT is not well known to many especially in this forum. Kama kweli JK aliestablish kuwa Balali alibenefit kutokana na kuhalalisha hizo pesa basi balali is corrupt. But also we are reading that, Gavana ni mtumwaji tu na wanaSiasa kutekeleza mambo; PS ndiyo anatoa order. Another issue here, why are some of you guys here want us to believe that JK sacked the right man while he is not revealing the whole Ernest & Young report? And also why shud balali mention others; hivi ni kazi yake kuwataja? Everything is well known, who authorised payments, and where the money was deposited. Gavana hawezi kukataa ku-realese pesa ambayo imehitajika kutoka kwa wakubwa zake. The president must act fast!
 
But also we are reading that, Gavana ni mtumwaji tu na wanaSiasa kutekeleza mambo;


Mkuu IO,

Heshima mbele mkuu, sijakuona siku nyingi ila ninakumbuka mara ya mwisho ulikuwa unampa big support Tafiti Then Jadili (TTJ) sikuji aliishia wapi,

anyways, nafikiri kama unafuatilia kwa makini hiii mijadala tumeanza na Mama Meghji, baada tu ya kugundua kuwa alihusika na ku-support barua ya ulaji ilioandikwa na Balali, na since then tumekuwa tukilia na hawa wawili unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu so far tuna a hard evidence kuwa walishiriki kwenye ufisadi, including Mgonja, na Mramba, wote tumekuwa tukiwapiga mawe sawa sawa,

Mawe ya Balali, (sitaki kuamini kuwa wewe ni Jasusi), ni kwamba Balali amejiongezea mzigo mzito kuhusiana na tuhuma dhidi yake kwa mambo aliyoyafanya mwishoni kuaniza kusaifiri nje, na mpaka kufikia kuandika barua ya kujiuzulu akiwa nje ya nchi, wenziwe owte wako bongo hawajakimbia, yeye peke yake ndiye aliyekimbia, mara anaumwa, hataki kuongea na mtu, sasa imekuwa hadithi nyingi mno kuhusiana na yeye tu huku wnegine hawasemwi, ni kwa sababu alijitafutia mwenyewe hiii attention, sasa nyinyi apologists wake msimlaumu mtu ila mlaumuni Balali mwenyewe kwa kujiletea unwanted attention ambayo inafikia mahalai hata wengine waliohusika hawatajwi ila yeye tu, ndio maana tunasema arudi nyumbani ajibu tuhuma dhidi yake ambazo tayari zipo, sasa kwenye kujibu ndio atatuambia nani alimtuma na nani hakumtuma, uamuzi wa kama anayosema ni kweli au sio kweli ni wa kwetu wananchi sio nyinyi mnaomtetea,

Naifikiri unaijua bongo vyema na kwamba msema kweli ni mpenzi wa Mungu, wananchi tutaamua kulingana na tunayosikia kutoka kwa viongozi wetu waliohusika, lakini tunahitaji kusikia Balali's side now, maana wanamtuhumu wameshasema, until atakapoongea yaani Balali, sisi wananchi tutaendelea kumkoma nyani based on evidence at hand ambayo tunayo tayari, inayoonyesha kuwa Balali, alichota na kumuomba Mama Meghji, amsaidie na uchunguzi, nothing personal against Balali, wale wote mnaomtetea naomba mtuelewe kwamba sisi ni wananchi acting on information already at hand!

Hatuwezi kua-act on information ambayo hatuna lakini mnayo nyinyi tu mnaomtetea tu, hapana tutaendelea kumkoma nyani tu mpaka giladi!
 
Nahisi siku Balali atakapoongea hizi posts zote tutazifuta, tutajiona weupe kweli. Hata hivyo washauri wa Balali inabidi wajue kwamba wakati ni factor kubwa hapa na wamkumbushe pia kwamba uongo ukikaa muda mrefu hugeuka kuwa ukweli! Haya yeye aendelee kukalia habari, anafikiri wenzake wamelala au ndio wanajiandaa kummaliza zaidi?
 
.......................the mode of operation of the BOT is not well known to many especially in this forum. Kama kweli JK aliestablish kuwa Balali alibenefit kutokana na kuhalalisha hizo pesa basi balali is corrupt. ..................!

Maneno mazito sana hayo ndg IO

1. Operation ya BoT
2. Who is corrupt within BoT?.................... (at this instance Balali ni culprit) why kwa sababu yeye ndio Accounting Officer wa BoT

Tujue ya kwamba Acoounting Officer wa BoT (Balali) hufanya kazi yake kwa ushauri/mapendekezo toka kwa wasaidizi (kuanzia senior officers yaani Directors mpaka manaibu wake) + Bodi ya BoT, na wakati mwingine yeye mwenyewe hutoa directives....

sasa tatizo limetokea ni kutokana na
1. directives zake yeye kama Gavana au
2. kutokana na mapendekezo ya Officers below him (this includes him) au
3. Bodi ya BoT

kwa hiyo utaona kila sehemu Balali yupo kwa ni rahisi kum-pinpoint yeye kutokana na maelezo hapo juu

Huko nyuma niliwahi kuuliza Gavana anaripoti kwa nani? Rais?, Waziri? au PS? Bodi? na je Gavana kama anapewa directives je hizo directives hutoka kwa nani kati ya watu hao hapo?

Tukisha-establish hiyo chain then tutajua nani alifanya nini kwa madhumuni gani. Mpaka sasa hivi watu ambao uteuzi wao ilibidi UTENGULIWE (maana isiwe balali peke yake) nafikiri ni

Gavana....huyu tayari
Wakurugenzi wake wahusika
Naibu/Manaibu Gavana

Bodi ivunjwe na itakayoteuliwa iwe na wajumbe wapya.....thus inabidi akina PS nao uteuzi wao utenguliwe.......ofcourse bila kumuacha Waziri Mramba
 
Maneno mazito sana hayo ndg IO

1. Operation ya BoT
2. Who is corrupt within BoT?.................... (at this instance Balali ni culprit) why kwa sababu yeye ndio Accounting Officer wa BoT

Tujue ya kwamba Acoounting Officer wa BoT (Balali) hufanya kazi yake kwa ushauri/mapendekezo toka kwa wasaidizi (kuanzia senior officers yaani Directors mpaka manaibu wake) + Bodi ya BoT, na wakati mwingine yeye mwenyewe hutoa directives....

sasa tatizo limetokea ni kutokana na
1. directives zake yeye kama Gavana au
2. kutokana na mapendekezo ya Officers below him (this includes him) au
3. Bodi ya BoT

kwa hiyo utaona kila sehemu Balali yupo kwa ni rahisi kum-pinpoint yeye kutokana na maelezo hapo juu

Huko nyuma niliwahi kuuliza Gavana anaripoti kwa nani? Rais?, Waziri? au PS? Bodi? na je Gavana kama anapewa directives je hizo directives hutoka kwa nani kati ya watu hao hapo?

Tukisha-establish hiyo chain then tutajua nani alifanya nini kwa madhumuni gani. Mpaka sasa hivi watu ambao uteuzi wao ilibidi UTENGULIWE (maana isiwe balali peke yake) nafikiri ni

Gavana....huyu tayari
Wakurugenzi wake wahusika
Naibu/Manaibu Gavana

Bodi ivunjwe na itakayoteuliwa iwe na wajumbe wapya.....thus inabidi akina PS nao uteuzi wao utenguliwe.......ofcourse bila kumuacha Waziri Mramba

Ogah,

Wana JF wanajua kati ya tuhuma na facts. Mpaka sasa tuna watu wawili ambao
uwizi wa BOT umeonyesha wazi wanahusika kwa njia moja ama nyingine. Hao ni Meghji na Ballali. Wote tumewajadili hapa bila upendeleo.

Wanaobaki bado ni tuhuma na ndio maana mapambano ya kuilazimisha serikali ili itoe report ya E&Y yanaendelea maana hata sisi tuna uwezo wa kuisoma na kuielewa.

Hapa hatumuonei Ballali, yeye kwanza kafukuzwa kazi, ikiwa na maana kuna makosa kafanya, katajwa na waziri wa fedha tena kwenye vyombo vya habari kwamba alimdanganya na kwamba hizo pesa hazikutumika kwa kazi ambayo Ballali aliisema mwanzoni.

Pamoja na hayo yote yeye kakaa kimya, kajificha nje ya nchi, anasema anaumwa, mara kapewa sumu na kigogo, mara kaambiwa asirudi TZ, ili mradi kuna juhudi ya makusudi ya kutaka kuonyesha kama Ballali anaonewa.

Kama anaonewa si atoke nje na aseme wazi yeye mwenyewe? Kwani kuna haja ya kusemewa na watu?

Tunataka yeye awataje waliomtuma ili tuendelee kuipanua list yetu mpaka tutakapofika kule juu ambako aliyewatuma ndio yuko.

Kwa yeye Ballali, mimi naona ni guilty maana hata kwa kwenda tu bungeni na kudanganya tayari ni kosa kubwa. Ilitakiwa hata sasa spika aite polisi na kumchukulia hatua maana aliidanganya kamati ya bunge.
 
Mtanzania,
Nakuhakikishia hakuna coordinated efforts from Balali's side to spin. Tunayoyasikia na kuyasoma kwenye magazeti au hata hapa JF nothing has come directly from Balali. Soma tena bandiko la Halisi. He is closer to the truth on this. FMES, bado niko mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, uwe umefanywa na kiongozi nimjuaye au nisiye mjua. Lakini katika hili there are so many factors, and I know from reading threads here kwamba there is an anxiety that Balali should speak up. Ndugu zake have adviced him the same pia marafiki zake. But that is a decision he has to make on his own taking in consideration his health status. I have said it before and I will say it again, let us be patient. God willing, and his health allowing, he will help to put this issue to rest.
 
Heshima mkuu Jasusi,

Nimekusikia mkuu, sasa naona tusubiri tu what Balali has to say, lakini the more anavyochelewa ndivyo anawapa nafasi wa uapnde wa pili kujiweka sawa kwenye kimjibu au hata kumuwahi kabla hajajibu, anyways binafsi nitasubiri mpya from now on!
 
Hivi Gavana anaripoti kwa nani?.........najua kuna appointment fulani ambazo wateuliwa wanaripoti kwa Rais moja kwa moja.......nao ni kama ifuatavyo (correct me if im wrong)

Gavana wa Central Bank
DG wa TISS
Chief Justice
CDF
IGP
Chief Secretary (ofcourse)
DG wa PCCB

Hawa nafasi zao somehow/somewhat ni very powerful kuliko hata mawaziri....wee chunguza utaona

sasa kama Balali alipewa some Directives na President wakati huo....tulishaambiwa na JK kuwa tumuache Mzee wetu apumzike....case closed......na vile vile yeye mwenyewe Balali akija na kusema pesa alizozitoa zilikuwa ni kwa ajili ya Usalama wa Nchi na ikithibitika hivyo yenyewe pia itakuwa Case Closed.......ndio maana wakti ule mtu kaanzisha mada hapa Balali ni kafara hii ilikuwa statement nzito sana ya kuitazama kwa undani

Kama E&Y walikutana na vitu....wakataka kudadisi wakaambiwa ni classified inf...........then Case Closed!!!

Tunayo jadili sasa hapa JF ni haya makampuni yaliyotajwa na wahusika wake.

Balali kama alitumia nafasi (madaraka) yake kwa advantage yake na kupindisha (be it kwa kushauriwa or not or both) taratibu basi Kesi anayo ya kujibu na ndilo linaloonekana hapa JF sasa hivi.

sidhani kama kuna mtu anamtetea Balali...........Balali ana madhaifu yake meeengi sana......kuanzia kwenye Zabuni za kutengeneza fedha mpaka hizo Twin Towers............kuna wakti quality ya noti zetu ilikuwa ni kichekesho...........mpaka ikawapa mwanya matapeli kuutumia mwanya huo kutengeneza pesa feki..............hao ndg zake waache kuweweseka, Balali mwenyewe ikifika wakti wake atasema kama alivosema siku ile na waandishi wa habari...........Mungu aendelee kumpa uzima ili asije akanyamaza na ubaradhuli uliotokea
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom