Ballali aibuka na kujibu

Status
Not open for further replies.
Andrew Chenge...Yumo..Na huyu nani nani...Mkapa..Jamani wapo wengi...

Ni Aibu...Ina naana Huyu Jaamaa Tayari alisha kua Raia wa nchi Mbili Kabla hata Ya Sheria ya nchi Yetu Kuruhusu Hivyo?
 
Lunyungu: hizi barua zitakuwa ziliandikwa na waziri kweli au ni ni sumu hiyo, naona zimekaakaa tu!
 
Kitila i had the observation when i saw the letters. Kwenye tovuti mja mpiga picha alipiga picha vizuri sana kwa hiyo maandishi yaliweza kuonekana, Zakia mwenyewe akiwa ameshika hizo barua!
Huwezi amini barua ya kitoto kama hiyo anaandika waziri!
 
Nimelata hapa ili kusaidia kuona kwamba kuna kampeni kali na wanataka kuzima the whole kwa jina la Ballali. barua haya sahihi haina ? Ile ya Ballali kujiondoa alianguka .Barua hata ref hazina . Wana mtandao sasa wamepata pa kuegemea na kuanza kusema hizi ndiyo barua lakini mimi nazikataa nimeleta tu for your preusal na si kwamba ndiyo za Meghji . Najaribu kutafuta zile original lakini zimefukiwa mbali ila sitakata tamaa kuzitafuta .Hizi si za kweli ni danganya toto .Serikali haina tabia ya kuweka nje mambo yake iweje hili waweke ? Wanajisafisha lakini tutaujua Ukweli . Nangoja Ballali amwage njugu hapo tuanze upya kukamatana .

Majira wanakazana na story za kila siku za kujenda PR lakini si hapa JF na hata wadanganyika wanaamka si mchezo .

Salaam toka kivuko cha Zanzibar .
 
Lunyungu,

Jamani hapa bado kabisa ngoma mbichiiiiiii!... Yaani barua aandike Balali lakini sahihi chini iwe ya waziri wa fedha!...kisha hakuna CC kuonyesha kwamba copy imekwenda kwa gavana.. Haya ile ya majibu imetoka kwa waziri wa fedha na copy tunaiona kwa Balali yaani hata sielewi kabisa mchezo mzima ulifanyika vipi...Je, ina maana Balali alitumia mdomo wake tu kumfunga kamba Bi. Zakhia bila maandishi?...yaani kiofisi hakuna barua (kama yake kwa hao jamaa) inayomsisitiza yeye kuweka sahihi?
 
Hutu Mama amekuwa muongo wa kila wakati na mara kadhaa amesema uongo akiwa chini ya kiapo .Unajua hapa ndipo wanapokosea sana kila mara once they are caught .Wakitaka tuelewe maadam wameanza kutoa barua zao basi aanze na zile za kuelezwa na Ballali . Mimi nachojua mtake msitake simtetei Ballali lakini kama ilivyo sema yeye alikuwa anapewa amri tu . Kama kachota na yeye basi si sehemu kubwa . Wanapiga tarumbeta sana lakini ukweli wa mambo upo pale pale .

Walisema hana Visa ya US lakini hadi sasa yuko US . walisema kakimbilia Malta nasema bado katulia US na hana wasi wasi . Yote hii ni PR na hili litawaumiza wengi. Slaa kasema amesikia kwamba kakimbilia Malta hakuko confirm alisema amesikia magazeti yakapokea kwa ushabiki lakini watakuja kujuta .

I urge Ballali aje aseme kilicho tokea wakati huo maana kinacho tokea leo sote tunakiona .

Wanasema account kuwa freezed hilo ni dogi because we cannot verify it ila wawakamate wote kwa mpigo hapo tuone kama hawajaanza kutajana . I am not sure to what extent the investigation has gone ila all in all najua makampuni bado na watu wako ambao hawajatajwa . Wakamateni wachache muone mslulu utakavyo kuja juu .

Ndiyo nakubaliana nawe Mkandara kwamba Ngoma hii bado sana .
 
eti nilikuwa natumiwa? mpuuzi sana huyu na bora aje aseme ukweli tujue who/where is the money? akiwa mkweli wananchi tunaweza kumpa immunity maana atakuwa ametusaidia kuondoa mafisadi wengi sana
I agree, this man should come and show us the money. Ingawa system nzima imeoza bado niko positive kwamba tunaweza kupata pa kuanzia.
 
..HABARI ZA UHAKIKA NI KUWA ..HIZI PESA ZA BOT ..MUHUSIKA MKUU NI ROSTAM AZIZI ALIYEAMINIWA KUPEWA HIZI PESA KWA AJILI YA KUFINANCE MAMBO YA KAMATI YA UFUNDI CCM WAKATI WA UCHAGUZI...ALIPEWA BILIONI...40 HIZO MOJA KWA MOJA KUPITIA KWAKE...HAKUFIKISHA ZOTE KAMA MNAKUMBUKA WAKATI WA UCHAGUZI WALIKUWA WANASEMA PESA NYINGINE ANATOA ZAKE ZA MFUKONI..HII SI KWELI ..ALIKUWA NA HIZI PESA ..NA UKWELI NI KUWA PESA ZILIZOFIKA KWENYE KAMATI YA USHINDI HAZIZIDI BILIONI TANO.....

ZAIDI YA HAO WAFANYABIASHARA WALIOTUMIKA ..PESA NYINGINE ALIKUWA AKIKAA NAZO MVI....HAJATUMIA ZOTE...[ALIKUWA AKIGHARAMIA MAMBO YA PR ets]...nyingine zimepitia makampuni ya ccm [ie mwananchi,deep green ets ..kama ilivyokwishaongelewa na wengine hapa]

makampuni yote yanayowahusu hawa wandugu kwenye ripoti yamerukwa..

napenda mjue hakuna kitakachoendelea.....
 
...pia ifahamike kuwa kuna uwezekano mkubwa kwenye kamati ya ushindi ya jk...jk binafsi hakuwa akijua vyanzo vyote vya mapato.jk binafsi hana interest sana na pesa zaidi ya hobby zake binafsi.....hiyo iliacha mwanya kwa wapambe na kina mvi na rostam kutumia mwanya huu kujipatia pesa nyingi sana...zaidi ya bot,pesqa pia zilitoka makampuni ya madini na wawekezaji wakuu,wafanyabiashara wa ndani,nchi rafiki allied to jk[ie iran,drc ets]..ni pesa nyingi kuliko mnavyoweza kufikiria zilipatikana...

kuna uwezekano mkubwa pesa hizo wanalenga kujinufaisha nazo kibiashara...na pia as KING MAKERS watazitumia kufikia malengo ya kisiasa ya siku zijazo.....

kuna uwezekano mkubwa kadiri jk anavyogundua uchafu huu anazidi kuchanganyikiwa na marafiki zake asijue la kufanya......tukumbuke usia wa mwalimu kuwa tusije pata rais anayewekwa madarakani na majangili...anaweza kuwa mwema ..lakini awe na uwezo wa kuwakemea...je jk ana huo uwezo wa kuwakatalia hawa mafisadi..kama hawezi na yeye atajeuka fisadi!!???
 
Breaking News toka Iringa ni kwamba mganga wa kienyeji wa Balali anayejulikana kwa jina GM (nafupisha kutomharibia soko) amethibitisha kuwa ndugu Balali ni mzima wa afya na atarudi Tanzania kusafinya jina lake baada ya yeye Mganga kukamilisha shughuli za maandalizi ya ujio wake!
NB: This is not a Joke

Mambo ya mganga wa Jadi siyaingilii lakini NI KWELI kwamba Ballali anajiandaa kurudi (si kurudishwa) nchini wakati wowote na katika mambo mengine anataka achunguzwe kwa undani na afikishwe mahakamani ili huko ndio mambo yajulikane. Anataka mali zake zichunguzwe na zilinganishwe na kipato chake na pia kama mali zake zinalingana na hizo fedha zilizoibwa.
 
Mambo ya mganga wa Jadi siyaingilii lakini NI KWELI kwamba Ballali anajiandaa kurudi (si kurudishwa) nchini wakati wowote na katika mambo mengine anataka achunguzwe kwa undani na afikishwe mahakamani ili huko ndio mambo yajulikane. Anataka mali zake zichunguzwe na zilinganishwe na kipato chake na pia kama mali zake zinalingana na hizo fedha zilizoibwa.

Halisi, nimekusoma vyema ama? una maana Balali anataka arudi kumkoma nyani??

Hapa litakuwa limesanuka hasaaaaa!

Wasi wasi wangu ni je mahakama zetu zitatenda haki?? ama yatakuwa yale yale ya slayer Ditto??
 
Halisi, nimekusoma vyema ama? una maana Balali anataka arudi kumkoma nyani??

Hapa litakuwa limesanuka hasaaaaa!

Wasi wasi wangu ni je mahakama zetu zitatenda haki?? ama yatakuwa yale yale ya slayer Ditto??

Naamini kesho kuna gazeti moja litaandika kuhusu hizo taarifa za ujio wa Ballali... AMEKERWA SANA na KUTAJWA KWAKE PEKEE WAKATI WALIOCHOTA MGONGONI MWAKE WANAPETA
 
Mdogo wa Ballali ambaye anaishi naye Boston, Marekani ameliambia gazeti hili kuwa kaka yake ambaye sasa anaendelea vyema baada ya kushambuliwa na maradhi, anatarajia kuuweka ukweli wa kile alichoeleza kuwa uongo unaosambazwa dhidi yake.

100% Balali, hayupo Boston kwa hiyo hii artcile ni doomed kabla hata haijaanza, licha ya kuisha, aache ujinga wa kitoto arudi bongo na kujibu mashitaka, hayo maneno yake tumechoka nayo,

Siku zote alipokuwa bongo alikuwa akiongea yeye mwenyewe, sasa all over sudden anaongelewa na wengine, WHY? Arudi aongelee wizi wake kwanza asilete maneno ya wengine, hayo ya wengine atuachie wenyewe wananchi tutaamua, lakini fisadi kama yeye hawezi kutuamulia sisi wananchi what to do!

Arudi na kubeba msalaba wake kwanza!
 
Kuna ujumbe ulipelekwa jana kwa Balali.. subirini hii wiki inayokuja.. unapocheza chess hakikisha unamlinda King! CCM wamesahau hilo..
 
Mwanakijj samahan..thread ya ufisadi ATCL siioni...nimepost kidogo link ikaunganishwa kwa admin..vipi tena kulikoni...
 
usiwe na shaka angalia PM yako. Kwa kifupi na mimi niliuliza na jibu ni kuwa kuna mambo fulani ya kuangaliwa kwa haraka na uamuzi wa haraka ulitakiwa kuchukuliwa. Hata hivyo nimeambiwa itarudi haijafutwa imehifadhiwa tu temporarily.. na zitakaporudi nasikia zimeenda kuongeza kachumbari, limao na pilipili hoho..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom