Ballali aibuka na kujibu

Status
Not open for further replies.
Naona huyu jamaa labda bado hajapona vizuri, hawezi kusema ametumiwa. Yeye na hao anaodai wamemtumia wana tuhuma za kujibu. Kwa nini anakubali kutumiwa kufanya jambo ni la kuhujumu uchumi wa nchi? Ilitakiwa akatae wakati anaambiwa, kama alikubali basi anahusika moja kwa moja. Ataje tu hiyo timu yao.
 
Msing'oane meno bure. Mnataka kujua pesa za EPA zipo wapi? Nendeni Kunduchi Beach, Bahari Beach, Masaki, Makongo etc
 
Hivi kuna watu wanaamini Balali ni safi hakushiriki katika hili(kimawazo,kimaamuzi au kupokea chochote)?
 
Jana niliwaambia kwamba I was in touch na close people to the former Gavana mkadhani natania .Mzee atasema yaliyo msibu lakini chanzo kikubwa cha kusakamwa ni RA baada ya kuombwa returns za pesa za TISS na DeepGreen maana alizichukua yeye ndipo uchuro umeanza. Ngoma ni mbichi Balali wape watu wanayo stahili them kesi iende mahakamani hata Mkapa na JK hawatasalimika kwenye hili .
 
Hivi kuna watu wanaamini Balali ni safi hakushiriki katika hili(kimawazo,kimaamuzi au kupokea chochote)?

Icadon,

Issue ni hii perception ambayo kina Meghji CAG wanataka kuiweka mawazoni kuwa culprit ni Balali peke yake, ndiyo maana mimi binafsi ningependa Balali afanye what is called "plea bargain" na watanzania ili tumsamehe socially, ataje wenzake maanake yeye adhabu yake keshapewa ambayo ni just a slap on the wrist.

Ka kifupi he is the guy who opened the door wengine wakashindwa kujizuia inagwa hakuwaambia waibe.
 
Icadon,

Issue ni hii perception ambayo kina Meghji CAG wanataka kuiweka mawazoni kuwa culprit ni Balali peke yake, ndiyo maana mimi binafsi ningependa Balali afanye what is called "plea bargain" na watanzania ili tumsamehe socially, ataje wenzake maanake yeye adhabu yake keshapewa ambayo ni just a slap on the wrist.

Ka kifupi he is the guy who opened the door wengine wakashindwa kujizuia inagwa hakuwaambia waibe.

Now you are talking!
 
Pamoja na ushahidi wote juu ya Ballali kama JK na wenzake wako serious na hawadanganyi toto mbona hawafungui kesi ? Lakini hata kesi zao huwa zinaishia njiani maana Mahalu anapeta tu ilikuwa tuliza kelele ile na hii ni yale yale wote ni wezi .
 
Mtanzania:
Hapana. Jambazi mwenye kujua mambo anaponaswa na polisi habwabwaji hovyo kwa vitisho; kwani anazijua haki zake, na huyo polisi kama ni polisi kweli atamsomea haki zake kuwa "Lolote utakalolisema litatumika katika mahakama kukupa kbano." Huyo jambazi anayo haki ya kutosema kitu bila kuwepo kwa mwanasheria wake.

Kwanza mafia wenyewe hata huko Napoli? wameshindikana, kwa kung'ang'ania biashara za taka kiasi kwamba mji mzima umekuwa mlima wa taka!

Kama ni kweli Ballali anataka kujisafisha, ama kuzama na walaji wenzie, njia iliyo bora kwake ni kushirikiana na watu kama akina Dr. Slaa, wenye uchungu na mali za walalahoi. Ballali anatakiwa atoe kila habari na kitu alichonacho kama ushahidi utakaowezesha kuwanasa mafisadi wote waliomo.

K<alamu,

Tunaongelea vitu tofauti na sidhani kama inasaidia hii hoja. Ballali hawezi kwenda kwa Dr. Slaa, naamini hata wewe unajua hilo.

Hayo ya kusomewa haki ya mwenye makosa, hivi kuna hata haja ya kuyaandika? Maana kila mtu anajua, ninachosema mimi ni kwamba kama JK anataka kunasa wengi zaidi basi inabidi kumtumia Ballali maana yeye ndiye anajua ukweli wote.

Haina maana wamwachie huru lakini wanaweza kutaifisha kila kitu chacke na bado wakampa favours chache chache.

Vinginevyo wote tunataka haki itendeke ili wananchi wasiendelee kuibiwa, tunachotofautiana ni hiyo haki itapatikana vipi.
 
Msishangae yaliyomtokea Mh. Amina Chifupa, yakamjiri na Balali.

Hiyo RIPOTI anayosema ataitoa, hakuna kitu kama hicho kitatokea. Tanzania can not afford his big scandal, it wont allow him to add more to it

" RUMORS FLYING AROUND, JUST SPREADING IT"
 
Nyie watu wa ajabu sana. Yaani mnashabikia kitu kilicho obvious, kwamba Balali hakuwa peke yake.Kuna yale makampuni 22 na kuna wengine sisi hatujatajwa. What is news there? Hata hivyo, sijapata kuona mwizi anayesema yeye kweli ni mwizi na sijapata kuona mwizi kwenye mpango wa wezi wenzake akawa tayari kufa peke yake bila kutaja wenzake. Mbona mnajionyesha vilaza kwa kushabika jambo ambalo ni la kawaida na ambalo hata mtoto wa miaka minne angelitegemea.

Hakuna mtu wa ajabu hapa. Huu ufisadi hatujui ulianza lini, uliwahusisha akina nani, pesa zilizofisadiwa ziliwekwa wapi. Kwa hiyo Balalli kama akiongea na kutufumbua macho kuhusu hayo niliyoyaweka hapo juu basi kuna news ambazo siyo tu zinawahusu Watanzania bali hata jumuiya ya nchi za wafadhili.

Hakuna ukilaza wowote kutaka kujua details za ufisadi uliofanyika na hakuna mtu anayeweza kutoa details hizo vizuri kama Balalli ambaye alikuwa jikoni kama akiamua kuzungumza yote yaliyojiri katika ufisadi huo. Usidhani umesikia yote kuhusiana na ufisadi wa BOT, subira yavuta heri.
 
K<alamu,

Tunaongelea vitu tofauti na sidhani kama inasaidia hii hoja. Ballali hawezi kwenda kwa Dr. Slaa, naamini hata wewe unajua hilo.

Hayo ya kusomewa haki ya mwenye makosa, hivi kuna hata haja ya kuyaandika? Maana kila mtu anajua, ninachosema mimi ni kwamba kama JK anataka kunasa wengi zaidi basi inabidi kumtumia Ballali maana yeye ndiye anajua ukweli wote.

Haina maana wamwachie huru lakini wanaweza kutaifisha kila kitu chacke na bado wakampa favours chache chache.

Vinginevyo wote tunataka haki itendeke ili wananchi wasiendelee kuibiwa, tunachotofautiana ni hiyo haki itapatikana vipi.


Mtanzania:
Mimi ninakuelewa vizuri kabisa; na wala hatuongelei vitu tofauti hapa, unaongeza ubishi tu.

Ukweli ndio huo, polisi hana sababu ya kumbabaisha mtuhumiwa, kama mtuhumiwa anazifahamu haki zake.

Sikubaliani na wewe kuhusu Ballali kwenda kuomba fadhira za Kikwete.
 
....Halafu pamoja na yote haya-Richmond, Loliondo, Benki Kuu, Mkapa kufanya biashara ikulu, maisha duni, rada, Buzwagi na mengine mengi tu ambayo nikiamua kuyataja sitamaliza-lakini bado CCM inachaguliwa kwa vishindo na watu wanaimba nyimbo za kuisifu na kuipigia vigelele. Ujinga kama huu unapatikana Afrika peke yake na mifano iko wazi kabisa. Hakuna maelezo zaidi ya kwa nini ufisadi umekithiri na kushamiri zaidi ya watu kuwa wajinga.

kwanini inapatikana afrika pekee??
 
Nyani ngabu,
Hapa mkuu umenipa somo la mwaka huu 2008!..

Kwa nini ufisadi umekithiri na kushamiri zaidi ya watu kuwa wajinga.
 
(Kutoka gazeti la "Kulikoni" kama ilivyoahidiwa na Halisi)

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Daudi Ballali, ambaye alifukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete mapema mwezi huu amedai kuwa wanaompakazia wamemfanya mbuzi wa kafara.
Kwa mujibu wa watu walio karibu na Ballali, gavana huyo kasema katika utendaji wake wa kazi BoT kwa miaka tisa amefanya kazi kwa uaminifu mkubwa na kamwe hakuhusika na ufisadi unaotajwa sasa.

Mdogo wa Ballali ambaye anaishi naye Boston, Marekani ameliambia gazeti hili kuwa kaka yake ambaye sasa anaendelea vyema baada ya kushambuliwa na maradhi, anatarajia kuuweka ukweli wa kile alichoeleza kuwa uongo unaosambazwa dhidi yake.

Amesema Ballali anasikitishwa na namna baadhi ya viongozi wa serikali wanavyojikosha kuhusu ufisadi BoT wakati wakiutambua ukweli wa kile kilichotokea.

Ballali amedai kuwa kutokuwepo kwake nchini ndiko kumesababisha yeye kubebeshwa lawama zote kwa wizi huo wa BoT.

“Hata watu waliohusika na wengine wakishinikiza kulipwa kwa fedha kwa kampuni ambazo mimi sikuwa nazo shaka kwa kuwa zilikuwa na mkono wa wakubwa, nao wananilaumu,” amenukuliwa Ballali akisema.

Habari za uhakika zinaeleza kuwa Ballali ameapa kuwataja wote wanaompakazia kwa wizi huo, ambao ameueleza kuwa hakuutambua mara moja.

Gavana huyo amesema anao ushahidi wa kutosha kuthibitisha ‘kuagizwa’ na wale aliowaita wakubwa kulipa fedha kwa sababu ambazo hata hivyo alizieleza kuwa aliambiwa ni kwa ‘usalama wa taifa’

Ballali aliyeondoka nchini kwenda kutibiwa Marekani, baada ya kupata tiba Afrika Kusini kwa muda wa wiki tatu, amekuwa akipamba habari katika magazeti zikinukuu baadhi ya viongozi wa serikali wakieleza namna alivyohusika na ufisadi wa kutisha katika Benki Kuu ya Tanzania kupitia ulipaji wa madeni ya nje (EPA).

Zaidi ya bilioni 133/- zinaelezwa kuibwa kwa utaalamu mkubwa kwa kuhusisha kampuni 22, zikiwemo hewa, za ujanja ujanja na za kitapeli ambazo zilitumika kufanikisha wizi huo.

Ukaguzi uliofanywa na kampuni za ukaguzi wa hesabu zinazoheshimika; Ernst & Young na Delloite & Touche ndio uliogundua kuwepo kwa uozo huo wa kudidimiza uchumi na neema ya Watanzania baada ya kupewa kazi hiyo na serikali ya Rais Kikwete.

Kiasi hicho cha fedha bilioni 133/- kingetosha kujenga shule za sekondari 266 zenye madarasa maabara na samani za kisasa. Kiasi hicho pia kingeweza kuendesha wizara kama ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka 15 bila nyongeza ya bajeti yake ya sasa.

Wathamini wa majengo wanaeleza kuwa kiasi hicho cha fedha pia kingeweza kujenga majengo ya ghorofa zote yaliyoko Kariakoo, Mnazi Mmoja, na katikati ya jiji la Dar es Salaam na fedha nyingine kujenga barabara, kwa kiwango cha lami kuunganisha majengo hayo.


“Hakuna ubishi kuwa kaka hawezi kufanya jambo la kijinga namna ile, hana tamaa na wala siyo mwizi, ndiyo maana amekuwa akiaminiwa na taasisi kubwa za fedha za kimataifa ambako analipwa vizuri kwa kazi za ushauri, iweje leo azuliwe uongo na kuchafuliwa jina, lazima atasema kuukanusha,” alisema mdogo wake huyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini kwa sasa.


Mdogo huyo wa Ballali ambaye mwaka jana alikuwa hapa nchini amesema mshahara wa kaka yake unamtosha kufanya mambo makubwa na ya maendeleo bila hata kuiba mali ya umma.

“Huwezi kuamini, kaka Daudi hapendi mtu anayepindisha sheria, na huo ndio umekuwa msimamo wake mara zote katika maisha yake na hata kumfikisha hapo alipo, ni mwaminifu sana. Hizo pesa kama zimeibwa BoT, basi yeye siyo mfaidi, bali zimewafaidisha wengine,” aliongeza kwa sauti ya kushangaa na kusikitika wakati akizungumza na gazeti hili.

Inaelezwa kuwa mshahara wa Ballali, pamoja na kuwa na magari mawili ya serikali aliyokuwa akitumia nyumbani na ofisini, kupewa nyumba iliyo na samani zote na wafanyakazi, alikuwa akilipwa mshahara wa milioni 25/- kila mwezi.

Ballali amefanya kazi Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa zaidi ya miaka 25 akiwa Washington, Marekani.

Mbali na kufanya kazi IMF na Benki ya Dunia, Ballali anasifika kwa kushauri na kufanikisha uimara wa uchumi wa baadhi ya nchi za dunia ya tatu, ikiwemo Ghana ambayo inang’ara kwa uimara wa uchumi wake.

Kufuatia wasiwasi wa usalama wa maisha yake, mdogo wa Ballali amesema kaka yake amelazimika kuishi katika makazi ambayo hayafahamiki kwa wengi kwani wanaompakazia wanaweza kumdhuru kwa lengo la kuficha kile atakachokieleza kwa umma.

“Hivi sasa, kaka anapumzika mahali wanakokujua wachache, kwani kuna hatari ya kudhuriwa na watu wanaoendelea kumpakazia huku wakiutambua ukweli kuwa walikuwa wahusika wakuu wa kutolewa kwa fedha hizo za BoT kwa njia ambazo sasa hata yeye anatambua hazikuwa halali,” amesema mdogo huyo wa Ballali.

Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza ni lini Ballali atarejea nchini kwa ajili ya kuweka bayana kile anachoamini ni ukweli wa shauri hilo ambalo limekuwa gumzo ndani na nje ya Tanzania, nchi yenye idadi kubwa ya watu masikini, wengi wakishindwa hata kumudu mlo wa siku moja.

Ballali aliteuliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa kushika wadhifa huo kwa mkataba wa miaka 10 na kurithishwa kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye alimfukuza kazi bada ya kupata taarifa ya ukaguzi uliogundua kuibwa kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Katika kipindi hicho, akiwa amedumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka tisa, Ballali alikuwa akiripoti kwa Basil Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha wakati wa Mkapa na Zakhia Meghji ambaye ni Waziri wa Fedha wa sasa.
 
Napata shaka na utetezi unaoendelea hapa.
kama alijua na anajua kuwa yeye ni msafi kwa nini asilipuke na majina ya walimlazimisha aende kinyume na utaratibu? kwa nini ajibu kwa jeuri kuwa tuhuma hazikuwa na ukweli wowote na zilikuwa za kutungwa??

nina hasira ya kukosa elimu eti kisa bodi ya mikopo haina hela kumbe zimechukuliwa na watashi wa kisiasa....

Liwalo na liwe mafisadi watafuchuka na ninamwombea balali afya njema ili aweze kutoa taarifa adhimu kuhusu WIZI wa mali yetu (Watanzania)
 
Excerpt of letter drafted by Ballali that the deceived Zakia Meghji signed:



Deloitte & Touche
Private Bag No X6
Gallo Manor, 2052
Johannesburg
South Africa

PAYMENTS TO KAGODA AGRICULTURE LIMITED

I would like to confirm the following with regard to your current audit of the Bank of Tanzania for the year ended 30th June 2006

As you well know all Sovereign Governments do have secrets as well as the need to undertake and finance expenditure discreetly. Accordingly, as has been extensively discussed with you, the payments of US$ 30,222,658.82 to Kagoda Agriculture Limited by the Bank of Tanzania were authorized by the Government and used by the Government to finance sensitive Government expenditure. It was necessary to take this course of action to maintain the necessary confidentiality.

I would like to confirm that there are no other similar transactions of funds paid from the Bank of Tanzania during the period of 1st July 2005 to 30th June 2006. Indeed, it is very rare that the Government has to face the need for this level of secrecy and it only occurs when the national interest demands it.

I would like to confirm that the course of action taken by the Government in the circumstances is in line with the Bank of Tanzania.

regards,

Zakia hamdani Meghji (MP)
MINISTER FOR FINANCE


below is part of the letter to rescind the above letter



I would like to refer to my letter of even reference dated 15th of September 2006 on the subject above.

It has come to my notice that the letter I wrote to you, referred to above, which was based on advice of, and drafted by, the Governor of the Bank of Tanzania was issued by mistake. I signed the letter because I trusted the Governor. It has been established that the payments to Kagoda Agriculture Limited were not related to Government Expenditure.

In the circumstances, my letter dated 5th of September, 2006 is forthwith rescinded.

Regards,

Zakia hamdani Meghji (MP)
MINISTER FOR FINANCE

CC. Governor
Bank of Tanzania
P.O. Box 2939
Dar es Salaam
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom