balaaa balaaa

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,347
11,610
UKIMWI na mzunguko wake:
Kijana wa Kitanzania aishiye huko Marekani alimpigia simu mama yake.
Maongezi yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Kijana: Mama, nina virusi vya UKIMWI!
Mama: Mwanangu, ninakusihi, ninakusihi, ninakusihi sana, usirudi nyumbani kabisa.
... Kijana: Kwa nini mama?
Mama: Endapo utarudi nyumbani, mkeo pia ataathirika. Mkeo akiathirika
atamwathiri pia mdogo wako. Mdogo wako akishaathirika atamwathiri pia msichana wetu wa kazi. Ujuwe mwanangu, msichana wetu wa kazi naye
atamwathiri pia baba yako. Baba yako naye atamwathiri mdogo wangu, mdogo
wangu atamwathiri mumewe ambaye naye ataniathiri mimi pia. Mimi nikishaathirika nitamwathiri mtunza bustani wetu. Mtunza bustani wetu
akishaukwaa atamwambukiza pia mdogo wako wa kike. Mdogo wako akishaupata
tu, ujuwe kijiji kizima kimeupata!
Mwanangu, kwa jina la Mungu, tafadhali, tafadhali kiokoe kijiji chetu.
Ninakusihi tena mwanangu, USIRUDI TENA NYUMBANI
 
Duh! Hii ni kama ile riwaya ya KUSADIKIKA!
 
Hongera Smile kwa visa na stori za moto.Vyote ulivyovileta vilinigusa sana lakini hiki cha ukimwi ni zaidi, ndo maana nachangia. Mzunguko wa iukimwi ni mkali sana, unaingia hata makanisani.
Nasubiri mchapo mwingine kutoka kwenye keyboard yako, maana umeshakuwa fundi wa stori kiasi cha kumfikia Baba Cantalisia; Mzee Mtambuzi.
 
Ama kweli ni balaa, inabidi abaki huko alipo kuokoa kijiji
 
Back
Top Bottom