Balaa kubwa: Baada ya kutimliwa na JK; Mkulo, Maige kortini

Unataka kusema kwamba wakina Mramba wao au serikali inapenda kesi zisiishe?

Mbona kuna wananchi wa kawaida kesi zao zipo miaka 10 haziishi? kwanini wakina Mramba kesi iishe fasta wao kama wakina nani?


Kesi zao zinatakiwa ziishe haraka ili wananchi waone kwamba serekali ina nia ya kushughulukia janga la rushwa/ufisadi. Yote tisa kumi ni kwamba haki itendeke regardless of how quickly or not, kuna mdau kasema hapo juu 'It matters how it ends'. But as a patriot I would feel a heck lot better if the government acted swiftly and fairly on such high profile cases, that will go along way in deterring potential offenders more than any awareness campaign ever would. Then again that is all dependent on if the 'Government' is serious about getting rid of corruption, the keyword being 'if'.
 
sheria ni msumeno inakata kotekote

wangeachwa pia tungelalamika mahakama itatupa jibu juu ya tuhuma dhidi yao

Acha porojo wewe, sheria zetu zina maeneo yakuwa msumeno na maeneo yakuwa butu, kwa ujinga wa watawala wetu chini ya mfumo mbovu wa serikali na chama tawala usishangae mahakama ikatumika kuwasafisha. Kwani hushangai Prof Mahalu anatetewa na rais mstaafu lakini kashtakiwa na serikali, utafikiri kesi ilifunguliwa na cdm sasa serikali inamtetea!
 
Hawa wanachezea akili zetu tu, hakuna lolote hapo. Andrew Chenge ambaye ushahidi upo hadharani mbona bado anatesa tu? Si ajabu tukamsikia Jk akimteua kuongoza taasisi fulani.
 
Hao watu wana mali nyingi za wizi,mkulo ni fisadi mali zake nyingi amezificha kwa mfanyabiashara al-sayeed wa morogoro,mkulo kwa kumtumia al-sayeed amenunua yutong nne ambazo zinafanya kazi morogoro,pia anashirikiana na tajiri wa kilosa(babylon) kuingiza pesa chafu katika majengo,majengo mengi ya kilosa mapya mapya ni ya mkulo.
Hawa watu wachunguzwe kwa makini wana mali nyingi sana wametuibia kama serikali kupitia DPP wakipotezea nguvu ya umma itawashinda tu,aluta continua
 
Mimi kwa kumbukumbu zangu huyu Mkulo aliwahi kustaafishwa kwa manufaa ya umma katika awamu ya Mkapa. Sasa sijui ****** alitoa wapi mawazo ya kumpa uwaziri wa fedha ikiwa ukurugenzi tu wa NSSF (kama si PPF) ulimshinda
 
Kwa nini washitakiwe wawili tu? Mbona Mamvi na Rost Tamu, na wale wa EPA ambao bado uchunguzi unaendelea, na wengine wengi kibao. Kwani Maige alikula peke yake? Wote wenye makosa wapelekwe mahakamani ili wasafishwe tupat kuwaamini.
 
Maigizo hayaishi nchi hii!

Ha ha ha! Umesema sawa kabisa, kesi zitatajwa kama zile za Mramba na Yona lakini hamna ushaidi wa kutosha. JK, DPP & co wanajua wanachokifanya. Baadae watasema tumewashtaki mahakama imewasafisha. In short wanachofanya nikuwasafisha sasa- Changa la macho kwa watanzania. Ile ya Yona na Mramba itaisha soon - habari za uhakika ni kwamba hamna ushaidi wakutosha.
 
Huo ni usanii tu, kwani kina Mramba na wenzake miaka mingapi kesi inasikilizwa? Ni kusubiri tu upepo upite watu waendelee kula kuku. Na wezi wa mali ya umma Tz. Wako wengi na wanafahamika lakini hawaguswi.

Ha ha! DPP ameomba aongezewe muda akusanye ushahidi (evidence hazijajikamilisha).
 
Hakuna kitu kama hicho ndani ya utawala wa CCM kwani mali ya nchi hii imeanza kutafunwa siku nyingi ususani baada ya Baba wa Taifa J.K.Nyerere kung'atuka wezi wanajulikana lakini hadi sasa nani amekwisha filisiwa? amekwisha shitakiwa na kuhukumiwa? amekwisha pewa karipio adharani na mkuu wa nchi? vyote hivyo hakuna tusitegemee miujiza kutokea. ikishindikana wote hao tutasikia kama ya BALALI
 
jamani mie naona hapa hakuna balaa lolote kama post inavyodai, uliyepost huu uzi unataka kututangazia kuwa una blog yako "gumzo la jiji", please tupe source makini
 
Ha ha
ha! Umesema sawa kabisa, kesi zitatajwa kama zile za Mramba na Yona
lakini hamna ushaidi wa kutosha. JK, DPP & co wanajua
wanachokifanya. Baadae watasema tumewashtaki mahakama imewasafisha. In
short wanachofanya nikuwasafisha sasa- Changa la macho kwa
watanzania.
Ile ya Yona na Mramba itaisha soon - habari za
uhakika ni kwamba hamna ushaidi wakutosha.

wait and see. haitaisha kirahisi hivyo. watakutwa na kesi ya kujibu.
 
Kabla ya Kikwete uliwahi zisikia hizi kesi?

Kikwete anashirikiana na nani kuitafuna hii nchi, tunaomba uje kutowa ushahidi tunataka kuwapeleka mahakamani wote wanaohusika na msiba huu, jee upo tayari kujitokeza kutoa ushahidi? maana inaonesha unajuwa mengi sana.

Hapa kwenye RED, ina maana tokea ishu za EPA, KAGODA, ela za SHIMBO, ishu ya RADA, ishu ya JAILO, ela za STIMULAZ, ela za PEMBEJEO etc, bado tu hamjapata "ushahidi" wa kuwapeleka hawa "rafiki zenu" mahakamani? Kweli magamba yenu ni magumu... okay ni PM ili nikupe ushahidi wewe gamba la kenge...
 
Kiini macho!
MARA baada ya Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki iliyopita kulisuka upya baraza lake la mawaziri kwa kuwatosa mawaziri sita kati ya wanane waliokuwa wametajwa kwa kashfa mbalimbali katika ripoti ya Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), mawaziri wawili wamo mbioni kushitakiwa kortini. Habari kutoka ndani ya serikali zinasema tayari maofisa wa serikali wanaandaa makabrasha ya kuwafikisha mahakamani maofisa kadhaa akiwemo aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. MUSTAFA MKULO Mkulo ndiye aliyekuwa waziri wa kwanza kutakiwa na wabunge ajiuzulu kwa kutuhumiwa kuvunja Bodi ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) ili kuficha tuhuma zake ikiwamo uuzaji wa kiwanja Na.10 kwa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL). Ukaguzi wa CAG ulibaini kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wizara ya Fedha zilihusika moja kwa moja katika uuzwaji wa kiwanja hicho Na.10 kilichopo kando ya Barabara ya Nyerere bila kuishirikisha bodi ya CHC. Aidha, CAG alibaini kuwapo kwa matatizo katika hati ya madai ya Shilingi bilioni 2.4 kutoka katika Kampuni ya DRTC kama gharama za ulinzi na tozo la matumizi ya barabara ya kuingilia kwenye Kiwanja Na.192 kando ya Barabara ya Nyerere. Upungufu pia ulionekana kwenye uuzwaji wa jengo la Kampuni ya Tanzania Motors (TMC) lililopo kiwanja Na.24 kilichopo katika eneo la viwanda la Chang’ombe kwa Kampuni ya Maungu Seed. EZEKIEL MAIGE Maige akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ripoti ya CAG ilieleza kuwa ofisi yake ilipoteza Shilingi 874,853,564 baada ya kufanya uamuzi wa upendeleo wa kutoa kiwango cha chini cha mrahaba kwa mauzo ya misitu. Katika kipindi cha ukaguzi wa hesabu za Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (Tanapa) ilibainika kuwa shirika liliingia katika mkataba na Kampuni ya CATS Tanzania LTD unaohusiana na matengenezo ya kawaida, ufungaji wa vifaa vya mawasiliano na vifaa vingine katika mkataba wa jumla ya dola milioni moja za Marekani. Alishutumiwa kwa kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji, ugawaji ambao inadaiwa ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwa ni pamoja na kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha ni vitalu vipi walivyopewa. Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili ilieleza kuwa kampuni 16 zilizopewa vitalu hivyo hazikuomba na kwamba vitalu hivyo vilikuwa vya daraja la kwanza na la pili. Mbali na tuhuma hizo, Maige hivi karibuni alidaiwa kununua nyumba kwa Dola za Marekani 700,000 iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tuhuma ambazo alizipinga na kusema kuwa nyumba hiyo ameinunua kwa Dola 410,000, (sawa na zaidi ya shilingi milioni 600 za Kitanzania). Habari za ndani kutoka serikalini zilizotufikia zinasema mara baada ya Rais Kikwete kutoa tamko la wahusika wa ubadhirifu huo ‘washughulikiwe’, tayari nyaraka mbalimbali zimeanza kushughulikiwa na vyombo vya dola ili kuona nani aliiba na nani hahusiki. Waliokuwa mawaziri na kutemwa nao wanamulikwa na vyombo vya sheria. KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA BAADA YA KUTIMLIWA NA JK MKULO, MAIGE KORTINIGUMZO LA JIJI
 
Mchezo wa kuigiza...nani atawapeleka hawa mahakamani, Takukuru hii hii?
 
Back
Top Bottom