BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.

Huwezi kufananisha Tanzania na Uingereza, Misri, au Israel. Wamepevuka kifikra na nchi kama yetu ni rahisi sana raia kukimbilia kwenye vurugu za kidini au kikabila. Nawashauri wenzetu watumie muda mwingi kuzungumzia maendeleo ya kuwakwamua waumini wao kupambana na adui ujinga na umaskini.
 
tanzania bana, as if dini zipo mbili tu nchi hii.....

Wakihesabu hivyo wasirudi kusema wameonewa/wamehesabiwa vibaya
 
Tukimaliza kuhesabu Waislam, watasema tuhesabu na wasiosali swala tano, wasiofunga mwezi Mtukufu, wasiovaa hijab, wenye wake wawili, n.k. Hii ni kwa sababu ikiwa mtu unang'ang'ania kipengele cha dini katika sensa, ina maana unataka kufanya mipango fulani iendane na jinsi watu walivyo waaminifu katika dini yao.

Jamani hawa wananifanya nijione siko Tanzania!

Hoja wa dini fulani kuwa inataja idadi ya waumini wake ni ya kitoto kwa sababu kuna baadhi ya madhehebu yana utaratibu wake wa kufanya sensa ya waumini wake.

Kamanda hapo umenena hawa jamaa wanataka kuonewa huruma kila mahali ............ saa zingine hawasomi ila wanataka kufaulu wawe sawa ........... sasa hebu tujiulize swali la msingi kila dini ikitoa masharti kwa serikali je kutakuwa na nchi hapo.................... hawa jamaa mi nadhani wakae chini watafakari kwa kina maana sasa niaamini hata uamsho znz wanawaunga mkono hawa jamaa.
 
Ninatumaini kuwa maamuzi ya Waislamu yataheshimiwa katika nchi ya Kidemokrasia kama Tanzania.

Hivi kukataa kuhesabiwa si kosa la jinai? Kwa serikali makini ingekuwa imeshatoa tamko kuhadharisha hata kabla ya wanaharakati kuanza porojo zao.
 
Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.

hiyo 65% bila shaka ilikuwa Zanzibar...kwa bara sahau ndugu yangu au umeamua kutwist takwimu. Mwaka huo uislamu ulikuwa pwani tu...hata sasa kuna baadhi ya mikoa uislamu uko mijini tu tena miji ya mikoa na wilaya. Nenda Ifakara mjini kwa mfano, misikiti haizidi mitano. Mikoa kama rukwa, katavi uislamu uko kiwango cha chini sana pengine chini ya 3%

TATIZO LENU
1-Mazingira ya zanzibar kidini mnadhani ni uhalisia wa Tanzania yote. Sensa ya udini ikifanyika hata hapa dar matokeo yake yatawashangaza.
2-Mnapenda kupayuka na kupiga kelele mno bila kufanya utafiti na uhalisia wa hali halisi.
3-Mkurugenzi wa Takwimu na Waziri wa mipango ni waislamu kwa nini wanapinga suala la udini? wanajua uhalisia wa population kidini hapa nchini, wafuateni muwaulize kwa siri watawaambia ukweli. Pia tembeeni vijijini mikoa yote ili muone na mjue namna uislamu ulivyo mgeni katika jamii za makabila mengi hapa nchini.
 
Hivi katika nchi hii, dini zinazotambulika kisheria ni uislamu na ukristo? kwa nini dini nyingine hazizungmziwi hapa,mfano dini za kimila sijasikia zikizungumziwa kabisa.

Niliwahi kwenda Polisi, katika kuandikisha malezo yangu nikaulizwa dini yangu, nikajibu kuwa sina dini, mimi ni mpagani, lakini yule askari alilazimisha kwamba lazima nina dini, baada ya kubishana sana akaniuliza dini ya wazazi wangu nikamwambia nao hawana dini, yule askari akasema haiwezekani na mwishowe akanipachika dini ambayo si yangu...

Mtambuzi,

Kwa kweli mi huwa nashangazwa sana, manake katika nchi hii dini ni uislam na ukristo tu, sie wengine tusioamini katika dini hizi hata huwa hatuongelewi Kama tupo. Niliwahi kwenda kampuni moja receptionist alikuwa dada mmoja wa kiarabu kavaa nikab. Sasa akaniuliza dini katika maongezi, nikamwambia pia sina dini, alikataa kabisa kuwa eti haiwezekani.

Anyway sijui kwa nini watu wagombane kutaka tu kujua wao wako wengi kiasi gani badala ya kuhangaikia mambo ya msingi katika maisha yetu. Na ajabu popote pale duniani ni waislamu na wakristo tu ndio wanaleta migogoro kwa watu wengine, kugombania ipi Kati Yao ni dini kubwa!
 
Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.

Kila nchi inafanya mambo kutokana na mazingira yake. Tanzania haiwezi kuendesha mambo kama Uingereza, Misri, Israel au hata Kenya tukasalimika. Tuna kundi kubwa sana la watanzania ambao wanaburuzwa na kundi/makundi ya watu kwa maslahi yao binafsi. Na tukiruhusu mambo kama udini, ukabila kwenye sensa tunaweza kujiingiza kwenye historia nyingine, historia iliyojaa huzuni.

Kelele za Sheikh Ponda na sasa BAKWATA zina msukumo wa mbali, msukumo wa wanasiasa wanaotaka kuwekeza kwenye makundi fulani fulani ili wafanikishe azma zao. Tanzania hadi sasa hivi haina dini, serikali haifanyi mipango yake kwa kuangalia dini na ndio maana hata kwenye mawizara hutasikia wanasema tunajenga barabarana kwa kuzingatia dini etc. Hata leo hii watanzania wote wakaamua kuachana na dini zao na kuwa wapagani bado serikali haitabadili mipango yake maana hakuna madhara yoyote.

Lakini kama hatukuwa makini, hiki wanachopigania BAKWATA kitatumaliza wote (waislam na wasio waislam). Wanasiasa wa sasa wanaonekana kuiga mtindo wa Kenya wa kuwekeza kwenye makundi watataka sana kujua dini fulani ina watu wangapi na ingewezekana wangetaka pia kujua kabila gani lina watu wangapi halafu waanze kuwekeza huko.

Siungi mkono kodi yangu kutumika kuhesabu dini au kabila. Lazima tufike mahali tuelezane ukweli. Na ni bahati mbaya sana sasa hivi ina ombwe la uongozi, madai kama haya ya BAKWATA yangemelizwa na BAKWATA wenyewe. Wapitie kila msikiti ili kujua idadi ya waumini wao. Najua kuna madhehebu ya kikristo wamekuwa wanafanya hivyo kila mwaka kujua wana waumini kiasi gani, na hata siku moja hutasikia wanasimama majukwaani wakidai serikali iwafanyie hiyo kazi. Haya ni mambo ya imani na yabakie huko huko kwa hao wanaofuata imani husika.
 
It is very true kwamba kila mtu au kundi la watu lina haki ya kutoa maoni na maoni yao kusikilizwa, hii ni haki ya kikatiba, na kama haki hii itavujwa, wanayo nafasi ya kuidai through art 30 of the Constitution of URT.

Ni muhimu sana kujua idadi ya wananchi ili tujue mipango tunaipangaje, tunaanzia wapi tunaishia wapi. So to the issue of idadi ya watu katika dini fulani. Ili kwa namna moja au nyingine taasisi hizi zijue zinawaumini wangapi, nao wapange mipango yao ya kimaendeleo kwa watu wao.

Ila for the case at hand, National Census caries with itself PUBLIC INTERESTS, and it is solely for the purpose of the entire nation. Inclusion of domination information, will serve what a purpose? Will it be amongst the things leading to the success of the core motive of Census? Is it for the public interests? Or it is just to satisfy a group of people? Without regarding whether they are majority or minority?

I am afraid not!

In my own opinion: Inclusion of denomination information is quite okey and fine, but some of us may use it as a loop hole to raise issues of majority ruling, influencing and preferred and the minority serving.
BAKWATA reasoning is very very correct, but not at this issue.
Tanzania is a non-secular state. May if we want to change it to a secular, denomination will serve a great purpose thereto.

My take: Naomba tuhesabiwe kama watanzania, ufungamano wa aina yoyote usio na maslahi ya kitaifa wala usio na mchango wowote katika lengo mahususi la sensa usiwepo.

God bless Tanzania.
 
Mchambuzi,

Kwa kweli mi huwa nashangazwa sana, manake katika nchi hii dini ni uislam na ukristo tu, sie wengine tusioamini katika dini hizi hata huwa hatuongelewi Kama tupo. Niliwahi kwenda kampuni moja receptionist alikuwa dada mmoja wa kiarabu kavaa nikab. Sasa akaniuliza dini katika maongezi, nikamwambia pia sina dini, alikataa kabisa kuwa eti haiwezekani.

Anyway sijui kwa nini watu wagombane kutaka tu kujua wao wako wengi kiasi gani badala ya kuhangaikia mambo ya msingi katika maisha yetu. Na ajabu popote pale duniani ni waislamu na wakristo tu ndio wanaleta migogoro kwa watu wengine, kugombania ipi Kati Yao ni dini kubwa!
Correction...ni dini moja tu inayoleta migogoro duniani...dini yenye kutoa matamko tunayojadili hapa...!
 
Ndio maana mimi niliamua kuwa MPAGANI..........

Na huwezi kuamini wapagani ndio wanaishi maisha ambayo vitabu vya hao wenye dini vinataka...wao wenye dini wamebaki kueneza chuki dhidi Yao na kuuana. Ni nadra kusikia wapagani wameuleta vurugu za kidini, kila siku tunasikia waislamu na wakristo katika fujo.
 
A massive failure to a failed state leader.... ukiona wananchi wako wanashindwa hata kuamini serikali kwenye sensa basi jua huna mamlaka ya kutawala

Na hasa kwa chama ambacho kiko tayari kukubaliana na kila upuuzi mradi tu kwa kukubali huo upuuzi kina hakika ya kuendelea kuwa madarakani.
 
Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.

kWENYE HIZO NCHI KUNA AGENDA KUBWA YA KUDHIBITI KUNDI FULANI LA DINI. MBONA WOTE TUNAJUA HILO
 
Kama BAKWATA wamefikia hatua ya kugomea sensa simply because kipengele cha dini hakijawekwa,ninashawishika kuamini kuwa kina umuhimu kwao. Kama mimi ningekuwa ni serikali ningewaambia BAKWATA hivi, LETENI SABABU ZA MSINGI ZITAKAZOIFANYA SERIKALI IINGIZE KIPENGELE CHA DINI KWENYE SENSA. Hapo ndipo tungeona uwezo wa watu kufikiri.

Wazo la busara: Ukiona mtu analalamika kila wakati na kukimbilia kufanya vurugu/fujo kama njia mbadala ya kutatua matatizo yake badala ya kujenga hoja zenye maana na ushawishi,mfanyie tathmini kwenye mambo yake mwenyewe.
 
It is very true kwamba kila mtu au kundi la watu lina haki ya kutoa maoni na maoni yao kusikilizwa, hii ni haki ya kikatiba, na kama haki hii itavujwa, wanayo nafasi ya kuidai through art 30 of the Constitution of URT.

Ni muhimu sana kujua idadi ya wananchi ili tujue mipango tunaipangaje, tunaanzia wapi tunaishia wapi. So to the issue of idadi ya watu katika dini fulani. Ili kwa namna moja au nyingine taasisi hizi zijue zinawaumini wangapi, nao wapange mipango yao ya kimaendeleo kwa watu wao.

Ila for the case at hand, National Census caries with itself PUBLIC INTERESTS, and it is solely for the purpose of the entire nation. Inclusion of domination information, will serve what a purpose? Will it be amongst the things leading to the success of the core motive of Census? Is it for the public interests? Or it is just to satisfy a group of people? Without regarding whether they are majority or minority?

I am afraid not!

In my own opinion: Inclusion of denomination information is quite okey and fine, but some of us may use it as a loop hole to raise issues of majority ruling, influencing and preferred and the minority serving.
BAKWATA reasoning is very very correct, but not at this issue.
Tanzania is a non-secular state. May if we want to change it to a secular, denomination will serve a great purpose thereto.

My take: Naomba tuhesabiwe kama watanzania, ufungamano wa aina yoyote usio na maslahi ya kitaifa wala usio na mchango wowote katika lengo mahususi la sensa usiwepo.

God bless Tanzania.

Mkuu hapo kwenye red, huu ni uzembe ikiwa taasis kubwa kama BAKWATA haijui idadi kamili ya waumini wake. Matokeo ya sensa ni ya jumla jumla. Haitoi uhalisia wa imani za watu, siju kama hilo hawajaliona.
 
Basi hakuna tatizo Bakwata kujitoa, Serikali wafanye sensa yao.

Wewe ni shia au suni maana hao si wamoja pia katika mipango yao kama ilivyo kwa wakristo pia ambapo kuna waanglikani, wakatoliki n.k. Inayofanya sensa ni serikali sasa wanadini wanataka takwimu za nini. Tatizo la Waislamu ni utawala uliogawanyika ambapo kupata idadi hao kwa sensa yao wenyewe ni kikwazo. Mfano. Utakuta shehe wa Tabora anaitwa kuja kufungisha ndoa hapa Lindi lakini shehe wa hapa Lindi hajui na hana taarifa yoyote. so, kumbukumbu ya msikiti wa hapa Jirani hawana records. Ni kukosa busara kwa Bakwata kutokuwa na mipango yake ya kujijua yenyewe na watu wake bali kutegemea vya bure toka serikalini. Yawezekana serikali ikawakubalia but matokeo yakaja kuwa wakristo wako wengi na hapo waislamu watakuja na hoja ingine ya kuwa takwimu zimechakachuliwa na hivyo NBS iundwe upya ili na dini zishiriki. Waislamu ni tatizo kubwa mno!!!
 
Huyo anayewatia ujinga watanzania kawapata kweli......
Mnapigania dini huku madini yenu yanasombwa...........
Mnabishania dini huku maliasili zinabebwa......

Kweli ngozi nyeusi inasikitisha............

Na zaidi wanabishania kuhusu Mungu wa kiarabu, kizungu na kiisrael...
 
Back
Top Bottom