BAKWATA Yapinga maandamano ya Waislam tarehe 23 Dec 20011

Mkuu hakuna wakati wa msiba mmoja.. Misiba inapotokea ni ktk mipango ya Mungu na mnazika na kuendelea na maisha. Maandamano lazima yawepo kwa sababu tunaitaka Tanzania isiyokuwa na upendeleo wala kuomba maana uongozi wa nchi ni majukumu tulowapa sisi wananchi na sio wananchi wakaombe Ikulu, laa hasha -Hatudanganyiki.

Muafaka wa MoU ufutwe na sheria ya katiba iundwe kwa ushirika wowote baina ya serikali na shule ama Hospital lakini kusiwepo kabisa na kukabidhi swala la Elimu na Afya mashirika binafsi bali mashirika haya yaifanye kazi chini ya sheria na serikali itayasaidia iwezavyo. Serikali haiwezi kuunda wizara ya mseto na kanisa halafu watu mnashindwa kuona tatizo ati kwa sababu tunasaidiwa. Basi ni bora tuunde serikali nzima ya mseto na Marekani, UK au Canada ijulikane kabisa tunatawaliwa...

Kwa muafaka kama huu mnawaona CUF ni CCM - B, sasa mnashindwa kipi kuiona CCM imeshikwa na kanisa kwa kuweka muafaka ambao unakabidhi huduma za Afya na Elimu wizara ya mseto baina ya serikali na kanisa.

je? Maandamano ni solution ya kila tatizo? Kuandamana cku hizi imekuwa ni fashion cku hizi. Cpingi maandamano, maandamano ya wepo, ila si kila tatizo ni kuandamana.
 
Back
Top Bottom