Elections 2010 Bakwata, TEC, CCT - mwende na huko pia

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
viongozi wa dini zetu wameanza ziara za kutembelea vyama vya siasa wakiwa na ujumbe wa amani na wakubaliane na kuvitaka vyama vikubaliane na matokeo ya uchaguzi,rai yangu ni hao viongozi wetu wa dini wajue kukubali matokeo ni matokeo ya kuwepo na uwanja huru wa ushindani wa kisiasa,naomba wakimalizana na ziara ya vyama vya siasa waende kwa msajili wa vyama ndg tendwa na wamkemee na kauli zake utata na zinazoashiria uwezokano wa uvunjifu wa amani,kisha waende kwa jaji makame na ofisi yake wanaokaa kimya huku mgombea wa chama tawala akivunja sheria ya uchaguzi huku wao wakiwa kimya,kwa kufanya hivyo hao viongozi wa dini watakuwa wamelisaidia taifa
 
Kwa hiyo tukubali hata tukiona wizi wa kura macho makavu,mchana kweupe!lo hilo hatuwezi kukubaliana. Mimi nimefikia mahali siwaamini hata viongozi wengine wa dini.wanaweza wakawa hata mawakala wa vyama. Viongozi wa dini bakini makanisani na misikitini wafanye kazi zao. Naamini mafisadi watakuwa wamejiandaa kupita kwa gharama yoyote,unafikiri hayo yatavumilika? Kazi ya viongozi wetu wa dini ni kuwaasa vyama vyote wasichakachue matokeo ya uchaguzi,kwani watasabisha machafuko.Kitu wanachotaka ni kutufundisha woga,hatudanganyiki.
 
viongozi wa dini zetu wameanza ziara za kutembelea vyama vya siasa wakiwa na ujumbe wa amani na wakubaliane na kuvitaka vyama vikubaliane na matokeo ya uchaguzi,rai yangu ni hao viongozi wetu wa dini wajue kukubali matokeo ni matokeo ya kuwepo na uwanja huru wa ushindani wa kisiasa,naomba wakimalizana na ziara ya vyama vya siasa waende kwa msajili wa vyama ndg tendwa na wamkemee na kauli zake utata na zinazoashiria uwezokano wa uvunjifu wa amani,kisha waende kwa jaji makame na ofisi yake wanaokaa kimya huku mgombea wa chama tawala akivunja sheria ya uchaguzi huku wao wakiwa kimya,kwa kufanya hivyo hao viongozi wa dini watakuwa wamelisaidia taifa

Kwa imani yangu sala zinatosha kabisa kumwomba Mungu ili tuwe na amani badala ya kuzulula kwenye vyama vya siasa na kuacha kuhubiri na kutoa mawaidha kwenye nyumba za ibaada.
 
Back
Top Bottom