BAKWATA: Mgomo wa madaktari ni batili

Tatizo hii inayojiita Jumuiya ya Kiislamu na baadhi ya makundi ya Kiislaamu yamekuwa yakitumika na serikali ya Kikwete kwa maslahi binafsi.

Bakwata wameshindwa hata kuboresha zahanati zao- hawana hata hospitali moja ya mkoa, achilia mbali ya Rufaa. Hawa ni kupiga domo tu: Sasa kama mgomo ni batili, kipi halali? Ni serikali kushindwa kutoa huduma za afya wa wananchi wake?

Au kwa kuwa Bakwata wameshindwa, ndiyo wanataka kuhalalisha kushindwa huko na kushindwa kwa serikali.
watu mnatia aibu na mnaudhalilisha uislamu. Mmetumika wakati wa uchaguzi, mmepata nini? Mbona kila uchao ndiyo kwanza mnalalamika eti, matokeo ya watoto wenu yanachakachuliwa!


si afya tu hata shule zao za sekondari matokeo yao no mabovu na hasa zile za vijini, na hii si leo tu ni mlolongo wa siku nyingi .Kimsingi unapotoa mada jaribu kuwa analytical , huyu jamaa kama anatoka bakwata achunguze bakwata kama iko sawa .wao wenyewe wameuza mali za bakwata kama viwanja wakamuuzia manji wakapewa rushwa wakanyamaza, leo wanadandia la madaktari, wasafishe nyumba zao kwanza
 
Nimesema mara nyingi na sitaacha hadi wa-Tz waelewe hatari ya kuruhusu viongozi wa dini kutoa matamko!
Mzee Kingunge alipinga waraka wa maaskofu mkamuona mpuuzi, aliona mbali!
Dini na Siasa (hasa ya demokrasia) havihusiani.
Kwenye siasa kuna mijadala na kulumbana na hoja, kwenye dini kuna pre-conceived beliefs ambazo hata kuzihoji ni mwiko
Misikitini na makanisani padri/shehe/mchungaji akihubiri hakuna kuomba muongozo... Ni udikteta uliokubaliwa!
Watu hawa waliozoea kuwa mawazo yao ni sahihi na ya wengine yamepotoka hawafai kwenye demokrasia
Wanaropoka na wanataka tufuate miropoko yao kisa wao ni viongozi na wanataka viongozi wa kisiasa waabudiwe kama wanavyoabudiwa wao!
Ukimhoji kiongozi wa siasa kwao nongwa na utovu wa adabu maana wao kwenye misikiti na makanisani hawahojiwi
Wa-tz msikubali dini ichanganywe na siasa kama msivyokubali chumvi kwenye chai.
Viongozi wa dini mna wajibu wenu lakini si kwenye mambo ya siasa
Msithubutu mawazo yenu mlazimishe yawe ya waumini wenu
Kuwa viongozi haina maana mnatuzidi uelewa
 
Kila siku Mnalalamika MOU,MOU,MOU..Kwani nyinyi mlikatazwa kuanzisha hospitali zenu ili na nyie mpokee hiyo ruzuku kama ya Mou? Acheni kupiga domo tu,kama vipi na nyie anzisheni hospitali zenu mtapewa ruzuku na serikali ya baba rizi1.
 
Pamoja na Uislamu wangu, napinga hili tamko la Katibu Mkuu wetu wa Vijana BAKWATA. Napinga pia shinikizo la kutulazimisha tusihesabiwe kwenye sensa. Hivi sisi Waislamu tuna tatizo gani? Kwa nini tunalalamikia mambo ambayo hayana mshono na Uislamu wetu?

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com

bro big up! Kudos!
 
Katibu Mkuu wa Vijana wa BAKWATA amesema mgomo wa madaktari unaoendelea hauna nia njema kwa taifa.
Amedai mgomo huu unaweza kusababisha vifo vya watz wasionahatia.
amewataka wote wanaoshabikia mauaji ya watz kwa kisingizio cha maslahi kuacha kufanya hivyo kwani ni *kinyume na ubindaamu.
Amewataka waislam na wapenda amani kwa Ujumla kuacha kushabikia vitu visivyo vya msingi

SOURCE: REDIO IMAAN
KIPINDI CHA MWANGAZA KWA JAMII

Kugomea sensa ndo kuna maslahi kwa taifa. Ahsante sana. KICHEFUCHEFU!
 
Pia mimi namshauri yule Padre aliyesema 'JK ni chaguo la mungu' ajitokeze kukemea huu mgomo, kwa lengo la kumsaidia kazi kiongozi dhaifu. Pinda alisema madaktari waliogoma atawafukuza kazi- akawa dhaifu. JK nae alikutana nao na kutoa ahadi ya kumaliza matatizo nae kashindwa!. kumbe mnyika alikuwa sahihi pale bungeni.
 
Pamoja na Uislamu wangu, napinga hili tamko la Katibu Mkuu wetu wa Vijana BAKWATA. Napinga pia shinikizo la kutulazimisha tusihesabiwe kwenye sensa. Hivi sisi Waislamu tuna tatizo gani? Kwa nini tunalalamikia mambo ambayo hayana mshono na Uislamu wetu?

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com

We TUMBIRI mbona jina lako si la dini yetu? Wajiitaje wa dini yetu yakhee....!
 
hivi waislamu wanapokwenda hospitali na kuona akina mama wanalala wanne au zaidi kitanda kimoja, au pale MNH hasa wodi za sewahaji watu wamelala hadi mlangoni chini tena wagonjwa wa ajali wenye vidonda vikubwa, je huwa wanaridhika? sasa madaktari wamegoma ili serikari iweze kurekebisha hali hiyo nyie mnatuambia eti ''mgomo huu batili'' kweli mna nia nzuri na watanzania?
 
Binafsi sifurahishwi na uamuzi wa mgomo wa Madaktari kwani naamini serikali bado milango yake ipo wazi kwa majadiliano.Kauli za viongozi wa dini kuhusu masuala mbalmbali ya nchi ni jambo la kawaida na tumeishalizoea,si BAKWATA tu waliotolea kauli suala hili hata kuna baadhi ya viongozi wa dini nyingine wametoa matamko yao.Hebu tusiwe bias kwa chuki zetu binafsi.
 
ivi mgomo wa madaktari ni wa maslahi tu au kuna vitu vingine?mbona hawazungumzii madai ya madaktari ya kutaka mazingira bora ya kufanyia kazi na kutolea huduma jambo ambalo ni cost effective..jamaa wakiendelea kutibu watu kwa uduni na upungufu wa vifaa ivi inahitaji akili ya ziada kujua madhara yake ni makubwa zaidi??
Dhaifu anahaha kutafuta public support kitu ambacho hawezi kukipata kwa watu makini.

acha upoyoyo wewe ,hapo ni maslai tu na ubinafsi, hayo mengine ni kutafuta uhalali tu,kama wanapigania uboreshaji wa huduma za afya kwa ujumla wake kwa nini walikataa kujumuishwa watumishi wengine katika kuboresha hayo maslai.tatizo watanzania ni wavivu wa kufikiri kila jambo mnalichukulia kiushabiki kama simba na yanga
 
bakwata inaongozwa na vilaza wanakurupuka na kuropoka,mlaaniwe bakwata.

Mods lugha hizi za kejeli,dharau na kuudhi natumaini kama mnazifuatilia. Kwa haiba nzuri ya furum hii naomba mchukue hatua dhidi ya kauli hizi na mtoa kauli hii.

Back to the nukta. Tukiondoa ushabiki wa dini, jambo gani baya walilotamka BAKWATA, hivi kutowataka madaktari kushiriki katika mgomo badala yake warudi makazini kwani uamuzi wao huu una athari kubwa sana kwa wananchi.

Naamini, ikiwa maamuzi yakuipinga BAKWATA hayakutawaliwa kisiasa inayolenga kuiangusha serikali iloiyoko madarani kwa kufanya nchi isitawalike. Leo Madaktari, kesho waalimu. Hivi nyie pro-CDM mbona mko kwenye the same line? Kutukana uislamu na taasisi zake sambamba na kuunga mkono maamuzi haya ya kinyama ya madaktari.
 
Back
Top Bottom