BAKWATA: Hatuutambui waraka wa Waislamu

Bluray,
Nitashukuru sana siku serikali itakapo ipiga vita Bakwata, kisha tuone kama wananchi watakuwa nyuma ya Bakwata badala ya kukisia kingetokea kitu gani. Na upo uwezekano mkubwa wa wtu kushindwa kuelewa kwani mara nyingi ujumbe wa Bakwata unachukuliwa kuwa ni ujumbe wa Waislaam . Hivyo kiongozi mmoja au wawili wa Bakwata wakipiga kelele kuonewa ni rahisi kwenu kufikiria kuwa waislaam wanalalamika kumbe ujumbe huo umetolewa na Kiongozi wa Bakwata akapewa wadhifa kama Mufti wa Waislaam.
Kifupi mkuu wangu waislaam wanakabiriwa na taitizo kaa la tanzania nzima yaani mnapewa rais na Uongozi wa CCM lakini kuna ujinga fulani wananchi wanashindwa kuwakataa viongozi au kuwawajibisha viongozi hao hao wabaya.. Binafsi nitapenda sana kuona Waislaam Wa Tanzania kwa mara ya kwanza wanafungua siku ya Idd siku moja wote bila kujali Mufti au bakwata kasema nini..
Nii Ujinga mkubwa kutofuata mwezi uloandama na kutangazwa na Saudia lakini tukafuata matangazo ya Pakistan na Afghanstan kuhusu kuandama kwa mwizi huo huo siku ya pili yake hata kama sisi hatukuuona mwezi..
NDIVYO TULIVYO ni pamoja na kuweka tabaka kama hizi yaani bila sababu mtu anachukulia kuwa hili ni swala la Wwaislaam au Wakristu bila kufahamu kwamba kwa kila uwezesho wa Mtanzania mmoja ni pato kwa nchi nzima na sio kundi la watu fulani.. Maendeleo ya Tanzania hayawezi kuhesabiwa kwa makundi ya dini wala tusijidanganye kwamba kuna mtu anaweza kusema wakristu wameendelea kwa hili kuliko dini nyingine.. NI ujuha mkubwa sawa na Msudan au Ethiopia wanaamini kabisa kuwa nchi yao imeendelea kuliko Tanzania, Au Mtanzania kufikiri kuwa tumeendelea kuliko Zimbabwe..Yote inategemea na unaya tazama vipi maendeleo ya nchi au mtu.
Ndugu zangu Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu..kesho ktk kura za 2010 tutashindwa kwa upuuzi kama huu..
Mkandara,
Lazima ukubali kwamba Waislamu wanatakiwa kuwa na chombo kimoja cha kuwaunganisha, yaani structure fulani ili serikali ikitaka kuwasiliana na waislamu ijue imuendee nani na kuongea naye. Ndivyo ilivyo kwa wakristo. Wao wana vyombo vyao, kama vile TEC na CCT. Serikali ikitaka kuwasiliana na wakristo inaenda kwenye vyombo hivi na kupata maoni yao au misimamo yao katika masuala mbalimbali.

Kwenu waislamu chombo kinachofahamika na serikali ni Bakwata. Sasa kama hamuitaki Bakwata basi muioneshe serikali mnataka chombo gani cha kuwawakilisha kama waislamu. Na hili ni jambo la lazima kwa kweli. Si kwamba kila muislamu atajitokeza tu na kusema yeye anawakilisha waislamu. Haiwezekani. Shida iliyoko kwa waislamu ni kukosa umoja katika jambo hili. Kila kikundi kinataka kiwe msemaji wa waislamu na kiwe na nguvu ya juu. Hii inaleta anarchy. Mkae pamoja na kuamua chombo gani kiwawakilishe ninyi nyote. Sidhani kama mkiamua wote kwa pamoja kwamba "chombo chetu ni hiki" serikali itakataa
 
Back
Top Bottom