BAKWATA: Hatuutambui waraka wa Waislamu

Mimi ninavyojua na ndivyo ilivyo Bakwata iliundwa mara baada ya rais JK Nyerere kuvunja jumuiya ya waislam ya Afrika mashariki ambayo ilikuwa na nguvu sana.

JKN alitumia vyombo mbalimbali vya usalama na kuwatumia baadhi ya waislamu makachero kuuwa Umoja huo na baadaye akashinikiza kuanzishwa kwa BAKWATA chini ya katibu mkuu Kachero Adam Nassib, akina Kachelo Alhaj Kundya na wengine wote.

JKN aliunda Bakwata kwa nia na madhumuni ya KUWADHIBITI WAISLAMU kwani ni wao waliokuwa tishio kwake katika kuupenyeza Ukatoliki Nchini. Kwa maana hiyo JK alitumia ushawishi wake mkubwa kuhakikisha kuwa Bakwata ni chombo kinachowakilisha maslahi ya madhehebu yote ya kiislamu tanzania na wakati huo huo ni taasisi ya Serikali katika kudhibiti movement za waislamu.

Kwa misingi hiyo. Bakwata sio chombo kinachokubalika miongoni mwa waislamu bali ni chombo kilichoundwa na Serikali ya Tanzania kuwadhibiti waislamu.

Hata Leo hii waislam wapige kura kuchagua kama wanaipenda Bakwata au jumuiya nyingine zilizoundwa za waislam sidhani kama Bakwata watapata hata 5% ya waislam.

Fikirieni Waislamu wa Tanzania pamoja na pesa zao walizonazo wanazojengea miskiti na kupeana misaada BAKWATA ilishindwa hata kupata pesa za kufanya mkutano wake mkuu wa kuchagua viongozi wake mpaka wakafanyiwa harambee na kuchangiwa na kanisa kufanikisha mkutano huo.

Swali lako Dr barubaru mimi sijui kwanini serikali inaipenda bakwata wakati waislamu wenyewe hatuipendi. labda labda wao wanausajili wa juu kulinganisha na taasisi nyingine za kiislamu. Hilo labda utufafanulie kidogo kuhusu usajili kwa mujibu wa sheria.

Namaliza kwa kusema. Bakwata si lolote si chochote kwa waislamu bali ndio sikio kuu la Serikali.
.

Kumbe Pengo na wenzake wanamchango wao mkubwa katika kumuweka Shehe mkuu madarakani. Basi ana haki zote kusubiri jibu la BAKWATA.


Nasriyah yupo Tripoli lakini atakujibu tu kuhusu huo usajili kisheria,

Nimefurahi zaidi kwa ufafanuzi wako Hafif
 
Barubaru,

Kwa kuuliza swali hili jiulize je, kabla ya BaKWATA hapakuwa na umoja mwingine wa waislamu, au jumuiya zingine za kiislamu?, pia jiulize kama zilikuwepo je zimeishia wapi? Pia tafiti iliundwa vipi na kwa kutumia vigezo gani? Ukitafita kwa ndani utagundua na kushangaa sana.

Choveki.
nafikiri HM Hafif kakujibu masuala yako. Mie sina cha kuongeza.
 
Nimekuwa najiuliza siku zote huko Tanzania. Je Bakwata ina wafuasi wowote ukilinganisha na jumuiya nyingine za waislamu huko Tanzania especially Tanzania Bara.

Mimi naona kuna Jumuiya kama Baraza Kuu, Shura ya maimamu .n.k Hizi zina misimamo ya kidini sana katika kutetea haki za waislamu na uislamu.

Kwanini Serikali ya TZ inaikumbatia Bakwata? Kuna agenda gani kwa serikali?

Wangeipiga vita, ungesema waislam wanaonewa na serikali.

Wameikumbatia, unasema kwa nini serikali inaikumbatia BAKWATA.

Tukisema huwezi kuridhishwa utakataa?
 
Inawezekana ukawa na points kwa baadhi ya unayoyaongelea lakini unapojifanya kuwa huoni uonevu juu ya Waislamu unafanya hivyo kwa ajili ya kuvutia upande wako. Hebu tuangalie suala dogo tu la Mahakama ya Kadhi hili lilitaka hiyo unayoiita elimu dunia? Hivyo hili la Wakristo kuhoji kila anapochaguliwa Muislamu kwenye nafasi kubwa huoni kuwa ni tatizo hilo?
Tunapoangalia tabaka au jamii fulani inajiimarisha katika vyombo vya jamii na kuwaacha wengine huoni kuwa hilo linajenga tatizo la kijamii?
Hebu natuangalie hili tatizo la tofauti ya kipato katika jamii yetu, kwanini tunaliona tatizo wakati wenzetu walio na kipato kikubwa waliwahi mapema ikiwa kielimu au kuhodhi rasilimali? Tukae kimya tu na tuache kulaumu na badala yake kama unavyowashauri Waislamu na tuendeleze elimu na tuone jee itafika siku tofauti hii iondoke.
Hili unalolifikiri wewe na pengine wengi wengine ni sawa na kuona kuwa Waislamu wanajitaki wenyewe kwa lililowakuta lakini unasahau kuwa kwa kipindi kirefu kuwa elimu ulikuwa chini ya KANISA na kuipata kulihitajika kupoteza imani ya mtu. Hali hivi sasa imerudia tena kwa utitiri wa vyuo vya kikiristo na ni siri iliyowazi kuwa upo mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa hali hii inaendelea

maneno sawia kabisa Ngekewa.

Allahu yazidikum jamiiya
 
Mimi nasema wacha hao sijui mashura waje na waraka wao maana ni haki yao.
Sisi huku tutaendelea kuchambua pumba na mchele. Hamna mbaya. Nini kinawagonganisha vichwa?
Watuwekee hapa huo waraka wao kama ulivyo tuusome na tulinganishe na wa wakatoliki na wengine wote watakaokuja na waraka/mwongozo, kisha tutajua tufuate wa nani, uliotungiwa kanisani? msikitini au kwenye dangulo? Uamuzi utabaki wetu.
 
Bluray,
Nitashukuru sana siku serikali itakapo ipiga vita Bakwata, kisha tuone kama wananchi watakuwa nyuma ya Bakwata badala ya kukisia kingetokea kitu gani. Na upo uwezekano mkubwa wa wtu kushindwa kuelewa kwani mara nyingi ujumbe wa Bakwata unachukuliwa kuwa ni ujumbe wa Waislaam . Hivyo kiongozi mmoja au wawili wa Bakwata wakipiga kelele kuonewa ni rahisi kwenu kufikiria kuwa waislaam wanalalamika kumbe ujumbe huo umetolewa na Kiongozi wa Bakwata akapewa wadhifa kama Mufti wa Waislaam.
Kifupi mkuu wangu waislaam wanakabiriwa na taitizo kaa la tanzania nzima yaani mnapewa rais na Uongozi wa CCM lakini kuna ujinga fulani wananchi wanashindwa kuwakataa viongozi au kuwawajibisha viongozi hao hao wabaya.. Binafsi nitapenda sana kuona Waislaam Wa Tanzania kwa mara ya kwanza wanafungua siku ya Idd siku moja wote bila kujali Mufti au bakwata kasema nini..
Nii Ujinga mkubwa kutofuata mwezi uloandama na kutangazwa na Saudia lakini tukafuata matangazo ya Pakistan na Afghanstan kuhusu kuandama kwa mwizi huo huo siku ya pili yake hata kama sisi hatukuuona mwezi..
NDIVYO TULIVYO ni pamoja na kuweka tabaka kama hizi yaani bila sababu mtu anachukulia kuwa hili ni swala la Wwaislaam au Wakristu bila kufahamu kwamba kwa kila uwezesho wa Mtanzania mmoja ni pato kwa nchi nzima na sio kundi la watu fulani.. Maendeleo ya Tanzania hayawezi kuhesabiwa kwa makundi ya dini wala tusijidanganye kwamba kuna mtu anaweza kusema wakristu wameendelea kwa hili kuliko dini nyingine.. NI ujuha mkubwa sawa na Msudan au Ethiopia wanaamini kabisa kuwa nchi yao imeendelea kuliko Tanzania, Au Mtanzania kufikiri kuwa tumeendelea kuliko Zimbabwe..Yote inategemea na unaya tazama vipi maendeleo ya nchi au mtu.
Ndugu zangu Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu..kesho ktk kura za 2010 tutashindwa kwa upuuzi kama huu..
 
Kwa nini Waislamu wasianzishe jumuiya nyingine ambayo wanaweza kuiamini? Na je Waislamu hawana utaratibu wa uongozi unao julikana? Kwa mfano kama ilivyo kwa makanisa? I'm just asking because kama waislamu wenyewe hawaitaki Bakwata sioni kuna shindwaje kuanzishwa jumuiya nyingine.
 
Bakwata ni chombo kinachoongozwa na Serikali ya CCM. Bakwata haitetei maslahi ya Waislamu. Nia yao kubwa ni kupunguza nguvu za Waislamu.
 
Nimekuwa najiuliza siku zote huko Tanzania. Je Bakwata ina wafuasi wowote ukilinganisha na jumuiya nyingine za waislamu huko Tanzania especially Tanzania Bara.

Mimi naona kuna Jumuiya kama Baraza Kuu, Shura ya maimamu .n.k Hizi zina misimamo ya kidini sana katika kutetea haki za waislamu na uislamu.

Kwanini Serikali ya TZ inaikumbatia Bakwata? Kuna agenda gani kwa serikali?

Hizi siasa za kupandikiza vibaraka ndani ya vyama vya kidini ilianzishwa na muasisi wao CCM, Nyerere. Bakwata ni chombo cha CCM na Serikali yake.
 
Kwa nini Waislamu wasianzishe jumuiya nyingine ambayo wanaweza kuiamini? Na je Waislamu hawana utaratibu wa uongozi unao julikana? Kwa mfano kama ilivyo kwa makanisa? I'm just asking because kama waislamu wenyewe hawaitaki Bakwata sioni kuna shindwaje kuanzishwa jumuiya nyingine.

Great thinking,

Hapa umeuliza swali la maana sana, kwamba kama ndugu zetu wasilamu hawaitaki Bakwata wanasubiri nini kuunda taasisi nyingine itakayosimamia maslahi yao? Wanamsubiri nani aianzishe?

Tatizo kubwa la ndugu zetu waislamu ni kuwa kuna matatizo ya msingi ya kimuundo na kiuendeshaji tofauti na makanisa na watu wa dini nyingine. Na ndio maana waona kila kikundi kinajipigia upatu ndio chajua uislamu na kujisingizia kuhodhi maazimio ya waislamu. Nadhani huu ni wakati muafaka kwa ndugu wasilamu kuacha kusingizia watu wengine kwa matatizo yalio ndani ya uwezo wao.

Inatia simanzi kuona watu wakiendelea kumnyooshea kidole Nyerere eti alitumia makachero waislamu kudhoofisha waislamu, hii ni aibu kwa mtu mwenye busara kuleta kauli ya kipumbavu kama hii hapa jamvini.
 
Jamini huko kudhulumiwa kwa waislamu walidhulumiwa na nani?Wakati wenzao wanakimbia wao wanatambaa(wanacheza tu bao).Hwataki kufanya kazi wanishia kuombaomba tu na ndio maana kila ijumaa imewekwa na baadhi ya wenzao kwenda kuchukua msaada.Fanyeni kazi,someni acheni majungu na vikao vya kucheza bao.Uwiano wa kipato ni kwa sababu ya ugiogoi wenu.Swala 5 kwa siku kazi utafanya saa ngapi?
 
Kwa nini Waislamu wasianzishe jumuiya nyingine ambayo wanaweza kuiamini? Na je Waislamu hawana utaratibu wa uongozi unao julikana? Kwa mfano kama ilivyo kwa makanisa? I'm just asking because kama waislamu wenyewe hawaitaki Bakwata sioni kuna shindwaje kuanzishwa jumuiya nyingine.
.

Waislamu wa Tanzania wana jumuiya nyingi sana ambazo zimesajiliwa kisheria kama baraza kuu , Jumuiya ya hibathi tanzania, jumuiya ya suni na nyingine nyingi.

Sasa suali kwanini Serikali ya Tanzania inaikumbatia Bakwata? hilo ndio suala langu.
 
Jamini huko kudhulumiwa kwa waislamu walidhulumiwa na nani?Wakati wenzao wanakimbia wao wanatambaa(wanacheza tu bao).Hwataki kufanya kazi wanishia kuombaomba tu na ndio maana kila ijumaa imewekwa na baadhi ya wenzao kwenda kuchukua msaada.Fanyeni kazi,someni acheni majungu na vikao vya kucheza bao.Uwiano wa kipato ni kwa sababu ya ugiogoi wenu.Swala 5 kwa siku kazi utafanya saa ngapi?

Hapo umenena jambo mkuu!!
 
Inawezekana ukawa na points kwa baadhi ya unayoyaongelea lakini unapojifanya kuwa huoni uonevu juu ya Waislamu unafanya hivyo kwa ajili ya kuvutia upande wako. Hebu tuangalie suala dogo tu la Mahakama ya Kadhi hili lilitaka hiyo unayoiita elimu dunia? Hivyo hili la Wakristo kuhoji kila anapochaguliwa Muislamu kwenye nafasi kubwa huoni kuwa ni tatizo hilo?
Mkuu, pamoja na kuwa ni haki ya kila mtu kutoa maoni yake (yoyote) bila kuvunja sheria, ila kuna maoni ambayo yana walakini mkubwa na madhara kwa jamii yetu. Kwa maoni yangu, sidhani kuwa suala la udini lina nafasi kubwa kwa waTanzania kama baadhi ya watu wanavyotaka ionekane. Waraka wa Shura ya Maimam unaelezea mambo mengi. Mengi kati ya mambo yanayoelezewa ni kutoka kwenye clips za magazeti mbalimbali na matukio ya udhalilishaji wa waislam wa India. Vile vile waraka/mwangozo huo unaelezea historia ya jinsi dini ya ukristo ilivyokuwa ikienezwa nchini (miaka mingi iliyopita). Ila kwa kifupi, malalamiko mengi yalitakiwa yawe kwa serikali zaidi kuliko kwa dini nyingine.

Mkuu, umeainisha wakristo kuhoji kuchaguliwa kwa Muislam kwene nafasi za juu. Sijui umeitoa wapi hii. Kwa maana nakumbuka waTanzania wengi (zaidi ya 80%) walimchagua Jakaya Kikwete (muislam) na Dr. Mohamed Shein (Muislam) kuwa viongozi wa juu kabisa kwenye uongozi wa Taifa hili. Uchaguzi huo ni wa pili kufanyika baada ya waTanzania 99% kumchagua A.H. Mwinyi mwaka 1985 na 1990. Najua kuwa hata wewe unafahamu kuwa asilimia kubwa kiasi hicho si ya Waislam pekee. Si ajabu viongozi hao walipata kura nyingi zaidi kutoka kwa wakristo kuliko hata kutoka kwa waislam wenzao.
Ni mara nyingi sana (tangu enzi za awamu ya kwanza) tumeona malalamiko ya aina hii yakitoka kwa waislam kuliko kwa wakristo. Sidhani kuwa mijadala kama hii ina maana nzuri wala manufaa yoyote kwa Taifa letu.

Tunapoangalia tabaka au jamii fulani inajiimarisha katika vyombo vya jamii na kuwaacha wengine huoni kuwa hilo linajenga tatizo la kijamii?
Hebu natuangalie hili tatizo la tofauti ya kipato katika jamii yetu, kwanini tunaliona tatizo wakati wenzetu walio na kipato kikubwa waliwahi mapema ikiwa kielimu au kuhodhi rasilimali? Tukae kimya tu na tuache kulaumu na badala yake kama unavyowashauri Waislamu na tuendeleze elimu na tuone jee itafika siku tofauti hii iondoke.

Mkuu, malalamiko yako ni ya kweli? Maana ninavyojua kuna waislam ambao wamejitahidi kiuchumi na kuwa matajiri wakubwa sana katika Taifa hili. Mifani ya akina S.S. Bakheresa, Yusuf Manji, Mohamed Dewji, Abood, Raza, na wengine wengi ni mifano ya uongo wa post yako.

Suala la kujikwamua kiuchumi ni la kila mmoja wetu. Wote tuna fursa sawa kabisa katika kufanya juhudi za kujiendeleza, na waliojitahidi wamefanikiwa na wengine wengi wanaendelea kufanikiwa. Haijawahi kutokea katika historia ya imani zetu makanisa popote nchini yakafanya jitihada za kuwawezesha waumini wao kiuchumi (au kufanya hivyo kwa kutumia serikali). Tufanye kazi kwa bidii ili tupate kila tunachokihitaji. Uwezo tunao, ila malengo yetu yanaweza kuwa tofauti. Tusiwalaumu wale wenye malengo yaliyoweza kuwasaidia kufanikiwa. Kama tunaweza, tuwaige kwa uangalifu.

Hili unalolifikiri wewe na pengine wengi wengine ni sawa na kuona kuwa Waislamu wanajitaki wenyewe kwa lililowakuta lakini unasahau kuwa kwa kipindi kirefu kuwa elimu ulikuwa chini ya KANISA na kuipata kulihitajika kupoteza imani ya mtu. Hali hivi sasa imerudia tena kwa utitiri wa vyuo vya kikiristo na ni siri iliyowazi kuwa upo mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa hali hii inaendelea.

Sidhani kuwa kuna mtu yeyote anaependa kuwa masikini au kuwa na hali mbaya kiuchumi, kielimu n.k. Ila ni kweli pia kuwa kama tusipofuata njia sahihi ya kujikomboa na umasikini, kutafuta elimu kwa bidii hatutaweza kuwa sawa na wale watakaofanya bidii kujikomboa kwa njia sahihi. Ni kweli kuwa Makanisa yalitumia rasilimali nyingi kujenga shule, mahospitali n.k. Juhudi hizo hizo zinahitajika kufanywa na taasisi nyingine zote za dini.
Kumbukumbu yangu inanionyesha kuwa miaka mingi iliyopita jitihada kubwa za waislam zilikuwa ni kujenga madrasa zaidi na kusisitiza watoto wao kusoma elimu ya dini na wakati mwingine kuacha kabisa kusoma elimu ya kawaida (Elimu Dunia). Ni dhahiri kuwa hali ingekuwa tofauti kama wangesisitiza kuelimisha watoto wao kwa elimu zote mbili kwa bidii zaidi. Kwa waliofanya hivyo, matunda mazuri waliyapata.

Kwa kuongezea tu, mashule hayo ya wakristo yalisomesha waislam pia. Mifano ni mingi. Na wote bado ni waumini wazuri wa uislam, si ajabu kuliko hata wale ambao hawakupata elimu kutoka kwenye shule hizo. Hivyo, si kweli kuwa waliosoma huko walitakiwa kubadilisha dini zao.
 
Nadhani bakwata wameukataa mwongozo huo kwa vile waislamu wana ugomvi na makundi mawili, Kwanza serikali na pili wakatoliki. Kama mwongozo ungeelelekezwa kwa serikali tu, angalau wangeeleweka.

Waislamu inabidi wamshukuru saaanaaaa NYERERE. Yaani kama asingetaifisha zile shule, gepu la elimu lingekuwa kubwa kuliko lilivyo sasa. Hii inatokana na wao kuingia sana kwenye madrasa kuliko "elimu dunia" kama wanavyoiita. Na inawezekana hii ndiyo inayofanya wao wawe nyuma sana katika mgawanyo wa madaraka. Maana huko kwenye madaraka, MADRASA haitumiki. Hata ukiwaangalia walioko madarakani asilimia kubwa walisoma SEMINARI, e.g Salimu A. salim, Kikwete, Akina Mudhihiri, na wengine wengi.

Swali la kiaina, "Hivi SHURA YA MAIMAMU inatambulika kisheria?"
 
kuanzia waraka wa katoliki na huu wa waislamu.
inaonesha jinsi gani tunavyotafuta golden chance ya kutibua amani yetu.

nawaambia maneno yangu kwamba tusipokuwa makini hii ngoma ambayo mwanzo wake ni lele itapata wachezaji kupitia dini. na ikianza kuchezwa itakuwa chamchela

Ni uelewa mdogo tu ndio unaosababisha haya. Sioni ni kwa jinsi gani waraka ule uliotolewa na Kanisa unaweza kutibua amani. Kinyume chake ni kwamba utaleta amani zaidi kwani unazungumzia uadilifu wa viongozi. Tunataka nini zaidi ya hilo jamani?!! Tatizo lipo kwa hawa wengine -- sijui Shura ya Maimamu -- ambao wamekuja na kituko. Wao sasa badala ya kuzungumzia mambo ya jumla yenye manufaa kwa Watanzania wote, wanaanza kujitenga kwa mambo ya udini. Hii ndiyo hatari. Hebu tujaribu kuwa understanding!
 
duh hii shura ya maimam nani kawapa kibali?naona hamna haja ya kuwajadili,kwani binafsi ninao friends kibao waislam tunapambana sice school hadi mtaani kimaendeleo,hawa jamaa wamegoma kuwapeleka watoto wao madrasa wakasema hiyo akili ya kukaririshwa bora waende shule za kawaida,lakini msikitini wanaenda,wanafunga ramadhan kama kawaida,the guys wao wamekuwa na mtazamo kwamba ninyi wakristo mnatumia muda mwingi kujifunza vitu vya humu duniani tunamoishi,so lazma kidunia muendelee,mashule,hospitals etc, so acheni kupiga domo lakuonewa,hiyo ya kipiga domo tumewaachia wanawake kulalamika wanaonewa,je nyie shura ya maimam ni wanawake?au tuwe na taasisi ya 'HAKI ZA WANAWAKE NA WAISLAMU' then mkutano muende wote BEIJING??be sensible ati!
Im sure ingekuwa JK na Shein wangekuwa wakristo tusingekunywa maji nchi hii hizo kelele zingepigwa hata anga kutoboka!!but christians tupo ok tunataka viopngozi si Dini ya kiongozi!!
 
ina maana viongozi wa dini kazi ya uchungaji ime washinda? nianacho kifahamu ni hiki ikiwa mtaweza kuwalingania waumini wenu kuwa wanyenye kevu kila siku wanapotoka kwenye mikusanyiko ya ibada ingetosha kabisa kuya maliza haya.ni ajabu sasa viongozi wa dini mmeacha kabisa mambo ya dini mna shughulika na mambo ya kidunia zaidi.ukisikia kondoo wana jichunga wenyewe ndiyo sasa maana mchungaji ana jishughulisha na utafutaji wa matunda ili ashibishe tumbo lake.
 
Back
Top Bottom