Bakwata, Basuta Walaani DC Kuvuliwa Hijabu

Status
Not open for further replies.
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.
<br />
<br />
Muwe mnaangalia na habari za kupost hapa,unatuletea habari za Radio ya kinafiki ipeleke msikitini hiyo habari yako.
 
Hao mashehe uchwara waache kiherehere chakuingilia mambo yasiyowausu wapambane na mahakama ya kadhi nawajue sisi wa Cristo ndotuna waamulia mamboyao tumeamua haitakuwepo na aitakuwepo
 
<br />
<br />
wewe sio muislamu, waislamu wote ni sawa na mwili kinapouma kidole mwili mzima unauma, sasa wewe amevuliwa hijabu muislamu mwenzako unasema huungi mkono, kama wewe ni muislam ni mnafiki au huijui dini yako, cdm itabaki hapa hapa duniani dini unakwenda nayo kwa mungu wako,

hapo redi, umesema kweli maana ndivyo mlivyo.
 
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.

Sherehe za EID wanasherehekea siku tofauti - Kwenye vazi wote wameungana!!! Njaa ni kitu kibaya sana!!!
 
Ningewaona wamaana kama wange-comment kuhusu kuzuiwa kwao kuanzishwa kwa Kadhi kuliko mambo ya kijinga namna hii, lile lilikua hijabu au mtandio? au kila kitu sasa kimekua hijabu? tuache unafiki na uzandiki.
 
Baraza kuu la waislam Tanzania(BAKWATA), na Baraza kuu la Answar suna Tanzania(BASUTA), kwa pamoja wamelaani kitendo cha viongozi wa CDM Kumvua hijabu DC Fatuma kimario wamesema kitendo hicho walichofanya chadema kwa mujibu wa uislam ni kama wamewadhalilisha waislam wote Duniani kwa hiyo amewataka viongozi wa chadema kuwaomba radhi waislamu alisema Naibu mufti akiwa mjini Tabora, Fatuma ana imani yake japo ni DC, heshimuni imani yake kwani waliomchagua wanajua kuwa imani yake inamtaka avae hijab alisema sheikh mohamed issa wa Answar Sunna. taarifa ya habari Radio Imani.

Ndiyo tatizo la kukurupukia jambo bila kulijua vizuri. Wanapaswa kujua hii ni siasa tu hakuna chochote cha kudhalilisha dini wala imani ya mtu hapa. Ndiyo maana mnakuwa walalamishi badala ya kuchukua hatua kama viongozi uwezo wao ndio huu ipo kazi kweli
 
Mkuu! Naona wengi wanajichanganya,mimi sitetei mambo DC aliyofanya! Ieleweke hivyo,na tafadhali isomeni post vizuri. Kumbukeni ni lazima kuiheshimu imani ya mtu! Kama wangetumia busara yote yangefika huku? Mimi nasisitiza CDM watuombe radhi! La sivyo kitakachofuatia watakijutia na kuomba radhi wakati huo watakuwa wamechelewa! Jamani mbona mambo yapo wazi? Tatizo kubwa la JF ni ushabiki. Ma great thinker wako wapi? Bandubandu humaliza gogo na kidogokidogo hujaza kibaba,hizi ni lawama CDM wanajikusanyia. Sijasahau kadhia ya uchaguzi mwaka jana kwa CDM kuwadharau Waislam kwa kumchukua mgombea mwenza darasa la saba,hii ni dharau ya hali ya juu! Na dharau nyinginezo,haya hayajengi na hayawezi kufanywa na watu makini.

Umeongea meengi kwenye post kadhaa katika jitihada za kuutetea Uislamu lakini hapo kwenye red umenishangaza.
 
Mimi nilijua tu ya kwamba CCM wamezungumzia Hijabu kwa maana maalum. Na nilijua kwa uhakika waislaam watakuja hapa na kupiga makelele kuhusiana na mwanamke kuvuliwa Hijab lakini bila weledi wa maudhui ya uvaaji wa Hijab. Sababu sii kuvuliwa Hijab kwa sababu hata unapokwenbda kupiga picha ya passport mwanamke hulazimika kuivua Hijab..
Tukio hilo halikutoa kwa kwa sababu ya imani, sera au ilani ya chama kupinga uvaaji wa Hijabu. Hii inadhihirisha wazi CCM wanatafuta siasa za majitaka na hao masheikh wa BAKWATA na BASUTA ni maamuma wanaotumiwa na CCM pasipo kufikiria kwanza..Kinachokatazwa kisheria ni kukataza wananwake wasivae Hijabu, na Chadema hawana tatizo na Hijab wala haki ya wananwake kuvaa hijab isipokuwa hijab ilimtoka kama vile viatu vilivyotoka...na mbona msizungumzie viatu vyake!

Kweli mkuu,

Hawa wameamua ama kwa kujua au kutokujua kununua kesi....Waache waendelee kutumiwa na CCM. Nasikitika kwamba mpaka sasa hawajajifunza kwamba cost ya kutumiwa ni kubwa sana. Mtu anayetumiwa anakuwa kama muwa, utamu ukiisha maganda yanatemwa chini. Wangejaribu kujichunguza ni mara ngapi wametemwa kama maganda ya miwa ili wasiwaingize tena wafuasi wao kwenye matatizo mengine!

Na kwa vile kesi iko mahakamani, wakae kimya ili wote tusubiri hukumu. Kama hawajaridhika na mashtaka yaliyopelekwa mahakamani basi waombe ruhusa kufungua kesi nyingine au kurekebisha hii inayoendelea..

Naamini historia itatusaidia kuwajua wasaliti wa nchi hii...Hawa ni miongoni mwao!
 
Kama mtu ni mwizi kuna faida gani hata ya kuvaa hijabu? kwanini msingelaani kitendo chake cha kushawishi hao viongozi wa vijiji kutenda wizi na badala yake wanashikilia hijabu(mtandio)? Dhambi ni ipi? kuiba au hijabu (mtandio)? kwa hio nikivaa kanzu/hijabu/mtandio mimi nitakua nimetakasika na uasherati, wizi, uzinzi na kadhalika? tuache unafiki bhana mbona tunauchafu na kuudhalilisha uislamu? siamini kama kweli waislamu watakubaliana na hoja ya mabaraza hayo mawili, hawa ni vibaraka wa CCM. Ndugu zangu waislamu liangalieni jambo hili kisiasa na liachwe kwenye siasa, lile sio hijabu ni mtandio wanaofunika wanawake regardless ya dini zao.....
 
Kiongozi wake ni nani? na Ibada zao wanafanyia wapi?

Paganism (from Latin paganus, meaning "country dweller", "rustic") is a blanket term, typically used to refer to polytheistic religious traditions (i.e. those with multi beliefs.It is primarily used in a historical context, referring to Greco-Roman polytheism as well as the polytheistic traditions of Europe and North Africa before Christianization. In a wider sense, extended to contemporary religions, it includes most of the Eastern religions and the indigenous traditions of the Americas,Central Asia, Australia and Africa; as well as non-Abrahamic folk religion in general. More narrow definitions will not include any of the world religions and restrict the term to local or rural currents not organized as civil religions. Characteristic of Pagan traditions is the absence of proselytism and the presence of a living mythology, which explains religious practice
.
 
CDM ile dhana ya udini iliyokuwepo wakati wa uchaguzi sasa ndio wanaidhibitisha! Hii ni hatari. Kama DC alifanya kikao na kutaka kuchakachua,basi wangechukua hatua kama watu wazima wenye busara na si kufanya na kuzungumza waliyozungumza. Kwahili mimi nazidi kujikusanyia ushahidi wa udini na chuki dhidi ya Uislam. Kama dhana hii itaendelea! Tutaikumbuka miaka 50 ya amani,kwani tutakuwa katika hali nyingine ya chuki ya hali ya juu.Ni kweli tumeichoka CCM na mfumo uliooza! Hivyo lengo ni kung'oa mfumo wote na kuanza upya,lakini kwa dalili nizionazo si njema kwani kunamgawanyiko na kudharauliana. Lakini kumbukeni jipu huanza kipele na mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipouziba ufa huu wa udini basi tutajenga ukuta kwa damu. Chadema tuombeni radhi Waislam kwa kitendo hicho! Kupuuzia,tutatangaza mgogoro mkubwa dhidi yenu. Kwani lengo lenu ni kuwatenga Watanzania kwa dini zao? Kuweni makini!

A very sensible and timely caution lakini ni watu wachache sana watakaoisoma hii contribution yako kwa umakini unaohitajika. Watu hapa wamejikita katika jazba na chuki zao dhidi ya chama hiki au kile, imani hii au ile. Lakini wahenga husema, samaki ndani ya maji hajui umuhimu wa maji. Wimbi la ukombozi likimtoa ufukweni na kumrejesha baharini ndipo anapotambua kwamba uhai wake bila maji si chochote. Lakini humu ndani hii thread yako itaishia kubezwa na kutukanwa, na utakuwa na bahati kama hutaambiwa kwamba hujasoma, mnywa kahawa, mvaa msuli, mtu wa madrasa n.k. Tena wengine wanaosema hivyo elimu zao ni duni kuliko wale wanaowakosoa. Pathetic!
 
Kama mtu ni mwizi kuna faida gani hata ya kuvaa hijabu? kwanini msingelaani kitendo chake cha kushawishi hao viongozi wa vijiji kutenda wizi na badala yake wanashikilia hijabu(mtandio)? Dhambi ni ipi? kuiba au hijabu (mtandio)? kwa hio nikivaa kanzu/hijabu/mtandio mimi nitakua nimetakasika na uasherati, wizi, uzinzi na kadhalika? tuache unafiki bhana mbona tunauchafu na kuudhalilisha uislamu? siamini kama kweli waislamu watakubaliana na hoja ya mabaraza hayo mawili, hawa ni vibaraka wa CCM. Ndugu zangu waislamu liangalieni jambo hili kisiasa na liachwe kwenye siasa, lile sio hijabu ni mtandio wanaofunika wanawake regardless ya dini zao.....

Kuna point moja nimekumbushwa na jamaa mmoja mweledi wa sheria, inasema kuwa "kila raia mwema anayo haki ya kumkamata mharifu (to arrest) na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria". Pia kwa maoni yangu, raia wema wanaweza kumtoa mtu mahali fulani ili kuepusha matatizo endapo kuwepo kwake kulikuwa kunatishia uvunjifu wa amani. Sasa katika process ya kumkamata mharifu, huwezi kukwepa purukushani ambazo zinazweza kusababisha kofia ya shekh, Askofu au mtandio wa Fatuma kudondoka. Naamini watu wengi hata hao Chadema watakuwa walipoteza vitu vyao katika kizaa zaa hicho.

Hata hivyo, naamini huko mahakamani waliopeleka kesi watatakiwa kumshawishi hakimu kwamba wanachedema walimfuata DC kwa ajili ya kumvua mtandio...Kama hawataweza basi hawa viongozi wa dini wasithubutu kuingilia kazi ya mahakama...la sivyo wasubiri hadi mwisho ili nao wakafungue kesi yao kwa mujibu wa imani yao. Kesi ya sasa haina kipengee cha imani hata kimoja na wasijaribu kuchafua hali ya hewa bila sababu ya msingi hata kama wameshopokea posho!!!
 
A very sensible and timely caution lakini ni watu wachache sana watakaoisoma hii contribution yako kwa umakini unaohitajika. Watu hapa wamejikita katika jazba na chuki zao dhidi ya chama hiki au kile, imani hii au ile. Lakini wahenga husema, samaki ndani ya maji hajui umuhimu wa maji. Wimbi la ukombozi likimtoa ufukweni na kumrejesha baharini ndipo anapotambua kwamba uhai wake bila maji si chochote. Lakini humu ndani hii thread yako itaishia kubezwa na kutukanwa, na utakuwa na bahati kama hutaambiwa kwamba hujasoma, mnywa kahawa, mvaa msuli, mtu wa madrasa n.k. Tena wengine wanaosema hivyo elimu zao ni duni kuliko wale wanaowakosoa. Pathetic!

Pathetic!
 
Masuala ya kisiasa tuyaache yatatuliwe kisiasa na maswala ya kidini yaachwe yamalizwe kidini.Masuala ya kuunganisha masuala ya siasa na dini mtazidi kutuharibia nchi.Hata mahakama ya kadhi mnataka kuifanya issue ya kisiasa wakati ni issue ya kiibada zaidi(waislamu na mambo yao).Hizo ni dalili za kufirisika kifkra!hakuna lolote na mtazikwa hivohivo na lawama zenu baada ya kujilipua mabomu hali makundi mengine ya dini yanazidi kusonga mbele na kustawi na kuwaletea waumini wao na watanzania kwa ujumla maendeleo ya kimwili na kiroho
 
A very sensible and timely caution lakini ni watu wachache sana watakaoisoma hii contribution yako kwa umakini unaohitajika. Watu hapa wamejikita katika jazba na chuki zao dhidi ya chama hiki au kile, imani hii au ile. Lakini wahenga husema, samaki ndani ya maji hajui umuhimu wa maji. Wimbi la ukombozi likimtoa ufukweni na kumrejesha baharini ndipo anapotambua kwamba uhai wake bila maji si chochote. Lakini humu ndani hii thread yako itaishia kubezwa na kutukanwa, na utakuwa na bahati kama hutaambiwa kwamba hujasoma, mnywa kahawa, mvaa msuli, mtu wa madrasa n.k. Tena wengine wanaosema hivyo elimu zao ni duni kuliko wale wanaowakosoa. Pathetic!

Kama kuna jambo nalichukia ni kuingiza imani za dini katika mambo ambayo hayahitaji kuingiliana na imani za watu ili yashughulikiwe....Kesi ya DC na CHADEMA haina hata chembe moja ya dini! Ndiyo maana toka mwanzo hatukusikia dhehebu lolote likishangilia kwamba dini fulani imekomolewa. Ila sasa nyie na hao viongozi wa dini mnaojaribu kuingiza facet ya dini kwenye hii kesi ndio wa kuogopa kama ukoma!
 
mimi nilijua tu ya kwamba ccm wamezungumzia hijabu kwa maana maalum. Na nilijua kwa uhakika waislaam watakuja hapa na kupiga makelele kuhusiana na mwanamke kuvuliwa hijab lakini bila weledi wa maudhui ya uvaaji wa hijab. Sababu sii kuvuliwa hijab kwa sababu hata unapokwenbda kupiga picha ya passport mwanamke hulazimika kuivua hijab..
Tukio hilo halikutoa kwa kwa sababu ya imani, sera au ilani ya chama kupinga uvaaji wa hijabu. Hii inadhihirisha wazi ccm wanatafuta siasa za majitaka na hao masheikh wa bakwata na basuta ni maamuma wanaotumiwa na ccm pasipo kufikiria kwanza..kinachokatazwa kisheria ni kukataza wananwake wasivae hijabu, na chadema hawana tatizo na hijab wala haki ya wananwake kuvaa hijab isipokuwa hijab ilimtoka kama vile viatu vilivyotoka...na mbona msizungumzie viatu vyake!

hii imetulia, nimeipenda sana!!! Mwenye masikio na asikie neno hili!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom