Bakteria husababisha ugonjwa wa Parkinson?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Bakteria husababisha ugonjwa wa Parkinson? Imeandikwa Na Administrator





Watafiti nchini Marekani wameonesha uwezekano wa bakteria wanaosababisha vidonda vya tumbo (gastric ulcers) kuhusishwa na kusababisha ugonjwa wa Parkinson. Kwa mujibu wa taarifa ya watafiti hao, ilionekana kuwa panya waliotumika kwa ajili ya utafiti huo walionesha kuwa na dalili za ugonjwa wa Parkinson baada ya kudungwa bakteria wa Helicobacter pylori.
“Maambukizi ya bakteria hawa kwa panya yalihusika kwa kiasi kikubwa kuleta dalili hizo’ Ilisema sehemu ya ripoti ya utafiti huo iliyowasilishwa katika mkutano wa chama cha wanamikrobaiolojia wa Marekani (the American Society for Microbiology).


Ugonjwa wa Parkinson ni ugonjwa unaoathiri ubongo na kumfanya mgonjwa kutetemeka, kupungua kwa uwezo wa kutenda na kutembea kwa kuchechemea.
Katika utafiti huo, wanasayansi waliwadunga na kuwaambukiza bateria aina ya H. pylori panya waliokuwa na umri wa kati, wakiwakilisha binadamu wenye umri kati ya miaka 55 hadi 65, umri ambao ugonjwa wa Parkinson hujitokeza zaidi. Baada ya kuwafuatilia kwa kipindi cha

miezi sita, panya hawa walionesha kuwa na dalili zinazofanana na zile za Ugonjwa wa Parkinson kama vile kupungua kwa uwezo wa kujongea, na kupungua katika ubongo kwa kiwango cha dopamine, kemikali inayohusika, pamoja na mambo mengine, na kusaidia uwezo wa kujongea wa mwili na viungo vyake. Hata hivyo mabadiliko haya hayakuonekana kwa panya waliokuwa na umri wa kati au panya wachanga.

Mmoja wa watafiti, Dr Traci Testerman, wa Chuo kikuu cha Sayansi za Afya cha jimbo la Louisiana alisema kuwa matokeo ya utafiti huo yametoa mwanga wa kuwepo uwezekano wa bakteria wa H. pylori kuhusika katika kusababisha ugonjwa wa Parkinson kwa binadamu.

Aliongeza matokeo kuwa panya wazee waliathirika zaidi kuliko panya wachanga yanaonesha kuwa kitendo cha kuzeeka kinaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa Parkinson kwa panya kama ilivyo pia kwa binadamu.
Aidha watafiti wanaamini kuwa sababu iliyowafanya panya wale kupata ugonjwa wa Parkinson baada ya kudungwa bakteria wa H.pylori ni

kuwa bakteria hao huzalisha aina ya kemikali ambayo ni sumu kwa ubongo wa mnyama. Wanasema bakteria hawa walionesha uwezo wa kutumia lijamu (cholesterol) kutoka katika seli za mwili wa panya na kuongeza kiasili cha sukari kutengeneza kemikali mpya ambayo hufanana sana kimuundo na kemikali nyingine inayopatikana katika baadhi ya mimea inayohusishwa na kusababisha ugonjwa wa Parkinson.

Hata hivyo watafiti wanasema, matibabu ya H.pylori kwa mgonjwa wa Parkinson ambaye tayari ameshaingia katika hatua za mwisho za ugonjwa huo hayasaidii kuleta unafuu wowote kwa vile tayari seli kadhaa za ubongo huwa zimeathirika na kufa kabla hata dalili za Parkinson kujitokeza. Aidha seli nyingine zaidi za ubongo hufa kadiri ugonjwa unavyoendelea na mbaya zaidi seli hizi za ubongo hazina uwezo wa kukua upya pindi zikishaharibika.

Hata hivyo ripoti hiyo inaonekana kuleta tashwishwi miongoni mwa makundi kadhaa yanayojihusisha na ugonjwa wa Parkinson. Chama cha hisani cha Ugonjwa wa Parkinson cha nchini Uingereza kilisema kuwa matokeo ya utafiti huo hayana budi kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa.
Mkurugenzi wa kituo kimoja cha utafiti wa Parkinson huko Uingereza, Dr Kieran Breen alisema inajulikana na kuaminika kuwa ugonjwa

Parkinson husabaishwa na mkusanyiko wa mambo kadhaa zikiwemo sababu za mazingira pamoja na nasaba ya muhusika mwenyewe. Aliongeza kuwa kuna ushahidi kuwa bakteria hao wana uwezo wa kuzuia ufyonzwaji wa Levodopa, dawa inayotibu ugonjwa Parkison, katika kuta za tumbo na utumbo mdogo lakini hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa kuwepo kwao kwenye tumbo kunasababisha Parkinson.
Aidha alisema pamoja na kuwa utafiti huo umeleta chachu na changamoto kubwa, matokeo yake hayana budi kuchukuliwa kwa tahadhari na akashauri tafiti zaidi kufanyika ili kuthibitisha matokeo hayo.


Imehaririwa mnamo Jumatano, 25 May 2011 01:30

Source:Bakteria husababisha ugonjwa wa Parkinson?
 
Parkinson's disease is a common movement disorder.. It results from the death of cells which contain a chemical called dopamine, in a part of the brain, called the substantia nigra2. Without enough dopamine, nerves in the brain which control muscle action do not work properly, so it becomes hard to move normally.Parkinson's disease should always be diagnosed by a doctor who specialises in treating it, and you shouldn't start treatment before the diagnosis is confirmed .This is because Parkinson's disease can sometimes be difficult to distinguish from other similar conditions.For example, some of the symptoms of Parkinson's disease can also occur as a result of strokes, dystonia (tremor), other degenerative nerve conditions, overactive thyroid, Alzheimer's disease, and as side effects of medicines.e is no specific test for Parkinson's disease. There is no specific test for Parkinson's disease. The diagnosis is based on:
Parkinson's disease is diagnosed in people with bradykinesia (slow movement) and at least one of the following2:
  • Muscular rigidity
  • Rest tremor (4–6 Hz)
  • Postural instability unrelated to primary visual, cerebellar, vestibular or proprioceptive dysfunction.[h=1]
























    Stages of Parkinson’s disease[/h]
    Parkinson's disease is often divided into2:
    • Early disease: when symptoms appear and start to affect how well you can perform everyday activities, such as washing, getting dressed and walking, so that you need treatment
    • Later disease: when movement (also called motor) complications occur, usually after long-term initial stage treatment. These complications usually happen when someone has been taking levodopa for some time. But people vary and they can occur after quite a short period of treatment. Movement complications include5:
      • Early morning lack of mobility and stiffness caused by the effects of medication wearing-off over night
      • On/Off phenomenon: unpredictable loss of function and movement which can last a few seconds or much longer, and may be unrelated to ‘wearing off' of medication
      • Abnormal movements (dyskinesias): Uncontrolled arm, leg, face or other movements, such as flailing arms or repetitive chewing motion[h=1]
























        Treatment of Parkinson's disease[/h]
        Treatment of Parkinson's disease aims to control symptoms by replacing the missing dopamine in the brain, so that nerves and muscles can work more normally.
        As no single medicine can achieve this for everyone, there are several different drugs to choose from and your healthcare professional can speak to you about the options available.
        The goal is to find a treatment that will provide good relief of symptoms, with the least risk of side effects and movement complications.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom