Bajeti yetu ya maadhimisho ya uhuru wa tanganyika hii hapa...ni kilio

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu kupitia kwa jamaa zangu pale hazina kujua gharama tulizoingia kwa kuandaa haya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..

Kwa haraka haraka bajeti nzima ya maadhimisho haya ni bilioni 24 na kinara wa matumizi ni hazina wenyewe ambao wametumia karibu bilioni 4.Gharama hizi zinahusisha posho za wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohusika kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru na hasa kwa kamati ya maandalizi iliyokuwa chini ya mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda....

Gharama hizi zingeweza kulipa kiasi kidogo cha madeni ya walimu ambacho kinafikia karibu bilioni 64..Je,hii imekaaje watanganyika?

Nawasilisha!!
 
Hayo ni mawazo yako,Lakini kunakiongozi wa TZ tunayoitaka anayeweza kuwa na mawazo hayo hayupo,Viongozi wanawaza matumbo yao na watoto wao tu!
 
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu kupitia kwa jamaa zangu pale hazina kujua gharama tulizoingia kwa kuandaa haya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..Kwa haraka haraka bajeti nzima ya maadhimisho haya ni bilioni 24 na kinara wa matumizi ni hazina wenyewe ambao wametumia karibu bilioni 4.Gharama hizi zinahusisha posho za wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohusika kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru na hasa kwa kamati ya maandalizi iliyokuwa chini ya mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda....

Gharama hizi zingeweza kulipa kiasi kidogo cha madeni ya walimu ambacho kinafikia karibu bilioni 64..Je,hii imekaaje watanganyika?

Nawasilisha!!
Asante mkuu! Lakini Kwa hesabu za haraka haraka,hiyo data uliyopewa siyo ya ukweli! Yaweza kuwa zaidi ya hapo!maana hapo hata watumishi wamejenga majumba na kununua magari kwa njia ya maadhimisho! ....tumedthubutu tumeshindwa na tumekwama hapa hapa!
 
Duh. Mimi sikuona umuhimu wa vyote vile walivyofanya Leo. Hizo fedha wangenunu hata ambulance kwa vituo vyetu vya afya. Hii nchi ina hela ila zinaliwa na hao wakuu.
 
Serikari dhaifu,legelege,ya kijambazi,yenye mafisadi,vivu kufikiri ya CCM ndiyo yenye kuendelea kuwaibia wananchi dhaifu na wenye ulemavu wa uoga na wa kufanya maamuzi magumu.Serikari hi ya CCM ukiwauliza ni uhuru gani wanaosherekea,je ni uhuru wa Tanzania au Tanganyika au watanzania bara,hawana majibu katika hilo,hawa ni wahuni wakubwa wanaofanya biashara ya kuiba hela za watanzania kwa kudanganya kuna uhuru,uhuru upi watuambie? Tubadilike watanzania tuache ujinga wa uoga tupambane na hawa majambazi CCM,wao wana polisi,mafisadi na pesa,sisi tuna Mungu anayeturinda vita hiyo tutaishinda risasi za polisi haziwezi kuwamaliza watanzania wote.
 
Kuna mambo yanaweza kukuharibia siku na hata kukuingiza mahakamani maana waweza Uwa mtu bure kwa upuuzi unaoendelea
 
Maskini kuna mamia ya walimu wetu wamepandishwa madaraja tangu mwaka jana lakini hadi leo hawajarekebishiwa mishahara yao.Fedha zipo zinatumika kupigia matarumbeta ya uhuru!Dr Slaa ninakuona hapa.Hebu changia kidogo kuhusu hil!
 
Asante mkuu! Lakini Kwa hesabu za haraka haraka,hiyo data uliyopewa siyo ya ukweli! Yaweza kuwa zaidi ya hapo!maana hapo hata watumishi wamejenga majumba na kununua magari kwa njia ya maadhimisho! ....tumedthubutu tumeshindwa na tumekwama hapa hapa!

Naunga mkono hoja R.I.P Ccm
 
ushaidi wa kimazingira unaonesha ni fedha nyingi. Hata hivyo sina imani na figure uliotoa kwa sababu sijaelewa source yako ya information....
pamoja na hayo, it is a disaster kutumia fedha nyingi kwa mambo yasiokua na msaada sana kwa taifa.. miaka hamsini ingeweza kutumika kama kitu cha kupinga vikali uozo unaoendelea nchini hasa mambo ya kubaguana kwa maswali ya kiimani..Naona kwa ujumla wake tumeinvest on a liability...
Nnachopredict, sio muda mrefu sana utapata taarifa za jinsi zoezi hili lilivofaidisha wachache kwa kujivunia mabilioni ya shilingi na tenda za hovyo hovyo
 
Sidhani kama kuna tatizo. Tusonge mbele. Serikali hii ni sisi ndo tuliiweka madarakani baada ya wao kutuonga kanga, chakula cha msaada na nk.
Kama haturidhiki nayo basi 2015 ni njia bora kuing'oa madarakani na si vinginevyo.

Na log off.
 
Hiyo figure ni ndogo sana mkuu,hela waliyotumia hawa maharamia wa CCM na serikali yao ya kifisadi kwa maadhimisho haya ni zaidi ya bilioni 50. Walaaniwe majambazi hawa.
 
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu kupitia kwa jamaa zangu pale hazina kujua gharama tulizoingia kwa kuandaa haya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..

Kwa haraka haraka bajeti nzima ya maadhimisho haya ni bilioni 24 na kinara wa matumizi ni hazina wenyewe ambao wametumia karibu bilioni 4.Gharama hizi zinahusisha posho za wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohusika kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru na hasa kwa kamati ya maandalizi iliyokuwa chini ya mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda....

Gharama hizi zingeweza kulipa kiasi kidogo cha madeni ya walimu ambacho kinafikia karibu bilioni 64..Je,hii imekaaje watanganyika?

Nawasilisha!!

Haswa walimu madeni yao mpk huruma. Sasa hivi wanamgomo baridi wanavyofundisha kwa kinyongo ni hatari kizazi kijacho.
 
Kama ungesikiliza BBC Swahili leo ndio ungeelewa TZ did nothing kwa maadhimisho haya. Kama tumetumia 24b kufanya nothing kuadhimisha, jee tungeadhimisha inavyopasa, tungetumia ngapi?!.

Wana jf wenzangu, tusikalie kulalamika tuu na kulaumu kila wakati!. Sometimes tuwe positive kwenye baadhi ya issues sio kila kitu negative!.

Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi kusonga mbele!.
 
kama watoto waliokuwa wanaitwa halaiki( waliokuwa wanaonyesha matukio mbalimbali) yupo mdogo wangu wa kike wamepewa laki 1 kila mmoja na walikuwa 4550 kati ya hao 500 walitoka zanzibar, hapo tuu ni watoto wanaoweza kuzurumiwa kwa bajeti waliyopewa inawezekana ni zaidi ya hiyo, je walipangiwa ngapi kwani hiyo tu jumla ni 455,000,000, je watu wazima wasioweza zulumika wakiwemo polisi jwtz, magereza, wizara zote wameghalimu pesa kiasi gani??????
 
Kwa mujibu wa Ukurasa wa facebook wa Rithiwan Kikwete ni Bilion 24.7, huku hazina wakitumia zaidi ya bil 4. Dogo mwenyewe kashangaa hayo matumizi hali iliyopelekea watu wengi kuhoji ikiwa huyo ni Ridhiwan au amekuwa hacked kwenye wall yake.
 
Ningelikuwa na uwezo,
ningeliwafungia baadhi ya wanasiasa wasishiriki siasa kwa miongo kadhaa ili kuokoa kichache kilichopo.

Nilipita hospitali ya Mwananyamala juzi nikaona namna wagonjwa walivyolazwa sakafuni hata NET hawawekewi. Very sad.

Nilidhani maadhimisho haya yangeendana na ukamilishaji wa miradi ya muda mrefu ambayo hadi kesho inatengewa pesa bila kutekelezwa.

I love my country
 
eti tuna wabunge wanaisimamia serikali,ukijumlisha hizo posho pamoja na za wabunge tunge nunua dawati na dawa kiasi gani
 
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu kupitia kwa jamaa zangu pale hazina kujua gharama tulizoingia kwa kuandaa haya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..

Kwa haraka haraka bajeti nzima ya maadhimisho haya ni bilioni 24 na kinara wa matumizi ni hazina wenyewe ambao wametumia karibu bilioni 4.Gharama hizi zinahusisha posho za wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohusika kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru na hasa kwa kamati ya maandalizi iliyokuwa chini ya mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda....

Gharama hizi zingeweza kulipa kiasi kidogo cha madeni ya walimu ambacho kinafikia karibu bilioni 64..Je,hii imekaaje watanganyika?

Nawasilisha!!

Mkuu hesabu hii imejumuisha maadhimisho katika ngazi ya mkoa na wilaya?
 
Wao hawaoni shida maana sisi wenye nchi daily kulalamika badala ya ku-act.

Kama tumekereka Tuhoji kama warusi
 
Back
Top Bottom