Bajeti ya Tanzania inawaua wananchi wake kweupe......viroba vimeshika hatamu.

kuna jamaa yangu zamu yake ya kucheza pool table ikifika lazma atupie kiroba. et ndo inamsaidia kulenga. hafu hachanganyagi ata na xoda. kavkav tu.

jaribuni kuandika mambo yanayoeleweka. Xoda=?, kavkav=?
 
Hao wanakunywa hawajui kuwa zina madhara? Kama bia imepanda, huna uwezo wa kununua, acha. Waachie wenye uwezo. Kwani ni lazma unywe pombe?
 
banana,kimoraly,nyukiwine zinauzwa miatanotano nikipiga 3 tu ni 1500 tayari napata stimu..kwanza hizi zina ndizi ntakua nimeshiba na kulewa
 
maweee unaua wanao kisa ulabu asee hufai,kwani bia itakuwa bei gani kwa sasa
navyopenda bia ntaathirika sana kisaikolojia nahisi ntaahamia kwenye
mbege chubuku kimpumu maana wao bei itakkuwa chini asee

Bia!, hata iuzwe elfu kumi. Mimi nitakunywa tu. Bora watoto walale na njaa lakini mimi na kinywaji damdam.
 
haki ya mungu walahi nimechekena mpaka basi eti ndizi kuku
du taifa linaangamia yaani mtu anafanya kazi bila malengo kama sa 4 vijana wote
wanakuwa bwibwi maendeleo yanakujaje?
ulichokisema ni kweli viroba ndio vipo kwenye to ten kwa sasa na huku kaskazini kuna pombe inaitwa banana wine na kimorali vijana wanakunywa sana akiwa na 1100 anapata banana 2 na kiroba cha jogoo wao wanasema kala ndizi kuku vijijini siku hizi ikifika saa nne kama kaburi halijachimbwa huwezi pata kijana mwenye nguvu kwa ajili ya ulevi
 
Yaani mtaona wenyewe hali isivyo shwari. watu maofisini Hangover hazitoki kuanzia asubuhi mpaka saa12 jioni....ukifuatilia walikunywa viroba au pombe kali sana ambayo inauzwa bei rahisi

Haha ha ha aha, Ta Muganyizi bana, wewe si ndiye mpenzi namba 1 kabisa? Lakini hoja yako ni nzuri. Nafikiri wokovu wa kuacha pombe unahitajika, japo hata maji na soda ni bei aghari, mf. jana nimenunua maji chupa ndogo kwa shs 700. soda ni shs 700.

Kwa hoja yako, viroba bao ni nafuu hata kwa maji na soda! Tuache kunywe soft na hadi drinks, matokeo ni.....Drs wanafahamu!!
 
Kwa sasa Kiroba ndicho kina bei nafuu.................watu wataungua maini hadi basi
 
Hivi ni lazima kunywa?
Nyie ndo mnasababisha sirikali ishindwe kutafuta vyanzo vingine vya mapato.

Siri hii wanaijua serikali..........kama sio lazima kunywa mbona kwa sasa Dodoma wanaongoza kwa kuuza bia. Hasa muda huu wa bunge? Sehemu kubwa za posho za wabunge zinaishia kwenye bia.
 
Siri hii wanaijua serikali..........kama sio lazima kunywa mbona kwa sasa Dodoma wanaongoza kwa kuuza bia. Hasa muda huu wa bunge? Sehemu kubwa za posho za wabunge zinaishia kwenye bia.

kibaya zaidi posho zao hazijui PAYE ni nini! Yaani bongo ni mkanganyiko tu. Kweli ukifikiri sana mwishowe unarudi tena Pub kugida tembo, na kuendelea kuifanya sirikali isipate muda wa kufikiri vyanzo vingine vya mapato.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom