Bajeti ya SMZ ni bil. 412.6/- mwaka 2009/2010

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
834
Mwinyi Sadallah


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inatarajia kutumia Sh. bilioni 412.6 katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2009/2010.

Akitangaza mwelekeo wa bajeti, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame, alisema bajeti ya mwaka huu Zanzibar imeathiriwa na kudorora kwa uchumi duniani.


Hata hivyo, alisema wananchi lazima wajifunge mikanda kwa kushirikiana na serikali na wahisani ili kufanikisha utekelezaji wa bajeti hiyo.

Waziri Makame alisema katika mpango wa maendeleo, serikali inatarajia kutumia sh. bilioni 239.9 sawa na asilimia 58.1 wakati sh. bilioni 172.6 zinatarajiwa kutumika kwa kazi za kawaida kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ya serikali.

Alisema kiwango hicho cha matumizi ya kawaida ni sawa na asilimia 42.9 ya bajeti kuu ya serikali na bajeti ya mwaka huu imelenga kuinua kipato cha mwananchi wa kawaida kwa kuimarisha sekta ya kilimo na uvuvi wa bahari kuu.

Waziri Makame alisema serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUZA) unatekelezwa katika mwaka ujao wa fedha ikiwemo kuimarisha huduma za afya na elimu kwa wananchi wake.
Hata hivyo, alisema kutokana na tatizo la mtikisiko wa fedha duniani vyanzo muhimu vya mapato vitaathirika ikiwemo sekta ya utalii na uwekezaji wa mitaji kutegemea masoko ya nje.

“Athari za mtikisiko wa uchumi duniani, tayari zimeanza kujitokeza katika uchumi wa Zanzibar na shughuli zinazotarajiwa kuathirika ni zile zinazotegemea mauzo kutoka katika masoko ya nje,” alisema Waziri Mwinyihaji.

Kwa msingi huo alisema serikali imeweka kipaumbele katika bajeti hiyo ikiwemo kuimarisha sekta ya utalii na ujenzi wa miundombinu ili kuwawezesha wakulima na wavuvi kutumia masoko ya ndani kwa muda muafaka.

Hata hivyo, alisema pamoja na athari za mtikisoko wa fedha kuanza kujitokeza serikali inatarajia kukusanya Sh. bilioni 42.6 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani na Sh. bilioni 199.1 ni mapato yanayotarajiwa kutoka kwa wahisani wakati miradi ya maendeleo na misaada ya kibajeti inatarajia kuwa Sh. bilioni 50.2 pamoja na mikopo isiyokuwa ya kibenki inatarajia kufikia Sh. bilioni 3.5.

Waziri Makame alisema katika mwaka ujao wa fedha serikali inatarajia kutekeleza miradi 65 zikiwemo programu 22 katika mpango wake wa maendeleo kwa wananchi wa Unguja na Pemba.

“Nguvu za wananchi, wahisani na serikali kuu zinahitajika katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu,” alisema.

Hata hivyo alisema wahisani wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kusaidia kuongeza misaada ya maendeleo kama ilivyofikiwa azimio la Mexico katika kusaidia nchi masikini duniani.

Bajeti hiyo inatarajiwa kusomwa kesho katika kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati soko la ndani la Zanzibar likiwa limeathiriwa na mfumuko mkubwa wa bei za vyakula na kuathiri wananchi masikini visiwani.
NIPASHE
 
Kwa nini Zanzibar hawasomi Budget yao siku moja na nchi nyingine za Afrika Mashariki?
 
Nawapngeza kwa akili yao ya kuweka matumizi ya maendeleo makubwa kuliko ya kawaida. lakini inawapasa waangalie suala la kupunguza misamaha ya kodi kwani kuna sehemu nimeona kwua misamaha yao ni asilimia 70 ya bajeti, hii ni mbaya sana.
 
Kuna mwenye taarifa kuhusu bajeti ya Zanzibar (ilikuwa wasome bajeti yao leo)? Kuna nini kipya? kuna tofauti gani na ile ya Tanzania bara?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom