'Bajeti-ya-Mlalahoi' Safari Hii Izingatie VIPAUMBELE Gani Bungeni Dodoma?

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,190
Ndugu wanabodi,

Wahenga husema siku zote ni mwenye kuvaa kiatu ndiye ajuaye ni wapi hasa kiatu chake kinambana na hivyo ni wajibu wake huyo huyo kujua afanye nini ili kujinasua na uchungu kutokana na kiatu chake.

Ni kweli kwamba nyumba ya usemi huo wa wahenga wetu kuna busara na hekima kemkem isiopingika kwa vyovyote vile. Lakini ni bahati mbaya sana kwamba busara na hekima hizo miaka yote hutupiliwa mbali pindi shughuli ya kuandaa bajeti ya nchi yetu kwa kutumia kodi zetu.

Mwezi wa bajeti ya serikali kwa mwaka mpya wa fedha ndio huo umewadi, na safari hii tofauti na miaka mingine iliopita, walalahoi tumejiandaa kila kona ya nchi kujimilikisha bajeti ya 2012 / 2013 kwa kuzingatia vipaumbele vyetu wenyewe na si vipaumbele toka kwa viongozi huko serikalini.

Ni utamaduni mbaya uliozoeleka kwamba miaka yote WAJANJA hujifungia maofisini kutengeneza MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI ya serikali kwa jina letu LAKINI BILA HATA MTU MMOJA kupita katika vikundi vyetu mbali mbaali katika jamii ya Tanzania Je tunapendekeza

Wananchi pindi tu tunaposikia ya Bajeti ya Nchi inaanza basi hatuishi kusikia WAJANJA walivyojiwekea MITEGO YA MIRADI HEWA NA MIKONGAMANO ISIOISHA kama njia za kuhalalisha wizi wa kodi zetu bila kuvunja milango ya ofisi zetu kule hazina.

Naam, ni kipindi kama hiki ndipo mtu unapata kusikia kwamba viongozi mbalimbali serikalini hujipangia safari kibao nje ya nchi, 'ukarabati' wa majengo, mikutano ya serikali zima Ngurudoto kwa semina elekkezi, mikutano ya vyama binafsi kwa kutumia miundombinu ya umma kama vile jengo letu la ikulu, magari yetu na ndege zetu kwa maslahi binaafsi ya kikundi lakini kwa gharama ya walipakodi wa vyama vyote nchini.

Ndio, pindi zoezi hii inapoanza ndipo unapogundua kwamba kumbe wajibu wa sisi wananchi huishia tu kwenye kuchangia kodi kwa serikali lakini kwenye kupanga matumizi yake sisi huwekwa kando na mwisho wa siku maendeleo yanayozungumziwa kwenye bajeti mbalimbali hutokea kutokua na mguso kwetu wala tija maana miradi hiyo yote hayatokana na sisi huku mashinani na wala miradi hiyo haijibu vipaumbele vinavyotuhusu.

Sasa ili wananchi tuendelee tu kuonekana taifa la WALALAMISHI, je sisi wenyewe tungependekeza kuona vipaumbele gani vikizingatiwa kikamilifu katika bajeti hii ya mwaka mpya wa fedha? Binafsi mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo:

MAPENDEKEZO YA MAMBO MUHIMU KUZINGATIWA KATIKA BAJETI IJAYO:

1. Jumla yote ya bajeti ya taifa letu, zaidi ya asilimia 75 % itengwe makusudi kwa kutuletea MAENDELEO.

2. Gharama ya Utawala kwa kila wizara isizidi asimilia 15 % ya bajeti yake yote.

3. Bunge letu lihakikishe kwamba kigezo muhimu ya Wzara gani ipitishiwe bajeti yake ya fedha kwa kiasi kagi katika kipindi kijacho SHARTI izingatie ushahidi usio mashaka wa 'MAFANIKI KWA MTAZAMO WA WANANCHI' ambayo wizara husika imeweza kutuletea katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita.

4. Maendeleo na miradi mbalimbali itakayoorodheshwa katika bajeti ya safari hii SHARTI IWE NA USHAHIDI kwamba ni wazo kutoka kwetu sisi wananchi wenyewe huku mashinani na wala isiwe ni wazo ya maendeleo inayoletwa kutoka juu serikalini.

5. Wizara za Elimu, Viwanda na Kilimo ziwe na kipaumbele maalum kupewa bajeti kubwa (mara mbili zaidi ya kile walichokipata mwaka uliopita wa fedha) zaidi ili kusaidia kuchochea upatikanaji wa elimu kwa watu wengi zaidi na kuondokana na ujinga, ajira nyingi zaidi na kusaidia kutupunguzia umasikini na uhalifu, na kutufanya Tanzania kuwa ni taifa lenye usalama wa chakula cha ziada kwa wananchi wetu kwa kipindi chote cha mwaka huku tukipunguza uagizaji wa vyakula kutoka nje ya nchi.

6. Serikali ifanye MAKUSUDI ya kutupunguzia gharama sisi walipa kodi kwa:

(i) kupunguza wizara hadi kubakia 18 tu.

(ii) Kuondoa nafasi za Manaibu Waziri maana tayari kuna Katibu Mkuu na jopo kubwa la wataalam utumishi wa uma.

(iii) Kuondoa Kamati za Bunge zinazojirudia majukumu

(iv) Kuweka Ceiling Point au mipaka ya safari / kongamano / ambayo afisa yeyote serikalini HATAKIWI kuvuka katika kipindi cha mwaka wa fedha.

(v) Kwamba OVERSIGHT COMMITTEE zitakazokua zikifanya kazi za kutadhmini matumizi ya kodi zetu katika wizara na miradi mbalimbali nchini watakua ni wataalam tu na wala si wanasiasa ambao tayari ni wabunge.

Lakini ripoti ya chombo kama hiki ndicho sasa kitakachopelekwa kwa wabunge kupitia kamati husika na kwamba OVERSIGHT COMMMITTEE inaweza ikapelekwa mahakamani kujibu maswali endapo wananchi au wataalam kama wao katika eneo husika wataona kuna haja.

Expert Oversight Committee Reports (Quarterly Reports - ipewe points 45 %) pamoja na Maoni ya Wadau (ipewe points 65 %) husika kuhusiana na miradi mbalimbali ya serikali ndio sasa zipate kuwa ni misingi rasmi ya kuamulia wizara gani ipate ama isipate fedha zilizoombwa katika kipindi kijacho cha fedha. Kwa mtindo huu shughuli za serikali zitakua shirikishi zaidi, uwazi zaidi na kupunguza kero za ufisadi nchini kwa kiasi kikubwa.

Sasa ni jukumu letu sisi kama JF kuibwa mjadala kwa mapna na marefu zaidi kusaidia kuboresha uundwaji wa bajeti kwa faida ya walalahoi nchini. Je, wewe hapo nini maoni yako juu ya mbinu za kutumia kufanya Bajeti ya Mwaka wa Fedha ujao uwe ni wa kuendana zaidi na Vipaumbele vya Walalahoi na wala kutokugeuzwa kuwa ni 'Kipindi Rasmi Cha Mavuno yasio kheri kwa baadhi ya wajanja serikalini
 
Kila unaposikia wananchi tunapolalamikia umasikini uliokithiri nchini maana yake ni kwamba haturidhishwi na viwango vya maendeleo tunayopata kama vile barabara zuri, maji safi na salama, tiba njema na ya kutegemeka, mikopo kwa wanafunzi, pembejeo kwa wakulima bila pembejeo hewa, yote haya ni kwa sababu watu huwa hatuna muda kufuatilia kwa makini uundwaji wa bajeti ya taifa letu na matokeo yake WAJANJA serikalini hujitwalia fursa hiyo kujinufaisha wenyewe.

Je safari hii ungependa kuona maendeleo ya aina gani na kwa asilimia ngapi jimboni kwenu ili ziwe kama mambo ya kuzingatiwa kama vipaumbele katika bajeti tunayoitazamia?
 
Kabla yote bunge lijadili scandal ya vyeti vya kugushi kwanza. Hili la masoja is tip of an iceberg tu.
 
kalale kwanza,je lini tz pana bajeti ya mlalahoi? hapa ni bora liende tu,unaelewa maana ya bajeti? acha uzembe lete vitu vyenye kufikirika achana ndoto za bajeti.
 
Mkuu Hans79,

Umepatia kabisa; WaTanzania tunapoteza kweli kweli kwa faida ya MAFISADI wachache kwa sababu tu tunaamini BAJETI ni jukumu la akina wale -
BORA IENDE TU HIVO HIVO - na kwamba sisi letu ni kulipa tu kodi kwisha.

Sasa kama huo ndio ukweli wa mambo inakua vipi vilio vitande hewani kwamba HATUNA MAENDELEO na kwamba serikali haifai kama hatuwezi kufuatilia bajeti ya taifa kwa hatua zake zote?

Hili ni jambo nyeti mno kwa kuwa BAJETI NDIO MKATE WA TAIFA na tusipofuatilia juu yake ndio hivo wajanja kazi kujipakulia tani zao na mwisho wa siku tunasikia MAFISADI papa kila kona.

Je, taasisi huru mlizojisajili kutuelimisha na kutuhamasisha kuhusu uelewa juu ya bajeti ya taifa letu na faida zake kwa ajili ya uwajibikaji kwa walipakodi, kweli na nyinyi hapo mnakubaliana na mtazamo wa mwenzetu Hans79 hapa kwamba BAJETI YA TAIFA ni 'Bora liende Tu' ndivyo mnavyotuelimisha huko mitaani.

kalale kwanza,je lini tz pana bajeti ya mlalahoi? hapa ni bora liende tu,unaelewa maana ya bajeti? acha uzembe lete vitu vyenye kufikirika achana ndoto za bajeti.
 
Back
Top Bottom